Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Ngoja nikufungue macho kidogo, siku zote ukiona kanisa katoliki linatoa kauli ujue hiyo imepita, kwasababu wao ndiyo wanao control mambo mengi hao ni zaidi ya kanisa. Hakuna kiongozi wa kiserekali anaweza kushindana nao.

Bakwata je au mpaka nao mashekhe kadhaa wavute?
 
Mkuu Quinine,

Umeleta mbio mbio huu waraka ukitarajia kilichoandikwa kitaiudhi serikali, pole sana.

Huu waraka hauna madhara yoyote ila utakuwa msaada mkubwa kusaidia katika kutoa elimu ya madhara ya ugonjwa husika hivyo kila mmoja kuchukua tahadhari. Kinachopingwa na serikali ni kufungia watu ndani huku shughuli za kiuchumi zikilala.

Mie nawaunga mkono kwakuwa hata uwasilishaji wake umejaa hekima ya Mungu, haujamshambulia yeyote kwamba ama amezembea au ndi chanzo cha kuibuka upya.

Kumbuka Vurusi havifi kama bakteria wanavyokufa unapowakabili madhara yake yanaanza na viungo vya ndani vikishambulia na kujificha kwenye ini ukilinganisha na vimelea vingine unahisi maumivu kutokana fujo zake vianapokuwa vinatafuta himaya kwenye mwili

1. Any virus infected disease in human body it works as a silent killer eg. UKIMWI/AIDS/HIV, UVIKO/KORONA, homa nyongo (hepatitis), polio, mafua (cold), homa ya mafua (influenza)
2. Any bacterial infected disease in the human being (victim) is an aggressive killer eg kifua kikuu (tuberclosis), tauni (bubonic plague), homa ya matumbo (typhoid), ukoma (leprosy)
3. Any parasite infected disease in human being it works aggressively eg Malaria, matende (elephantiasis)
4. Fungi-nyungunyungu ya ngozi (athletes foot)
 
Mambo mengine ni kumwachia Mungu tu. Hivi mnadhani USA wanakokufa watu 2000+ Hawana mbinu kama sisi?

Mungu yeye anajua kabisa hili gonjwa halina cha kujihami wala kwamba umejipanga. Likija limekuja hakuna cha kwamba una huduma nzuri za afya wala kwamba una mipango mizuri.

Ndiyo maana Magufuli amemwamchia Mungu. Tumaini letu watanzania liwe kwa Mungu.

Kama ni barakoa Marekani wana vaa sana, kama ni vitakasa wanatumia sana, lockdown wamepiga sana. Lakini kamwe gonjwa ndiyo bado lime simama.
Wewe unasali kwa gwajima, mwamposa au nabii kingu?
 
Sasa itakuwaje🤭🤭 serikali haina dini, haiamini uchawi haiamini kama kina kitu kinaitwaga korona
 
Naungana na tamko hili 100%

Tuungane tena kumwomba Mungu ili akomeshe wimbi hili jipya la maambukizi!

Kwani Hadi leo, Dunia yote inaimba wimbo huu mmoja, Na hakuna kiongozi yeyote ama nchi yoyote duniani iliyekomesha maambukizi nchini mwake
Ni muda wakuomba Mungu atuponye tena.naamini ni Mungu muaminifu na anatupenda pia
 
Wataalamu wa afya mnaopitia humu. Naomba mwenye maelezo ya kina ya uwezekano wa mtu ambaye ameumwa na nyoka ndani ya miaka mitano kutosumbuliwa na na maradhi ya upumuaji.
 
Hii kitu hadi bbc wameitangaza unadhani ni rahisi kwa namna hiyo? alafu hawa watu wanajua sana kula na kipofu. ila ukiwazingua wanakuzingua mara mia.
Ndugu, usifanye kama hujui tupo kwenye mazingira gani! Suala la BBC kutangaza sio issue. Na kama nilivyosema, tuombe ama wawe wamepata baraka za watawala au wasitikiswe! Kupata baraka kunakuja pale ambapo serikali inaweza kuona aibu kula matapishi yake yenyewe na hivyo kuamua kutoa uhuru kwa taasisi kutahadhalisha watu wao! Tanzania hii taasisi za dini zinazoweza kupingana ki ukweli na serikali ni zile zisizokula neema za serikali! Haya makanisa makubwa, hususani RC na BAKWATA, wote wala neema za nchi!! Wakipigwa mkwara wa kodi tu, wote wanaufyata!!
 
Wao ni Idara ya afya? Wanasemaje pia kuhusu Malaria?
Kila mtu( mwenye akili timamu) anapaswa kuchukua hatua yeye mwenyewe,na kuwakumbusha wengine,kila mmoja anajua kuwa corona IPO!!! Kusema tu haipo haifanyi isiwepo,malaria pia imepungua kwa baadhi ya mikoa hapa nchini,ila bado jitihada zaidi zinahitajika kuutokomeza kabisa,chukua tahadhari,corona ipo na inaua
 
Ndugu, usifanye kama hujui tupo kwenye mazingira gani! Suala la BBC kutangaza sio issue. Na kama nilivyosema, tuombe ama wawe wamepata baraka za watawala au wasitikiswe! Kupata baraka kunakuja pale ambapo serikali inaweza kuona aibu kula matapishi yake yenyewe na hivyo kuamua kutoa uhuru kwa taasisi kutahadhalisha watu wao! Tanzania hii taasisi za dini zinazoweza kupingana ki ukweli na serikali ni zile zisizokula neema za serikali! Haya makanisa makubwa, hususani RC na BAKWATA, wote wala neema za nchi!! Wakipigwa mkwara wa kodi tu, wote wanaufyata!!
Punguani
 
Back
Top Bottom