Wewe mbona unatupangiaga kuamini kua Mungu hayupo
Kiranga
Hapana,
Hujanielewa.
Kila mara naandika hapa Kiranga kueleweka ni vigumu sana kwa watu wengi.
Kila mara (hata jana nafikiri) narudiarudia kuandika kuwa imani ni haki ya kikatiba na kiutu iliyo mpaka kwenye "Universal Declaration of Human Rights" tangu December 10 1948. Hiki kitu nakithamini mpaka nimekariri hiyo tarehe.
Nimeandika hapa mara kadhaa hata wiki hii kuwa mimi si mtu wa imani ila nitatetea haki ya mtu yeyote kuamini au kutoamini anachotaka, naelewa hii ni sehemu ya "freedom of conscience".
Nimeandika hapa mimi siamini Mungu na wala si Mkristo, lakini natetea haki ya Wakristo wa Rwanda kuamini wanavyotaka, wasiingiliwe na Rais Kagame aliyetaka Wachungaji wawe na digrii za vyuoni iki kuongiza makanisa.
Freedom of conscience ni haki ya kikatiba na kiutu.
Sasa hapo nimekupangia vipi kuamini Mungu hayupo?
Usichoelewa ni tofauti ya msimamo wangu kuhusu imani (huo hapo juu) na maongezi yangu ya falsafa, mantiki, kutafuta ukweli kuhusu hoja ya kuwepo Mungu.
Hapo kwenyw faksafa si imani, nakuja kwa facts, kwa uthibitisho, kwa ushahidi, kwenye suala la kifalsafa ambalo nimeshasema sina nia ya kumbadili mtu imani yake (kwa sababu tushaona hapo juu imani ni haki ya kikatiba na kiutu, bila kujali ni imani sahihi au si sahihi).
Sasa hapo utasemaje nataka kuwapangia cha kuamini?
Tatizo lako wewe, na watu wengi kama wewe, ni kwamba hamjui kufuatilia hoja kwa nuance na kutenganisha wapi mazungumzo ni ya falsafa, mantiki, uthibitisho, ushahidi, na wapi mazungumzo ni ya imani.
Hujaweza kutenganisha mambo haya mawili.
Ndiyo maana unapata tabu kunielewa.
Kama hata una uwezo wa kunielewa.