Wapi mnapata pesa za kujenga wandugu? Mbona kwangu naona chenga tu?

Wapi mnapata pesa za kujenga wandugu? Mbona kwangu naona chenga tu?

Duh! We mzee ni mchakarikaji kama Mazaa ako. Una akili nzuri lakini Huna maamuzi. Ulitakiwa usiwe na mwanamke pamaneti kabla hujayafikia malengo ya msingi. Kwa mwaka 2017 ungeweza kupata kiwanja Mbagala KISEWE kwa milioni 2 ulizokuwa nazo. Halafu ungejenga urafiki na Mangi wenzio ili uwapate akina Manka. Ungeweza kusogea.

Hata hivyo, bado hujachelewa; toa NOTICE ya kumuacha huyo mwanamke na mwachie kila kitu. Kwani sh ngapi? Umepata fundisho, ANZA UPYA nebuchadnezzar

Nzuri sana hii
 
NImegundua kwamba wazaliwa wa chuga hawaoi, wao ni sogea tuishi tu..tabia mbaya sana.
Pole lakini, endelea kupambana
Kwani kuoa ni nini?? Unasubiri matarumbeta??mkishaelewana na kukubaliana na mwnzako wazazi wakawatambua ni ndoa tosha!!tupo nje ya muda

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuoa ni nini?? Unasubiri matarumbeta??mkishaelewana na kukubaliana na mwnzako wazazi wakawatambua ni ndoa tosha!!tupo nje ya muda

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Matarumbeta ni harusi.
Nimezungumzia ndoa.
Kuchukuana tu na kuishi huyo hajafata taratibu za wazazi wake. Angekuwa amefata taratibu asingesema kwamba wamefanya sogea tuishi.
 
Matarumbeta ni harusi.
Nimezungumzia ndoa.
Kuchukuana tu na kuishi huyo hajafata taratibu za wazazi wake. Angekuwa amefata taratibu asingesema kwamba wamefanya sogea tuishi.
Kuoa ni makubaliano ya pande mbili kati ya mwanaume na mwanamke sasa hivi watu wanaoana wawili na mchungaji wa 3 au hujaona watu wanaoana kwa kuptia mtandao yani mchungaji yupo mbali anaongeza ibada ya harusi.
 
Kuoa ni makubaliano ya pande mbili kati ya mwanaume na mwanamke sasa hivi watu wanaoana wawili na mchungaji wa 3 au hujaona watu wanaoana kwa kuptia mtandao yani mchungaji yupo mbali anaongeza ibada ya harusi.
Najua.
Hao hawajaenda kwa mchungaji. Unajua maana ya sogea tuishi?
 
Kabla ya kuingia kwenye ndoa muwe mnawaona waonaji wanaona ndani mtu alivyo kama ni sahihi au garasa thus wahindi na waarabu hawaowani hovyo just tu mnafanya mazoezi pamoja kitandani.
Pana watu wamebeba laana na mikosi utoboi,
 
Tulsa zipo chache bro, serikalini mpaka sekta binafsi, hatuna ajira(kipato kuanzia milioni)za kuwapa vijana wote wanaohitaji, kenge wa, CCM wanafikiri kwa, kutoza Kodi na, kuongeza, Kodi, ndio wataleta maemdeleo ya viwanda,
Nchi inakuzwa, na viwanda(manufacturing industry) sio uchuuzi wa bidhaa kutoka china unaofanywa na wafanyabiashara wengi.
Hata Freddy vunjabei, anafanya uchuuzi tu, unanunua bidhaa kutoka china, una kuja kuu za bongo, haina tofsuti na mama zangu wanaonunua samaki ferry na kwenda kuuza kitaa, wanapata pesa,lakini fikiria nguo,tv, friji, radio, viatu vyote vinavyoletwa kutoka china na kuuzwa kariAkoo , vingekuwa vinatengenezwa hapa bongo, faida ingekuwa, kubwa
Umeme na Kodi ni kikwazo
 
Inaendelea..

Inaendelea....

Jamaa akaniambia mfuko dazen 1 ni 1200,na mfukoni nilibakiwa na 3000 nikanunua mifuko,ilikiwa ni ile meupe mikubwa,basi nikaanza kuuza mifuko nikiwa na begi langu mgongo kweli siku hiyo nilipambana kwanzia saa 1 asubuhi mpaka saa 8 mchana nikauza dazeni 2 faida nilipata 2400.

Katika kuuza mifuko nilijuana na vijana mwenzangu waliotoka maeneo mbalimbali hapa tanzania,ila asilimia kubwa ya hao vijana walikuwa waluguru na wasambaa ila siku bahatisha kukutana na mchanga yeyote,ni mimi pekee ndo nilikua mengi siku hiyo hiyo wakanipa jina la mangi maana nilikua chapu tu pale niliposikia mtu anaitwa mfuko.

Wale jamaa wakanipa mbinu za kupiga pesa,wengine aliniambia kwa siku wanaingiza 15000 mpaka 20000 nilishangaa sana,wengine waliniambia wameoa na wanamaisha yao,ila walinipa mbinu za kutusua kama hao,basi wakaniambia natakiwa niwe mchafu kwenye nguo nazovaa ziwe zimepauka zikiwa na vumbi la magunia,mbinu nyingine wakaniambia niwe mjanja pale napowaona wanaokuja kununua vitu niwe nakaa karibu nao,maana wengine hununuaga vitu vingi na hutafuta watu wakuwabebea.

Basi nikasepa zangu gheto,siku ikapita.

Kweli asubuhi nikawahi sokoni nikiwa nimechafuka kama porter wenyewe wa mabibo,mzee asikuambie mtu kweli siku hiyo nikauza dazen 4 na nikabebea watu mizigo na kuwapelekea kwenye magari ya goba,mbenzi,kwa rusungu,tegeta n.k hapo hapo sokoni kuna pickup huwa zinawapelekeaga wafanyabiashara wamagengeni mahali wanapofanya biashara zao.

Kweli siku hiyo nikaingiza 8000 nilifurahi sana,nikaanza kufahamika na kukubalika mabibo sokoni,nilikuwa sichagui mzigo,matango,nazi,majimbi,ndizi viazi,tangawizi hadi dagaa nilikua na nguvu mpaka wakawa wananishangaa,waluguru ndio walisifika kwa kubeba mizigo minzito ila wenyewe waliniwanzia mimi.

Nilipambana mabibo nikawa siunzi tena mifuko nikajiingiza kwenye UKULI.
Wengi tunapitia hayo na mengine ni mazito zaidi ya hayo....lakini suluhisho ni roho...kama ukiweza nenda kkkt kimara korogwe....Mungu atakusaidia.
 
Tunapenda kuoa ila wanawake wengi akili hawna,ukijifunga kwenye kuoa kaa ukijua umedumbukia kwenye tanuru la moshi,na majuto yake utayaona baadaye.
Kwani ujawasikia wanandoa wameuwana??
Hasa wanawake wengi wa Kikristo hawajitambui wao wanapenda zaidi Harusi kuliko ndoa.
Waislamu wamepewa option akikusumbua fukuza kama una huruma oa mke wa pili,watatu hadi umpate mtulivu.
Ukristo labda uishi nae uchumba sugu
 
Ndio maisha yetu vijana yalivyo story yako imefanana na ya yule jamaa ambaye ni mwenyekiti wa mabaunsa Dar es salaam.
 
Imepita siku kadhaa toka niandike huku,wengine walitaka muendelezo ila kwa kuwa nilikuwa bize sana sikuweza kuandika.
Kusema kweli kama nilivyosema huko mwanzo mimi ni hustler sana,kwenye swala la kutafuta pesa sinaga haibu na utani kabisa,
Baada ya kusoma comments zenu humu nilipandwa na mzuka wa kusaka pesa kwa njia yoyote bila ya kumtoa mtu roho,nimegundua mtu usijionee huruma ikane nafsi yako.

Kama nilivyosema mwanzo nilichokiandika kina uhalisia wa maisha yangu sijatunga chochote haya ni maisha yangu fo real.
Week 2 zilizopita kuna biashara nimepiga ya magendo na nihatari sana,nimegundua biashara zote hatari zina pesa nyingi.


Hiyo biashara siiwezi kuitaja hapa.......


Baada ya kupiga hiyo biashara nimeipata pesa nikanunua robo heka ya kiwanja huko pwani,
20231101_122114.jpg

Hii ni hati ya kiwanja changu.
Nmenunua tarehe 29,MUNGU NI MWEMA SANA
 
Back
Top Bottom