Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Watu washasahau kama serikali ya Tanzania ilikuwa ikilalamikiwa kutoka nje na ndani kuhusu kutokufuata ushauri wa kitaalamu katika kupambana na corona na Magufuli amekuwa akionekana kuudharau huu ugonjwa toka mwanzo mpaka sasa,et leo hii mtu anakwambia tulifanikiwa katika mapambano ya corona et tulifuata ushauri wa wataalamu na kufanikiwa kuondoa maambukizi ya corona. Tatizo ukisema vitu hivi watu hawataki kukuelewa wanakuona mbishi wao wanawaza wimbi la pili la Corona,cha ajabu hata hawaelezi ni kipindi gani ndio ilianza kupungua hiyo corona?

Corona ingekuwa inapiga kisawa sawa kama huko kwa wazungu ndio tungeelewana ila kwa hivi kila mtu anaongea lake huyu atakwambia imepungua mwengine atakwambia haipo kabisa.
 
Corona kweli ipo. Mnataka lockdown au? Huko walikofanya hivyo nini kimebadilika?
 
Nikajua wataisemelea kwa yesu au Mungu ili aiondoe! Wanakwama wapi..?
 
Hali imekua mbaya...naona kanisani kwetu tumeanza kusali ile Sala tuliyokuwa twasali enzi za Corona part1
 
Wizara ya afya iko wapi? maana sasa taarifa rasmi kuhusu magonjwa zinatolewa na baraza la maaskofu..
 
Wao ni Idara ya afya? Wanasemaje pia kuhusu Malaria?
Wao wametoa tahadhari kwa waumini wao. Wapo pia watakaosikia au kusubiri kauli za idara ya afya; nao ni waumini wa mtu au kikundi fulani. Haujazuiwa au kulazimishwa kufuata sauti yao
 
Toka mwaka jana serikali msimamo wake ni kwamba hakuna corona sio imepungua bali hakuna kabisa,na kwa muda wote imekuwa ikilalamikiwa kwa kusema hivyo ila watu leo wanasema Tz tulifuata ushauri wa wataalamu wa tukapunguza maambukizi na sasa wanataka serikali itangaze kuwepo corona.
 
Screenshot_20210126-230621.png
 
Kuna Mbwa Mmoja wa Jirani yangu Jonikov Yeye anapenda akibweka tu umuogope na umsifie ila ukimkwaza tu lazima akulipizie bonge la Kisasi.
 
Ukitengeneza mazingira ya mwanao kukuogopa jua hilo ni zaidi ya bomu la nyuklia. Ipo siku litakupiga likuachie ulemavu wa maisha ili kukuwekea kumbukumbu na kukfundisha kwamba usiwe katili kwa mtu yeyote au litakupoteza ubaki historia ya baba dikteta.
 


WHO: Vifo vitokanavyo na Malaria huenda vikaongezeka mwaka huu barani Afrika.


Idadi ya vifo vilivyosababishwa na Malaria katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara inaweza kuongezeka mara 2 hadi kufikia 769,000 mwaka huu, iwapo nguvu zote zitaelekezwa katika mapambano ya COVID-19.
Shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya katika taarifa yake kwamba hadi sasa Afrika imethibitisha kesi zaidi ya 25,000 za virusi vya corona huku vifo vikipindukia 1200, na serikali kwa kushirikiana na WHO, zimejielekeza zaidi kwenye kupambana na janga la corona.

Mkurugenzi Mkaazi kanda ya Afrika Dr. Matshidiso Moeti amezitolea wito nchi zote za kiafrika kuhakikisha kwamba juhudi za kupambana na Malaria zinaendelea.

"Uchambuzi wa hivi karibuni ulibaini kwamba vyandarua vilivyowekwa dawa vimeachwa kusambazwa na udhibiti wa kesi umepungua, vifo vya malaria katika nchi za Afrika kusini mwa Sahara vinaweza kuongezeka mara mbili ukilinganisha na mwaka 2018”, alisema Moeti.

"Hii itakuwa idadi kubwa ya vifo kuwahi kushuhudiwa katika ukanda huo tangu mwaka 2000”, aliongeza mkurugenzi huyo. Pia aligusia juu ya takwimu za mripuko wa kirusi cha Ebola barani Afrika, na kuonyesha kwamba watu walikufa kutokana na maradhi mengine, ikiwemo malaria, kuliko hata Ebola yenyewe, kutokana na ukosefu wa upatikanaji matibabu.

Vifo vitaongezeka iwapo kasi ya kupambana na Malaria itapungua


Mwaka 2018, kulikuwa na visa milioni 213 vya malaria na vifo 360,000 vinavyohusiana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika, ikiwa ni asilimia 90 ya kesi zote duniani. WHO imesema kama lengo la kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona itachangia kupungua kwa upatikanaji wa dawa za kupambana na malaria, vifo vitaongezeka mara mbili.

"Nchi katika ukanda mzima zina nafasi ndogo na fursa ya kupunguza uingiliaji katika udhibiti wa malaria, matibabu na kuokoa Maisha katika kipindi hiki cha mripuko wa COVID-19”, ilisema taarifa ya WHO.

Benin, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Sierra Leone na Chad zote zilianzisha programu za kupambana na malaria kipindi hiki cha mripuko wa corona, limesema WHO, na kuongeza kuwa nchi hizo zinapaswa kuwa mfano kwa mataifa mengine ya Afrika.
 
Moderator,

Kanisa lisipokanusha hii habari ndani ya saa 72 basi nipigeni ban! Naamini watakanusha sio kwa sababu hawajaandika au hawaamini suala la uwepo wa corona bali watakanusha kwa sababu kutoa taarifa kama hii ni kuipigana vita vya kiuchumi dhidi ya taifa letu huku kanisa likiwa upande wa mabeberu.
Ukumbuke huyo akifika kanisani upiga magoti kwa unyenyekevu mbele ya padre ndio sembuse Baraza la maaskofu?

Halafu hao wana msemo wao wanasema Roma ikiongea ni Finito causa.

Hao maelekezo yao wanapokea kutoka Vaticano.
 
Back
Top Bottom