Cement Kwa sasa Tanzania uhitaji ni mkubwa sana sababu miradi mingi ya ujenzi na watu wengi wanafanya ujenzi.
Serikali inabidi kuingilia Kati kuzuia mfumuko wa bei na kusaidia viwanda viongeze uzalishaji zaidi.
Kwa sasa serikali inafanya kazi ya clearing kwenye material ya cement kupitia Tasac. Viwanda vinaagiza material ila bei ya ku clear ipo juu hivyo wao wanaongeza bei Kwa mtumiaji wa mwisho maana ni sehemu ya gharama za uzalishaji.
Kama serikali itapunguza tozo kidogo hata Kwa kipindi cha miezi 6 Kuangalia matokeo yatakayo kuja kuanzia waagizaji, uzalishaji na bei ya mfuko wa cement Kwa mtumiaji wa mwisho. Pia itasaidia viwanda vya cement saizi ya kati kuagiza wenyewe meli ya material ya cement (clinker) na uzalishaji kuwa mkubwa.