Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Wanasiasa wetu wa upinzani wanahangaika na matukio badala uhalisia wa mambo kwa ujumla wake. Wanalalamika bila kutoa suluhu nini kifanyike. Walipaswa kuandamana baada ya ripoti ya CAG kuhusu umbadhilifu, walipaswa kuandamana kupinga ukosefu wa pembejeo kwa wakulima na wafugaji, walipaswa kuandamana kupinga ukosefu wa maji kwakuwa hitu vyote hivyo having uhusiano na katiba mpya. Maana katiba ya Sasa haizuii watu kupewa maji, chakula, elimu, mishahara mikubwa Wala ajira. Badala yake wanahangaika na Rais anaetaka kufanya mapinduzi kwenye bandari, maji, umeme, usafirishaji, michezo nk. Hakuna mwananchi mwenye akili atakaewaekewa. Hizi ni jitihada za wivu na kutaka kuingia Ikulu na wakishafika Ikulu wanakenua TU. Ruto alililia kwenda Ikulu na akafika Ikulu, je, wakenya wanapata ahueni gani chini ya Ruto? Ndugu zangu tatizo letu sio katiba Wala Chama tawala, bali tatizo letu ni zaidi ya katiba na Chama kilichoko madarakani, tusiwafanye watu kama vile hawana akili. Ukimuuliza mwananchi wa kule nanjilinji kuhusu bandari atakushangaa sana. Wewe muulize habari za umeme, dawa, barabara, masoko, maji ya kufulia nk.
Acha kudanganya watu wewe wapi umeona kuna ubadhilifu, wapi kuna ukosefu wa pembejeo kwa wakulima, wapi kuna ukosefu wa maji mpaka wapinzani waandamane kupinga vitu hivyo? Hii nchi hakuna shida chini ya utawala wa CCM🤣🤣🤣🤣🤣
 
Umesahau na TANESCO tuwape watu binafsi maana serikalini imeshindwa kuleta mabadiliko ya kuondoa migao 🤣🤣🤣
Hakuna ubaya hata tanesco ikikodishwa pia, shida iko wapo. serikali zote duniani hazifanyi biashara. Benk, mashirika, makampuni, mashamba na viwanda vya vilivyokuwa vikiendeshwa na serikali vyote havikufanya vizuri.
 
Wakati JPM anakama watu wote ambao wanadaiwa kodi, wakwepa kodi na wabadhilifu wananchi walipiga kelele sana kwakuwa sio utamaduni wetu kulipa kodi na kuwaadhibu wahujumu uchumi. Lakini hata JPM alikuwa hatumii sheria zilizopo kudai madeni na kuwaadhibu wakwepa kodi. Wakati adai madeni na kuadhibu wakwepa kodi nae alikuwa anazalisha makosa. sheria zetu sio kali hivyo haziwezi kusaidia mchakato wa kupata mavuno. Kule China na nchi nyingine ambazo serikali inasimamia michakato ya kupata mavuno hawana mtu mwenye kinga ya ubadhilifu, rushwa, magendo na adhabu zao ni kifo moja kwa moja kwa yeyote yule awae na kosa la ubadhilifu wa mali ya umma. Hapa kwetu kama utatunga adhabu kali kama hizo za usimamizi utakutana na watu wa haki za binadamu kutoka ndani na nje ya nchi. Bora tubinafsishe na kusimamia sera ya win-win.
 
Mimi si support ujinga wa bandali kuuzwa
Shida yetu kwenye jambo hili la bandari ni wanaopinga ni kwenye hoja zao kutumia maneno ya kibaguzi kama Tanganyika, watanganyika, mtanganyika, zanzibar, wazanzibar, mzanzibar, waarabu, waislam, mwisilam, uislam na Mama. Anaewasiliza hoja zao anapata harufu ya shida ya Muungano (UKAWA), udini, na genda. Kwa mtu ambae ameapa kulinda Muungano, Katiba na Jamhuri hawezi kuvumilia ujinga na ulevi kama huo. Kwanza Tanzania hakuna mwananchi ambae yuko tayari kuandamana kijinga kuunga mkono wasichokijua, kisichowaumiza na kisichowapa mkate wao, ndio maana akina Lissu, mbowe, mnyika, mo, na wengine walikutana na kadhia za serikali bila kuonekana mtu kuandamana kuwaunga mkono au kuoinga walichofanyiwa. Acha kuandamana utapata shida bure.
 
wewe ni kilaza hata ulichoandika inawezekana sicho unacho waza
Nchi hii ina viasi wengi. Kuna viazi eti wanataka kuwaaminisha watz wote kwa wakati mmoja kwa mara moja kuwa Katiba haifai, serikali haifai, bunge halifai na mahakama pia haifai. Huu ni upuuzi wa hali ya juu kwa watu waliozoea amani na utulivu kwenye maisha yao. Kama wamepewa fedha kwa kuifanya hiyo kazi basi kazi itawawia ngumu sana kuikamilisha. Huhitaji kupiga kampeni kwa jambo linalowakera sana watu wengi kwa wakati mmoja. Mfano, hebu atokee mtu akataze watu wote kulima au kufanyabiashara aone kitakachompata.

Kama jambo la bandari lingekuwa linawakera watu wengi sana nchini ungeona nchi nzima ingejitokeza kupinga kukumatwa kwa Dr. Slaa na wenzake, lakini ona mwenyewe mzee amekamatwa lakini watu wanaendelea na kazi zao kama kawaida kana kwamba hakuna kilichotokea. Tusijidanganye, tz haijafikia ngazi hizo.
 
Mimi na mke wangu ni watanganyika na hatuoni hivyo kama bandari yetu kuna mtu anaiuza, Dr. Slaa anapata wapi mamlaka ya kunisememea mimi na mke wangu kuhusu bandari yetu? Nani anajua Dr. Slaa anamtumikia nani. nani anaefahamu Dr. Slaa anapinga bandari isibinafsishwe kwasababu gani, ni kwanini anataka hisia zake kuhusu bandari ziwe ni hisia za watanzania wote?

Mimi na familia yetu tuna akili timamu, tunafahamu kuwa katiba hii haikuandikwa na Mama Samia, tunafahamu kuwa waliyoifuta serikali ya Tanganyika ni sisi watanganyika wenyewe kwa sababu zetu na wazanzibar wenyewe walikataa kuifuta serikali yao ya Zanzibar.

Tunafahamu kuwa Dr. Slaa ni mtafuta maslahi binafsi anayehama kati ya CCM na Chadema wakati wowote kwa maslahi yake binafsi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kumuamini Slaa any more, wote tuna kumbukumbu ya Dr. Slaa kwenda kujifungia Serena hotel chini ya ulinzi wa CCM akiisaliti Chadema. Dr. Slaa anaamini kwenye kukinga bakuri
 
Hao wananchi ni akina nani? wako wangapi? nani hataki? walikutana wapi? wananchi wangapi wanataka mkataba? kakojoeni mlale. Wananchi wangapi walipinga benk zisibinafsishwe na zikabinafsishwa? Hata Nyerere alipinga mashirika kama sigara na bruweries kubinafsishwa lakini yakabinafsishwa, kuna waliopinga nyumba za serikali zisiuzwe lakini ziliuzwa. Samia usirudi nyuma kwenye hili, wapingaji walikuwepo tangu wakati wa kutafuta Uhuru, wako ambao walipinga nchi kupata uhuru 1961. Hakuna asiejua kuwa wakatoliki (wamissionari) waliwatangaulia wakoloni kuja Tanzania, walisali nao, waliishi nao nyumba na mtaa mmoja na wakoloni waliwaacha tz wakati wao wanaondoka kurudi makwao. Tunafahamu huu ni mkono wa kulia wa mabeberu.

View: https://www.youtube.com/watch?v=mUYUwuviszA
 
Peleka wewe hzo hoja , kama rasilimali zinagawiwa hovyo Kwa watu wengine hayo maji utayapataje we kiazi
Kama serikali yenye ridhaa ya wananchi Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, wananchi kupitia bunge lao, na mahakama wote wametuhakikishia kuwa nchi na bandari zake viko salama kwenye mkataba huu, wewe ni nani utuambie nchi inaunzwa? Inauzwa bei gani? Ushahidi wa huo mnada unao? Tanzania tuko 60 milioni, Ni wananchi wangapi kati ya hao hawautaki mkataba? Kati Yao wanaukataa mkataba wanawake ni wangapi na wanaume ni wangapi? Waisilamu ni wangapi na wakristo ni wangapi, na kati ya hao wakatoliki ni wangapi, idadi ya wakulima wako wangapi? Wafugaji je? Machinga na watumishi wa umma wako wangapi wanaopinga?

Huna takwimu kaka tafuteni agenda madhubuti ya kuwapeleka Ikulu 2025 sio hii ya bandari. Mama kabana agenda zote kuanzia bandari, utalii, kilimo, ufugaji, usafiri, elimu, maridhiano, michezo, umeme na maji kote ameziba nchi inapaa. Tuna akili sisi.
 
wewe ni kilaza hata ulichoandika inawezekana sicho unacho waza
Baki hapohapo, Rais Samia anataka kutuonyesha pale tulipokuwa tumekwama kwa miaka 60, give her time. Anatumia kila sent kwaajili ya watu. hana msululu wa ndugu, marafiki wala nyumba ndogo. Nchi nzima inajengwa bila kuangalia kabila wala kanda.

Serikali imeamua, bunge limeamua na mahakama imeamua!!!!! kama wote hawa wameamua ni Amirijeshi gani atatishwa na mtu mjingamjinga ili akwame kutimia ndoto zake? Yajayo yanafurahisha. hata hivyo tusisahau kuwa hii katiba yetu inampa nguvu nyingi sana Mkuu wa nchi, mtu asije kusahau hili akajichanganya.
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kama mikipewa uongozi wa nchi kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi wapinzani mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi badala ya kujikita kwenye hoja na mbinu za kuwasaidia watanzania kwenye shida zao za msingi zinazowatafuna. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu badala ya kuokoteza matukio.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi ya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo, shida za wananchi zinabakia palepale vilevile hata wakibadilisha vyama tawala na viongozi wakuu. Hii inamaana kuwa tatizo sio katiba zao wala tume zao za UCHAGUZI wala rasilimali wala vyama tawala wala viongozi peke yake, bali tatizo liko nje ya bara la afrika na ndani ya mindsets za watu wetu.
Unateseka ukiwa wapi mkuu?
 
Unateseka ukiwa wapi mkuu?
Katiba mpya kila mtu anaitaka, lakini Ilani ya CCM haikuwa na agenda hiyo kama alivyosema Rais JPM (rip), endeleeni kusubirini. Ilani ya CCM ya 2025-2030 lazima itakuwa na ibara ya katiba mpya. Kwasasa inatumika Katiba hii ya 1977 kikamilifu kama watu walivyoapa kuilinda isichezewe. Rais ameapa kuwatumikia na kuwalinda watanzania kwa mujibu wa katiba hii.
 
Mimi si support ujinga wa bandali kuuzwa
Sio kuuzwa ni kukodishwa kwa DP World. Msidanganywe na wapinzani. Wananchi wenye akili nyingi ni vigumu kuwaamini wapinzani tena, hasa baada ya akina Nasari kudharau nguvu na jasho la wananchi kuwachagua wao kisha wakawasaliti kwenda CCM kuunga juhudi. Dhambi hii imefanywa wa wapinzani wengi akina Lyatonga, lamwai, tumbili, sumaye, lowasa, mwita, Dr. Slaa, Prof. Kitila, na wengine wengi. Wananchi wengi wamepata phobia ya upinzani maana hawajui nani ni nani. Eti Slaa amerudi chadema tena baada ya mambo yote Yale. Wacha mama zetu wawapogie kura safari hii sio sisi tena, vinginevyo lazima kuwa na mkataba maalumu wa kisheria kati ya wagombea wa upinzani na wapiga kura ili wakienda kuunga juhudi kuwe na consequences.
 
Watoe wapi wazee wa matukio hao,hii ya upotoshaji imebuma Sasa wakizido Ili walete vurugu watadhibitiwa maana wanatumia uhuru wao vibaya

Inasikitisha sana. Wapinzani walikuwa wamefungiwa kufanya siasa kwa muda mrefu, tulitegemea baada ya kufunguliwa kufanya saisa waje na hoja nzito kwa wananchi ambazo zitawafanya waonekane kuwa bora hadi kuchaguliwa kuingia Ikulu lakini hawafanyi hivyo. Wapinzani wote ni bandari bandari bandari inauzwa inauzwa!!, katiba katiba Halima mdee Halima mdee Huku mwenzao Samia na CCM vumbi linatimka nchi nzima kujenga barabara, mwendokasi, flyovers, shule, hosipatli, bwawa, reli, kusambaza maji, kuvutia utalii, viongozi wakuu wa kimataifa kumiminika nchini, kukuza kilimo kwa vitendo, nk. Wanadhani wananchi ni wajinga wa kiasi hicho?
 
Baki hapohapo, Rais Samia anataka kutuonyesha pale tulipokuwa tumekwama kwa miaka 60, give her time. Anatumia kila sent kwaajili ya watu. hana msululu wa ndugu, marafiki wala nyumba ndogo. Nchi nzima inajengwa bila kuangalia kabila wala kanda.

Serikali imeamua, bunge limeamua na mahakama imeamua!!!!! kama wote hawa wameamua ni Amirijeshi gani atatishwa na mtu mjingamjinga ili akwame kutimia ndoto zake? Yajayo yanafurahisha. hata hivyo tusisahau kuwa hii katiba yetu inampa nguvu nyingi sana Mkuu wa nchi, mtu asije kusahau hili akajichanganya.
umemaliza
 
Kinachowasumbua vyama vya upinzani ni kukosa dira Wala uelekeo. Dr. Slaa na Prof. Lipumba wanastahili kuwa wapinzani? Dr. Slaa anastahili kurudi chadema tena? Je, wapinzani wanasema nini juu ya wabunge na wagombea wa upinzani waliorudi CCM kuunga juhudi? Mbona viongozi wa vyama haombi radhi wapiga kura na wanachama wao? Wanatuonaje sisi tuliowapigia kura na kukesha kulinda kura zao?

Safari hii hatumpigii kura mpinzani bila kuapishana kwanza. Wasitugeuze saccos zao. Wengine wanamiliki mahoteli, mashamba, na mamiradi makubwa kwa kutumia jasho letu.
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kama mikipewa uongozi wa nchi kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi wapinzani mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi badala ya kujikita kwenye hoja na mbinu za kuwasaidia watanzania kwenye shida zao za msingi zinazowatafuna. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu badala ya kuokoteza matukio.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi ya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo, shida za wananchi zinabakia palepale vilevile hata wakibadilisha vyama tawala na viongozi wakuu. Hii inamaana kuwa tatizo sio katiba zao wala tume zao za UCHAGUZI wala rasilimali wala vyama tawala wala viongozi peke yake, bali tatizo liko nje ya bara la afrika na ndani ya mindsets za watu wetu.
Haa haa just haa haa.! Mmeshindwa kutetea LIMKATABA LIBOVU mnataka sasa na sisi tunao upinga tunyamaze. Halafu maisha yaendelee. Hili la kuuza bandari si sawa na la kuuza madini. Hakuna mwenye akili timamu atanyamazia hili. Mkataba ni MBOVU, UFUTWE. Ni LAZIMA UFUTWE.
#OkoaBandariZetu
 
Ni nani tumuamini akisema ni mzuri au ni mbovu? Ni wakati gani tunaweza kuondoa maslahi binafsi kwa wanaopinga na wanaotetea? Wanaotetea wako pamoja na serikali, bunge na mahakama, wale wanaopinga wako pamoja na nani, walanguzi? TICKS? washindani wa bandari za tz? wakwepa ushuru bandarini? Wanufaika binafsi au nani?

Ndiyo maana tunaounga mkono hatutetereki kwakuwa tuko pamoja na serikali yenye dhamana, bunge linalotunga sheria na kuwakilisha watanzania wote na mahakama inayotafsiri sheria na mikataba. Nyie mko na nani nyuma yenu hadi tuwaamini. Kwanza mnaopinga mko wangapi tuwajue?

Hakuna asiyefahamu kuwa Kuna watu wanakwepa kulipa ushuru kamili pale bandarini, hao Wana matumbo joto.
 
Back
Top Bottom