Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

10126120311.jpg
 
Hakuna heshima ktk kukwepa ukweli kuwa kuna maambukizi mapya yameibuka hapa nchini kwa hivi sasa ya COVID-19, eti tu kwa kuwa tulikwisha utangazia ulimwengu kuwa tulfanikiwa kulisambalatisha gonjwa hili kwa njia ya sala, dua na maombi.

Viongozi wakili tu ukweli kuhusu tishio la gonjwa hili lilivyokuwa hivi sasa. Pengine waje na kauli mbiu na hamasa mpya ya awamu ya pili ya kupiga tena maombi ya kitaifa ili kupambana na wimbi hili jipya la sasa.

Tukubaliane nao tu kinadharia kuwa wimbi la kwanza lilisambalatishwa na kuiacha nchi salama dhidi ya nyingine ulimwenguni kote. Walete nadharia mpya juu ya haja ya kuwepo maombi mapya yatakayo kabiliana na wimbi hili jipya.

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, asema BWANA.
 
Kanisa lisipokanusha hii habari ndani ya saa 72 basi nipigeni ban! Naamini watakanusha sio kwa sababu hawajaandika au hawaamini suala la uwepo wa corona bali watakanusha kwa sababu kutoa taarifa kama hii ni kuipigana vita vya kiuchumi dhidi ya taifa letu huku kanisa likiwa upande wa mabeberu.
Unajuaa vikao vya maamuzi hayo. Unadhaani ni maaamuzi ya msela kama gwajiboi na mzee wa upako?
 
Hii second half ni HATARI, ni uchaguzi wa kuvaa barakoa au kuondoka.

Dude limetoka South linapandisha mdogo mdogo.

Linaning'niza hadi naogopa maana naona dalili za Melinda Gates kuwa nabii.
Unajua ubishi mwingine ni janga kwa Taifa. Watu walionya na bado wanaonya: virus huwa wana mutate. Ukiamua kupuuza tu wanaweza kusababisha madhara makubwa.
 
NEMONIA ishaondoa wengi sana, na hii ya kisasa inashika watu wazima tu, wajanja wamejichimbia kijijini kwao huko pembezoni mwa ziwa kuu la Afrika mashariki, nyie endeleni kumbwela mbwela tu mjini.

Kuna Simba Cup, watu wataambukizana sana.
 
Chonde chonde tusije geuzana miradi kwenye majanga..., (by the way sijasema kwamba wewe ni mmojawapo huenda wewe unasaidia jamii kwa kuwapatia lishe
Nimezikuta mtandaoni tu, nyingine hata majaribio sijui yalifanyikia wapi. Unaweza kujikuta unakunywa maji ya mtaroni yaliyowekewa pilipili
 
Afadhali sasa sauti zinaanza kupazwa toka kila kona, tuache kuishi kwa kudanganyana kama watoto, kila mmoja popote alipo achukue tahadhari kwa kujilinda yeye na awapendao, Corona ipo na inaua.
Mambo mengine ni kumwachia Mungu tu. Hivi mnadhani USA wanakokufa watu 2000+ Hawana mbinu kama sisi?

Mungu yeye anajua kabisa hili gonjwa halina cha kujihami wala kwamba umejipanga. Likija limekuja hakuna cha kwamba una huduma nzuri za afya wala kwamba una mipango mizuri.

Ndiyo maana Magufuli amemwamchia Mungu. Tumaini letu watanzania liwe kwa Mungu.

Kama ni barakoa Marekani wana vaa sana, kama ni vitakasa wanatumia sana, lockdown wamepiga sana. Lakini kamwe gonjwa ndiyo bado lime simama.
 
Naungana na tamko hili 100%

Tuungane tena kumwomba Mungu ili akomeshe wimbi hili jipya la maambukizi!

Kwani Hadi leo, Dunia yote inaimba wimbo huu mmoja, Na hakuna kiongozi yeyote ama nchi yoyote duniani iliyekomesha maambukizi nchini mwake
 
Back
Top Bottom