Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Wacha ni kwambie ndugu yangu, pale Kenya wana katiba mpya ya kisasa kabisa, Wana mahakama yenye nguvu kabisa na Wana bunge imara, lakini hiyo haimaanishi kuwa Kenya wana hali nzuri kuliko sisi, pale Uganda na Rwanda Wana Rais huyohuyo miaka nenda Rudi lakini hiyo haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi tunaobadilisha Marais kila miaka 5. Uarabuni hakuna uchaguzi Kuna masulutani lakini haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi ambao tunachaguana kila miaka 5.

Shida yetu ni zaidi ya katiba mpya bro, think outside the box. Wanacholilia wapinzani ni wao pia wapate nafasi ya kula. Mfano, chadema walisusia uchaguzi na hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020, lakini Sasa hivi wanaona tabu akina Halima kuwa bungeni kwa kutumia janjajanja Yao. Wanataka akina Halima wafukuzwe ili wapeleke watu wao kwenye bunge ambalo hao wamelisusia.

Haohao wapinzani mnaweza kutumia nguvu zenu kubwa kuwachagua lakini wakaenda tena CCM kwenda kuunga juhudi. Watu walifanya hivyo tangu enzi zile za akina Lyatonga, mabere, lamwai, mkumbo, tumbili, selasini, sumaye, lowasa, mwita, nk. Ni mpumbavu TU ambae atapoteza nguvu na rasilimali yake kwa kumchagua mpinzani ambae hatabiriki na Wala Hana alama ya kuonyesha kweli ni mpinzani wa kwelikweli.
Elimu yako ni ndogo sana au iko kwenye makaratasi tu lkn kichwani hakuna kitu.
 
Wanasiasa wetu wa upinzani wanahangaika na matukio badala uhalisia wa mambo kwa ujumla wake. Wanalalamika bila kutoa suluhu nini kifanyike. Walipaswa kuandamana baada ya ripoti ya CAG kuhusu umbadhilifu, walipaswa kuandamana kupinga ukosefu wa pembejeo kwa wakulima na wafugaji, walipaswa kuandamana kupinga ukosefu wa maji kwakuwa hitu vyote hivyo having uhusiano na katiba mpya. Maana katiba ya Sasa haizuii watu kupewa maji, chakula, elimu, mishahara mikubwa Wala ajira. Badala yake wanahangaika na Rais anaetaka kufanya mapinduzi kwenye bandari, maji, umeme, usafirishaji, michezo nk. Hakuna mwananchi mwenye akili atakaewaekewa. Hizi ni jitihada za wivu na kutaka kuingia Ikulu na wakishafika Ikulu wanakenua TU. Ruto alililia kwenda Ikulu na akafika Ikulu, je, wakenya wanapata ahueni gani chini ya Ruto? Ndugu zangu tatizo letu sio katiba Wala Chama tawala, bali tatizo letu ni zaidi ya katiba na Chama kilichoko madarakani, tusiwafanye watu kama vile hawana akili. Ukimuuliza mwananchi wa kule nanjilinji kuhusu bandari atakushangaa sana. Wewe muulize habari za umeme, dawa, barabara, masoko, maji ya kufulia nk.
Maelezo yako ni sahihi kabisa lakini unakosea sana unaposema eti Katiba mpya inahusiana nini na hayo matatizo 😅😅 !!

Unataka waandamane ili wavunjwe migongo. ??!! 😂
 
Hawasemi watafanya nn kwenye bandari ili isihamwe na wateja, watatoa wapi matrekta ya kuwapa wakulima walime saidi, watafanyaje kuwaondoa machinga barabarani. Wanalalamika tu
Tatizo linaanzia hapo
 
Blah Blah za Bandari ndo mpango mzima.

Hoja zingine zisubiri kwanza maana hayo yote yametengenezwa na CCM ili yatumike kuombea kura
Mwanasiasa, mwanasheria na mbunge mwenye akili na busara mara zote na kila wakati siku zote huwa anatenda kwa mujibu wa Katiba ya nchi yake na nchi aliyomo. Hatakiwi kuyasahau mamlaka ya watu, taasisi na vyombo mbalimbali vilivyotajwa na Katiba hiyo.

Wanasiasa, wanasheria na wabunge bila shaka wanafahamu ila wanasahau nguvu za kikatiba za Rais, waziri, Mkuu wa mkoa na wilaya. Hawapaswi kusahau hata siku moja juu ya ukuu na nguvu za Rais na mwenyekiti wa CCM alizopewa kihalali na Katiba ambazo zinamsaidia katika kutimiza majumu yake ya kila siku katika nyakati mbalimbali kutoka zile za kawaida, za hatari, za njaa, za kiangazi, za fujo, za uchaguzi, za upotoshaji, za maandamano ya hovyo na Yale yenye tija, za michezo na hata zile za vita. Rais Magufuli alisema sibadili Katiba ng'o, Wacha niitumie katiba hiihii kuinyoosha nchi kwanza, na alifanya hivyo kweli. Katiba hii ilimsaidia na kumwezesha kuwateua akina Mama Samia kuwa Makamu wake, akina Gambo, Makonda, Sabaya, mkuu wa majeshi, IGP, na kila mtu kuwa wasaidizi wake. Ilimsaidia kwenda Dodoma kibabe, kujenga ukuta melelani, kujenga SGR, bwawa la umeme, barabarani na vivuko. Ilimsaidia kuwanyorosha vijogorokwinyo vilivyotaka kumchelewesha kwenye safari yake kwa kulala njiani. Aliyatumia mamlaka yake kuzuia makinikia, kununua ndege kibabe ambazo Leo hii tunajivunia nazo kupanda kwenda Algeria moja kwa moja bila kutua popote. Swali langu la msingi ni kwamba je, Rais Mama Samia hanazo hizi nguvu pia? Je, Hana nguvu ya kubinafsisha bandari ili ifanye vizuri? Je, ni kilaza sana kiasi Cha kuiuza nchi?

Tusimchukilie powa Mama maana katiba waliyotamba nayo viongozi wengine na CCM waliopita haijabadilika ni hiihii, tusije kilazimisha kuubadilisha mjusi kuwa nyoka.
 
Mambo ya hovyo tasipopatiwa ufumbuzi husababisha njia za hovyo kuyakabili
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi vya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo.
Watoe wapi wazee wa matukio hao,hii ya upotoshaji imebuma Sasa wakizido Ili walete vurugu watadhibitiwa maana wanatumia uhuru wao vibaya
 
Niambie siasa za wapi za sasa zinazoongelea mambo ya ujumla wake waliopo madarakani wanatetea kila uozo wao (kwa cost kubwa sababu tunawalipa) wapinzani wana-attack ili wao waingie kwenye ulaji (at least the latter hatuwalipi wala sio kazi yao kuweka mambo sawa kwa wakati husika)

Ni kazi yao kutoa Suluhu; na Suluhu ikitoka itafanyiwa kazi ? Na kama by design wapo pale ili waongoze unategemea watatoa suluhu ili hawa watekeleze hence wao wasiingie kwenye ulaji; Ndio maana nikasema mwisho wa siku ni wananchi wenyewe kwa umoja wao ndio wanaweza kujikomboa..., Ila kwa waliopo madarakani sio Hisani wala hizo mali sio zao ni za wananchi wote (Kwahio inabidi wanchofanya kwa niaba ya wananchi isiwe siri - we need transparency) sio kuja kuambiwa baada ya miaka kadhaa kwenye vitabu vyao kwamba waliteleza... De Ja Vu...

Issue za Katiba Mpya ni debate nyingine siku ukianzisha niambie ili nije nijazilizie hapo; Issue za kuandamana walishaandamana mara ngapi na nini kilibadilika ? Sanasana inapigwa propaganda kwamba hawa watu ni wafanya fujo ? Na je ni jukumu la wapinzani kuandama kwa ajili yako au hao wakulima na wafugaji kwa ukosefu wao wa pembejeo wapige kelele wasikike - Kwahio wewe unaona waliofanya kosa ni wale ambao hawakuandamana mambo yalivyokwenda mrama na sio waliosababisha mambo hayo kwenda mrama ?

Kwahio hayo mapinduzi umeyaona wewe na wenyewe hawajayaona wala hawahitaji kuhoji ? Kwahio huyo huyo anayetaka kufanya mapinduzi hausiki na madudu ambayo umetaja hapo juu amabayo umeshauri wapinzani waandamane kwa kuyapinga ? Kwahio tumuamini vipi huyu aliyeshindwa kutatua hapo juu kwamba anachofanya sasa (bila kushirikisha wananchi wote) kwamba ni jambo jema; tunajuaje kama anayofanya sasa sio madudu kama yanayosemekana yalitaka kufanyika Bagamoyo ? Si ni watu walewale ambao hapo nyuma wametuingiza kwenye shida ? Iweje leo waaminike ? Kwanini kila kitu kisiwe wazi ili tuelewe huko anakotaka kutupeleka kama panafaa ?

Unachanganya madesa even a Broken Clock is Right twice a Day..., hata kama wapinzani ni mashetaki mwenye busara anaangalia ni nini kinasemwa wakati huo na hata kama Watawala ni Malaika haimaanishi kila kinachowekwa mezani kimezwe tuanze kuchanganya issue utetezi wa kuongelea maisha magumu hakumzuii mtu kuongelea Bandari (in their defence na wao walivyoona ugumu huo wa maisha utazidi iwapo hata mandate ya hii commanding height yetu tutawapa watu na kutegemea hisani yao na goodwill kwamba hawatatuibia wakati tulishindwa kuwahimili wengine ambao kisheria tuliweza kuwakagua (hawa huenda hata kuingia ofisini kwao hautaweza)

Tatizo letu ni kubwa wala dawa yake sio moja; ila Chama Tawala ni moja ya Tatizo, hizi policy zote ni chama tawala; Chama Tawala kimeleta Tozo na kufanya watu wapunguze kutuma miamala; Chama Tawala kimepandisha Bundle kwa policy mbovu; Chama Tawala kinacheza siasa na wakulima leo msiuze nje kesho muuze; Serikali kwa matozo lukuki hadi mafuta ni bei juu; Sarakasi za waliopo sasa za kutafuta Crane n.k. Bwawa limechelewa kuisha; Unadhani nani ana mandate au kazi ya kuhakikisha maji, Umeme na Pembejeo zinafika panapofika ? Unadhani hata ukiagiza bidhaa kutoka China kwa Ndege ikafika hapa wakapiga Ushuru 60% hio ni sababu ya Bandari au kukamuana Kodi ambapo value for money haipo....

Kwamba hajui Bandari ndio inayosababisha kuleta mizigo au vitu vinavyoenda nje vinapatia pale au kwamba kukiwa hakuna security madudu yoyote yale yanaweza kupitishwa pale ? Hajui hayo yote ? Hata kama hajui mbunge wake inabidi ajue na afanye chini juu welfare yake huyu mwananchi na wajukuu wake iwe taken care of...

Na yote hayo haya connection na Chama Tawala wala matumizi bora ya Mali za Nchi kama vile Bandari ? Na kama hao wameshindwa kupeleka dawa, barabara masoko na hata kutoa maji sentimita mbili wataweza kumsimamia mtu ili asiibe au kufuja na kuiba katika utendaji wa bandari ?
Tatizo lako unafikiria mambo kwa vipandevipande (not integrated). Wewe huna ushahidi kuwa unapopinga uwekezaji huu unawawakilisha akina nani ambao wako wangapi na raia wa wapi. Kwa mujibu wa Katiba yetu tumekubaliana kuwa wabunge pekee ndio wamebeba agenda, mawazo, na matakwa ya watanzania wote, kwenye hili wananchi kupitia wabunge wao wameukubali uwekezaji huu. Kwa mujibu wa Katiba tuliyoapa kuilinda Mjadala huu umefungwa tangu pale wananchi (bunge) walipouridhia. Chochote kile nje ya hapo ni ukuwadi, utwezaji wa bunge (wananchi), uvunjaji wa Katiba, dharau kwa serikali, nuisance, na kusababisha mkwamo kwa serikali. Adhabu za makosa kama hayo sio za kupapasa, lazima utashindwa TU maana wananchi kupitia bunge lao wameshaamua, wewe unaepinga ni nani kwa maslahi ya nani?
 
Mkuu unafuata hata mtiririko wa mawazo yako mwenyewe kichwani au unajipinga mwenyewe....

Kwa mtizamo wako chochote kinachopitishwa Bungeni ni wananchi ndio wamesema na ndicho wananchi wanachotaka; Sasa unavyowaambia hao wapinzani wapeleke hoja nzito kwa wananchi (yaani kwamba kuna madudu yanayohitaji kuzungumziwa) huoni kwamba unajipinga mwenyewe iwapo wananchi hao (wabunge) wanachopitisha na wanachofanya Bungeni ndio wananchi wamefanya ?

Na katika kujibu kwako hapo nyuma ukasema wananchi hawahitaji katiba wala nini wanahitaji maji, umeme n.k. - Sasa huo umeme si wamekubali unavyosambazwa na wanavyopata kulingana na bajeti na sera ambazo zinapitiswa Bungeni ?

Mi nadhani kwanza nikupe muda uweze kuji-convince mwenyewe unataka nini au unazungumzia nini alafu tuendelee utakapokuwa na uamuzi na sio flip flopping....
 
HOJA GANI YA MANUFAA ZAIDI YA KULINDA ARDHI YETU ISIUZWE NA WAKUJA?
Bunge letu ndicho chombo halali Cha kuwawakilisha watu wote, na bunge limeuafiki mkataba, je, nyie mnamwakilisha nani? Hetu toa orodha ya watanzania wasioukubali huu mkataba. Sisi watanzania tuliowengi kupitia wabunge wetu bungeni tumeuafiki mkataba, tuna wasiwasi kuwa nyie mnaopinga mnatusaliti, mnaungana wa wezi wa bandarini na watu wa bandari nyingine za Kenya, Angola, msumbiji na Durban ili mradi huu isifanikiwe kwa maslahi yenu. Ndio maana sisi (bunge) tunawaona kama wahaini na dawa yenu tunayo. Hatuwezi kuendeshwa na hisia (assumptions) kuwa bandari/nchi inauzwa. Huu ni uchochezi uliopitiliza, unahoji utimamu/integrity wa akili wa Rais halafu mambo yako yaende hivihivi.
 
Haa hilo nalo bunge au mkutano wa nzi?
 
Mkuu unafuata hata mtiririko wa mawazo yako mwenyewe kichwani au unajipinga mwenyewe....

Kwa mtizamo wako chochote kinachopitishwa Bungeni ni wananchi ndio wamesema na ndicho wananchi wanachotaka; Sasa unavyowaambia hao wapinzani wapeleke hoja nzito kwa wananchi (yaani kwamba kuna madudu yanayohitaji kuzungumziwa) huoni kwamba unajipinga mwenyewe iwapo wananchi hao (wabunge) wanachopitisha na wanachofanya Bungeni ndio wananchi wamefanya ?

Na katika kujibu kwako hapo nyuma ukasema wananchi hawahitaji katiba wala nini wanahitaji maji, umeme n.k. - Sasa huo umeme si wamekubali unavyosambazwa na wanavyopata kulingana na bajeti na sera ambazo zinapitiswa Bungeni ?

Mi nadhani kwanza nikupe muda uweze kuji-convince mwenyewe unataka nini au unazungumzia nini alafu tuendelee utakapokuwa na uamuzi na sio flip flopping....
Mzee wewe unahoji quality ya wabunge na spika katika kuwawakilisha watanzania? Unaweza kuhiji integrity ya wabunge na spika lakini huna ushahidi kuhusu jambo hilo. Maana yako kama unahoji quality na integrity ya bunge maana yake unahoji uhalali uwakikishi wao na maamuzi wanavyofanya ya kibunge. Yaani huna imani na bajeti na sheria wanazotunga na kupitisha. Kuwaza kama hivyo ni ujinga kabisa.

Vyama vya upinzani tulikuwa tunawapa wabunge wengi ili wakaongeze nguvu na variety kwenye uwakikishi wa wananchi, lakini hebu ona ni wapumbavu kuliko wapumbavu, wanatuacha na kwenda kuunga juhudi za Rais aliyeko madarakani. Msululu wa wapinzani waliopoteza Imani na nguvu za wananchi kwa kurudi CCM ni mkubwa sana, kiasi kwamba wananchi hawana imani tena na wagombea wa upinzani.
 
Kwamba wewe unaamini integrity ya hawa rubber stampers ? Hata theoretically walioleta haya mambo ya Bunge, Serikali na Mahakama walijua kabisa Power Corrupts and Absolute Power corrupts absolutely.... Ndio maana wakaweka Separation of Powers..., Ila ni kitambo sasa hii ndoa ya mihimili hii mitatu imefanya the whole thing kuwa maigizo ya gharama kubwa sana kwa mwananchi... Ila all is not lost illusion ya kwamba kinachofanyika kinafanywa na wananchi kinaleta peace na a feel good factor watu kudhani kwamba kinachofanyika kule ni wenyewe ndio wanaamua

Ndio maana nikasema mtiririko wa mawazo yako unajipinga kama hawa watu hawaaminiki na wewe huwaamini kwanini sasa unaanza kuwachagulia hata Hoja za kusema; kwanini usipime kila wanachosema na kushukuru angalau wanakiongelea from different angle na sio kuunga juhudi ?
 
Ili wananchi wakuelewe na wakupe farasi wa kwendea Ikulu lazima kwanza uyavae matatizo Yao ya msingi na kuwaonyesha njia rahisi utakayotumia kuyaondosha kwa miaka 5 japo nusu ya shida zao kuu za kiuchumi, afya, chakula na elimu. Wanachi wengi hawaoni connection kati ya shida zao na Katiba na bandari. Ni mwananchi wa kiwango Cha juu sana ambae ana uwezo wa kuunganisha dots kati ya ukosefu wa maji tangu Uhuru na Katiba. Ili wakuunge mkono lazima useme tuandamane bila kikomo mpaka serikali ilete maji hapa, ilete dawa, ilete masoko ya mazao Yao. Kama serikali ikileta maji pale kwakuwa wewe umeandamana utasababisha wananchi wajenge imani na wewe na watakupa kura. Hebu Ona, mikoa na wilaya ambazo CCM inashinda kila uchaguzi hakuna maendeleo na wapinzani hawapati kura. Wapinzani ambao wanaweza kuwashawishi watu WA kwao kuandamana kudai barabara ndio wanaopata kura za wananchi.

Wapinzani wetu (UKAWA) walisababisha nchi kukosa katiba mpya yenye nafuu kwao kisa wanataka serikali tatu. Wananchi hawana haja na muundo wa serikali bali wanataka maji na chakula na Uhuru wao wa kulima na kufanyakazi na biashara ndani ya Tanzania.
 
Haa hilo nalo bunge au mkutano wa nzi?
Shida inaanzia hapo, kwa vigezo vyako unaamini kuwa hilo sio bunge sahihi lakini hakuna watu wamekwenda kulipinga mahakamani, badala yake unajisemea TU kama wapiga ramli.

Bahati nzuri serikali hii inafahamu mambo yafuatayo:
1. Ukoloni mamboleo bado upo
2. Udini bado upo
3. Ukabila bado upo
4. Wasioutaka muungano wapo
5. Ambao hawakupenda Mama Samia kuwa Rais wapo
6. Vibaraka wa Wazungu wapo miongoni mwetu
7. Ushindani wa utalii, bandari na uchumi kati ya nchi na nchi upo
8 wanasiasa uchwara na wanasiasa wa kweli kabisa wapo
9. Wanaonufaika na bandari hawawezi kuwa happy kama bandari ikikodishwa. Hata Simba na Yanga Kuna ambao hawakupenda kabisa Yanga na Simba kufanyiwa mageuzi ya mfumo wa uendeshaji, wahafidhina waligoma.
10. Wahafidhina (Status quo) wanaoogopa change wapo.

Hivyo, hakuna shida kabisa, ndio maana Kuna mambo serikali inakwenda polepole nayo, mengine kwa demokrasia na mengine kwa kutumia mamlaka. Kila dawa ya kila kundi IPO, ingawa nyingine ni tamu, nyingine chachu, nyingine za chumvi chumvi na nyingine chungu sana. ndio maana nchi imetulia tuliii kwakuwa dawa za watu wote hawa wanazo.
 
Kwamba wewe unaamini integrity ya hawa rubber stampers ? Hata theoretically walioleta haya mambo ya Bunge, Serikali na Mahakama walijua kabisa Power Corrupts and Absolute Power corrupts absolutely.... Ndio maana wakaweka Separation of Powers..., Ila ni kitambo sasa hii ndoa ya mihimili hii mitatu imefanya the whole thing kuwa maigizo ya gharama kubwa sana kwa mwananchi... Ila all is not lost illusion ya kwamba kinachofanyika kinafanywa na wananchi kinaleta peace na a feel good factor watu kudhani kwamba kinachofanyika kule ni wenyewe ndio wanaamua

Ndio maana nikasema mtiririko wa mawazo yako unajipinga kama hawa watu hawaaminiki na wewe huwaamini kwanini sasa unaanza kuwachagulia hata Hoja za kusema; kwanini usipime kila wanachosema na kushukuru angalau wanakiongelea from different angle na sio kuunga juhudi ?
Mzee hili ndio bunge letu halali na hii ndio level yetu ya demokrasia. Yaani ni sawa mtu ambae baba yake ni Matonya na mwingine baba yake ni Bakhresa. Wote Wana baba ingawa baba wenyewe na sifa tofauti. Wananchi waliwaamini vyama vya upinzani wakawachagua wabunge wengi wa upinzani lakini wabunge wa upinzani akina Nasari, chacha, mtolea, mkumbo, tumbili, nk wakawasaliti wapiga kura wao kwa vipande vya dhahabu wakaenda kuunga juhudi. Kurudisha uwaminifu huu tena ni kazi ngumu.
 
Back
Top Bottom