Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Duh. Aiseee harakati za King 👑Haaaa haya sirudii tena Marie.
Alafu ukome kunitongoza PM
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh. Aiseee harakati za King 👑Haaaa haya sirudii tena Marie.
Alafu ukome kunitongoza PM
Hahahaa embu ondoa njaa njaa zako hapaHakuna mwana JF mwenye pesa kama mimi
Duh. Aiseee harakati za King 👑
Ninadhani lingekuwa ni jambo la maana kama ungemsaidia na kiasi kidogo cha pesa badala ya kumkejeli huyo ndugu hapo juu.Hahahaa embu ondoa njaa njaa zako hapa
Mkuu, unajua huyo katika avatar yako alikuwa Police?Hana lolote huyo dada ni mayala tu
Polisi katika sakata la mauaji ya akina Zombe. Mjaluo huyo jamaa.Mkuu, unajua huyo katika avatar yako alikuwa Police?
Ushauri mzuri sana huu mkuu kejeli hazimjengi mtu bali zinamuua kisaikolojia.Ninadhani lingekuwa ni jambo la maana kama ungemsaidia na kiasi kidogo cha pesa badala ya kumkejeli huyo ndugu hapo juu.
Kuna swahiba anafanya kazi na wachina km mkalimani, anakula mshahara wa 2million .. kichina kwa sasa ni diliWachina wamejaa sana kariakoo alafu unasema lugha yao haina dili?
Badala ya kumzodoa, kwanini usimsaidie akaondokana na hizo njaa?Hahahaa embu ondoa njaa njaa zako hapa
Pesa zitatoka wapi usawa huu? Ngoja labda Rais mama Samia anaweza kulegeza kamba kidogo.Ninadhani lingekuwa ni jambo la maana kama ungemsaidia na kiasi kidogo cha pesa badala ya kumkejeli huyo ndugu hapo juu.
Mbona na wewe kama unaonekana ni njaa njaa tu?Hahahaa embu ondoa njaa njaa zako hapa
Acha ubishiMambo mtambuka ulipo kuwa na miaka 10 unayakumbuka.
Bill gate alikita kujua software akiwa mtoto, wewe unataka mtoto wako ajue mambo mtambuka, yamsaidie nini?
Life skill ndio muhimu kwa mtoto.
Kujua kila kitu ndio imetufanya tusiwe na watu waliobobea kwa undani. Tuige wazungu,wachina wanaanza kufundisha vitu kwa umakini matokea yake wanazalisha watu makini wanaokuja kututawala Africa.
Just imagine miradi mikubwa barani Africa inajengwa na wachina,wazungu na warabu,.why? .
Waandae watoto wko katika ulimwengu wa ushindani.
Iga Bill gate mkuu hakujua kla kitu zaidi ya business of cimputer.
Anaitwa afande Bageni alikuwa OC-CID KinondoniMkuu, unajua huyo katika avatar yako alikuwa Police?
Kuna watu hawana shukrani mkuu, yani unawasaidia leo kesho wanaanza kukucheka weweBadala ya kumzodoa, kwanini usimsaidie akaondokana na hizo njaa?
Uzi bomba Sana!Habari za wakati huu jamiiforums
Stories nyingi sana za KGB na zile zingine ambazo ninaandikaga kule jukwaa la jamii intelligence ni zile ambazo nilizisoma mwaka 2006 nikiwa kidato cha sita. Kipindi hicho hakuna smartphones lakini nilikuwa ninaiba muda kisha ninakwenda internet cafe moja iliyokuwa inamilikiwa na mama wa rafiki yangu maeneo ya Chang'ombe kule Keko wanapaita TAMECO.
View attachment 1758988
Baba yangu alikuwaga ni mtumishi wa serikali. Alifanya kazi muda mrefu sana katika viwanda vilivyoanzisha na mwalimu nyerere ila kwa bahati mbaya akaja kupata redundancy baada ya kiwanda kile kufa mwaka 1993 kama sijakosea na kuamua kuingia katika kujiajiri hivyo na kuwa na muda mwingi sana wa kukaa na sisi watoto wake baada ya kazi.
Mzee alikuwa anatupigisha stories nyingi sana za masuala ya siasa za wakati huo wa ujamaa, ushawishi wa nchi ya Russia katika Africa hivyo nikatokea kuipenda sana USSR pamoja na sera zao za ujamaa.
Ilifika kipindi mzee alikuwa akitoka katika shughuli zake za kujiajiri alikuwa anakuja na magazeti kisha anatupa tuyasome alafu baadae kabla ya kulala anaanza kutuuliza maswali mmoja badala ya mwignine na hiyo ndio iliyonijengea mimi kupenda kusoma vitabu.
Nimeamua kuanzia mbali kwa kuwaelezea story fupi ya maisha yangu baada ya kukutana na statement hii ya huyu bilionea wa kichina bwana Jack Ma katika moja ya magazeti ya online. Jack anasema hivi "I told my son: you don't need to be in the top three in your class, being in the middle is fine, so long as grades are'nt too bad". Only this kind of person has enough free time to learn other skills.
Kwa kweli hii ni kinyume kabisa na mifumo mingi ya elimu katika nchi tofauti hapa duniani na Tanzania ikiwa moja wapo. Katika mifumo mingi ya elimu hapa duniani, lengo pekee ni kuweka kila kitu pembeni na kulenga tu kwa mwanafunzi kupata alama bora zaidi darasani. Kupata As pamoja na Bs.
Na katika hali nyingi ujuzi uliojifunza nje ya darasa hauhesabiwi hata wakati mwanafunzi anapotaka kujiunga na elimu ya vyuo vikuu. Kwa hivyo, dhana hii hutoa hitimisho kwa mwanafunzi ya kuwa stadi za maisha isipokuwa zile zinazofundishwa na shule sio muhimu kabisa na njia pekee wanayoweza kutumia katika kufaulu ni kupitia kupata alama bora za darasani pekee.
Mwaka juzi wa 2019 nilipata kusoma kitabu fulani kuhusiana na maisha ya huyu tajiri wa China (Hiki kitabu nilipewa kama zawadi tu). Licha ya ukweli kwamba Jack Ma hakuwahi kuwa miongoni mwa wanafunzi watatu wa juu (tatu bora) wakati wa maisha yake ya shule enzi hizo, lakini aliweza kuifanya Ali Baba kuwa moja ya kampuni ziliyofanikiwa zaidi kwenye masuala ya biashara za mtandaoni hapa ulimwenguni.
Na hiyo ni hadithi moja tu kati ya hadhiti nyingi sana zaidi ya mia moja kama hiyo ya wajasiriamali wengi wanaoongoza na wavumbuzi wakubwa hapa ulimwenguni ambao hawakuwahi kupata alama nzuri saaaana ila bado mpaka sasa wanaongoza makampuni makubwa na yenye mafanikio ulimwenguni.
Kulingana na taarifa nilizonazo ni kwamba Jack Ma mwenyewe anataja kwa nyakati tofauti kwamba yeye mwenyewe alishindwa mara 3 wakati wa mitihani ya kuingia chuoni.
Kwa hivyo haijalishi ni As au Bs ngapi mtoto wako anaweza kuzipata ila anapojifunza masuala mbalimbali mazuri pamoja na masomo yake mara kwa mara basi unakuwa unampa exposure nzuri ya kuja kuwa mtu wa maana hapo mbeleni! Na kumbuka stadi hizi zinaweza kuwa kitu chochote kuanzia kujifunza jinsi ya kuwasiliana na watu wa rika tofauti mpaka kujifunza lugha za kigeni kama kifaransa.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
AsanteUzi bomba Sana!
Nilisomaga na mtoto wa kaka yake pale UDSM. Jamaa yupo vizuri sana kichwani.Polisi katika sakata la mauaji ya akina Zombe. Mjaluo huyo jamaa.
Alikuwa JWTZ sio PolisiMkuu, unajua huyo katika avatar yako alikuwa Police?