Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.
Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.
2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.
3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.
4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.
5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.
6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.
Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.
Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.
Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.
Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu.
Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi vya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.
Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.
Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo.