Wapambe siku zijazo: Rais Samia ni jembe ameukataa mkataba wa bandari

Mwenge ni uchawi mbaya sana
 
Hii nchi shida kuu ilianzia baada ya ccm kuingilia kila mamlaka na taasisi,na kumpa rais nafasi ya uwenyekiti wa chama,hapa ndipo tulipokwama. Katiba mpya muhimu sana.
Kabisa, na ilikuwa kosa kubwa la kiufundi kuruhusu chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu. Automatically unaporuhusu chama kimoja kuhodhi madaraka muda mrefu hata kwa njia chafu, unasababisha udhaifu wa mifumo yote ndani ya nchi hiyo. Hali hiyo hupelekea kikundi cha watu wachache kuamua nchi iendeshweje na sio kwa sera. Bila katiba mpya sioni mabadiliko ya hali hii, na uwezekano wa kupata katiba mpya ya maoni halisi ya wananchi kwa njia ya amani siuoni.
 

Mzee Said, huu ni mkataba au makubaliano? Nijuavyo mimi mikataba nchi hii ni siri. Weka mikataba, au kama unaweza lete mkataba au makubaliano kwa lugha ya kiingereza waliyonao DP World. Achana na hizi story za mikataba kwa kiswahili, huku ni kupotezana maboya.
 
Acheni wizi mtafika mnapotaka la sivyo mtaishia kuteseka huku mkicheka kama wehu huku mnaumia

Kuendesha nchi sio kama baiskeli
Kuna watu nyumba zinawashinda kupanga bajeti na anajiibia mwenyewe itakuwa nchi na rasilimali zake?

Matapeli kila kona halafu mnataka mjiendeshe bollocks
 
Tindo,
Tuko mahali pazuri.

Wako wanaouliza tutakwenda hivi hadi lini?

Tatizo mkataba au Waarabu?

Vipi kuhusu ule mkataba wa Serikali na TEC/TCC?

Tunaweza kuujadili?
 
Tindo,
Tuko mahali pazuri.

Wako wanaouliza tutakwenda hivi hadi lini?

Tatizo mkataba au Waarabu?

Vipi kuhusu ule mkataba wa Serikali na TEC/TCC?

Tunaweza kuujadili?
Mzee, usiingie ktk mkumbo wa kimtandao. Tatizo siyo mwarabu. Ingekuwa tatizo mwarabu. DPW asingefukuzwa nchi zenye nasaba kubwa na waarab kuliko Tanzania. Nakuomba jiepushe na hii kadhia ya kuona tatizo ni uarab wa DPW au uislam wa waarab wa DPW. Kwa kuwa DPW kafurushwa Somalia. Je Tanzania kama nchi inashika uislam kuliko Somalia?

Kuhusu Tanzania na mikataba na taasisi za makanisa hili linawezekana kujadiliwa kabisa. Kwanza tujadili ukomo wa haya makubaliano ya URT na hizo taasisi. Na ikiwezekana kama hayana tija kwa serikali tuvunje hayo makubaliano. Simple. Lakini tusiingie ktk tatizo kisa kuna mtu alikosea pahala.

Tuyatafakari haya.
 
Alianza vizuri sana.

Alipoanza kukizoea kiti na kunogewa na Utamu wake akaanza kuharibu.

Ngoja tuone mwisho wa muvi itakuwaje.

Muda ni mwalimu mzuri, utatuambia kikubwa RISITI zake ziko mtandanoni maana internet haisahau.

Tutamkumbusha siku akija kurepent kwamba tulimwambia aachane na huo umangungo.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Isije ikawa wamerudisha mpira kwa kipa halafu wajipange, kisha walisongeshe kimya kimya., maana kama walikula hela za wajuba itakuwaje.
 
James...
Usitumie neno "kufurushwa," linatoa sura ya chuki.

Nchi nyingine waliyofukuzwa ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…