Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Hakuna serikali inachoweza fanya zaidi ya kutuhimiza kunawa, vaa barakoa, Epuka misongamano etc

Mambo mengine tu jiongezee. Serikali mfano ikaamua sasa watu wapigwe lock down mtasemaje?

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Mkuu tuache siasa, watz hatujui tunataka nini.

Siku akitangaza lock down nakuhakikishia watapiga kelele mno ooh anataka kuua raia, ooh uchumi utakufa.

Likija swala la siasa huwa nakuwa kimya tu
 
Hakuna serikali inachoweza fanya zaidi ya kutuhimiza kunawa, vaa barakoa, Epuka misongamano etc

Mambo mengine tu jiongezee. Serikali mfano ikaamua sasa watu wapigwe lock down mtasemaje?

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app

Swala siyo watu kupigwa lock down ni kusema kuna tatizo watu wachukuwe tahadhari kukaa kimya watu wakiendelea kufa kwa wingi siyo sawa. Kwani kuna ugumu gani kusema kuna corona wakati kila mtu anafahamu kuwa Corona ipo
 
Tulichukua hatua kwa kusali! Hivi Mungu wa wakatoliki wa Tanzania na wa wakatoliki wa Vatikani wana tofauti?
 
Mimi toka Covid-19 Vol 1 hadi hii ya sasa Covid-20/21 Vol 2 nilikuwa natandika na bado mpaka sasa natandika mchanganyiko wa tangawizi kali,limao,kitunguu twaumu mixer asali kila siku iendayo kwa Mungu ila majuzi hapo nilipigwa mafua moja na homa kwa mbali mpaka sasa sauti haijarudi normal naamini kwa uweza wa aliye juu tutavuka tena na hili.

Waafrika tuna shida zetu Mungu mwenyewe anajua mwafrika hajaumbwa afe kwa mafua sisi zetu ni ajali,milo mibovu malaria etc ila tuwe na tuzidishe tahadhari na huu ugonjwa.
 
Baraza la maaskofu lingekua sahihi kama hiyo ingekua internal memo lakini kuifanya public ni kuikosea serikali adabu.

Regardless.
 
Kanisa lisipokanusha hii habari ndani ya saa 72 basi nipigeni ban! Naamini watakanusha sio kwa sababu hawajaandika au hawaamini suala la uwepo wa corona bali watakanusha kwa sababu kutoa taarifa kama hii ni kuipigana vita vya kiuchumi dhidi ya taifa letu huku kanisa likiwa upande wa mabeberu.
Ngoja nikufungue macho kidogo, siku zote ukiona kanisa katoliki linatoa kauli ujue hiyo imepita, kwasababu wao ndiyo wanao control mambo mengi hao ni zaidi ya kanisa. Hakuna kiongozi wa kiserekali anaweza kushindana nao.
 
Wakotoliki tulisha wazoea hata mala ya kwanza ndio walikuwa wa kwanza kufunga makanisa yao, wanauakika upi kuwa Tanzania Kuna korona wakati shughuli zote zinaendelea kama kawaida?

Shule zote zimefunguliwa vyuo vyote viko wazi na ndio kuna mikusanyoko mikubwa, atujaona walimu wakilalamika kuwa Kuna mwanafunzi hata mmoja aliyepatwa na huu ugonjwa, taifa star wako kameluni atujaona wakirudishwa kuwa wana korona.

Hawa ni watumishi wa mshahara hata Yesu aliwasema kuwa wakiona hatali wanakimbia wanaacha kondoo, baada ya kuwatia moyo watu kuwa kama ya kwanza tulishinda kwa kumuamini Mungu na hii tunashinda,sio kuandika nyaraka za kuogopesha watu.
 
Lakini mbona kama waraka una mapungufu mengi.

RE: TAHADHARI..

badala ya

YAH: TAHADHARI...
 
Ngoja nikufungue macho kidogo, siku zote ukiona kanisa katoliki linatoa kauli ujue hiyo imepita, kwasababu wao ndiyo wanao control mambo mengi hao ni zaidi ya kanisa. Hakuna kiongozi wa kiserekali anaweza kushindana nao.
We bhana acha habari zako! Mara ngapi kanisa limeshawahi kukana waraka wao?! Tuombe tu wasitikiswe lakini kwa serikali hii don't say "NEVER"! Au tuombe tu iwe wameshapata baraka za wenye mamlaka!
 
Unajuaa vikao vya maamuzi hayo ... Unadhaani ni maaamuzi ya msela kama gwajiboi na mzee wa upako?
Kwani ile shule ambayo juzi tu hapa ilikanusha taarifa yake wenyewe nao maamuzi yao ni kama ya Gwaji Boi?

Mimi sina shaka na taarifa ya kanisa bali shaka yangu ni wale ambao wakiona mambo kama haya wanakimbilia kusema "hii ni hujuma na vita vya kiuchumi" na kwahiyo wanawashinikiza watu wakanushe taarifa zao kama ilivyokuwa kwa ile shule.
 
....................Mimi toka Covid-19 Vol 1 hadi hii ya sasa Covid-20/21 Vol 2 nilikuwa natandika na bado mpaka sasa natandika mchanganyiko wa tangawizi kali,limao,kitunguu twaumu mixer asali kila siku iendayo kwa Mungu ila majuzi hapo nilipigwa mafua moja na homa kwa mbali mpaka sasa sauti haijarudi normal naamini kwa uweza wa aliye juu tutavuka tena na hili.

Waafrika tuna shida zetu Mungu mwenyewe anajua mwafrika hajaumbwa afe kwa mafua sisi zetu ni ajali,milo mibovu malaria etc ila tuwe na tuzidishe tahadhari na huu ugonjwa.
Inshallah Allah atakupa shufaa
 
Back
Top Bottom