Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Ni mbwa au mbweha? Maana kwa uoga alionao!
 
Stupid mind. Ngoja siku ukinasa au anase anayekuhusu utaropoka uharo hapa!!!!

Sisi ambao tulizaliwa kabla ya ukimwi tuna uelewa wa jambo moja. Ugonjwa ukiingia mahali au duniani. Kutoka ni ngumu sana. Ni kama unavyoungia mwilini, ni kazi sana kutoka. Ndivyo ilivyo kwa uviko-19, hautaondoka ghafla bin vuu. Bali utaendelea kukaa kwa muda mrefu tu. Hata pengine utadumu kama ukumwi. Hivyo nionavyo kila mtu anajua hali ilivyo. Tahadhari ziendelee kuchukuliwa. Tusizushe taharuki au kulaumu huyu alifanya hivi au hakufanya hivi. Hiyo haitatusaidia. Bali kitakacho tusaidia TAHADHARI, TAHADHARI TAHADHARI.
 
Madaktari wa thiolojia wameamua kutema cheche..

Safi..Tz sio kisiwa,tusidanganyane kama watoto..Serikali ije na measures upya,wazee wanapukutika tu daily
Nipo Zanzibar kwa Sasa nawaona mabeberu wanazid kufurika na familia zao kuja kula maisha au wao wameshapata chanjo ya covid19?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
ONDOA MASHAKA YAKO NI MAELEKEZO TOKA VATCAN HANA NAMNA.

Halafu mnataka muambiwe CORONA IPO ili iweje au mmeambiwa dawa imepatikana. AU kuna pesa utapata.

SASA KAMA TZ KUNA CORONA MBONA MAKABURI MAPYA YALIYOPO KWA WINGI HATUYAONI .
Zanzibar watalii wana kuja kwa wingi na hawataki kurud makwao

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Wao ni Idara ya afya? Wanasemaje pia kuhusu Malaria?
Kama wameandika upuuzi wewe wapuuze,subiri covid ikishaondoka na wakaribu yako ndipo ujifunze,

Huyu jiwe anawafanya muwe wavivu wakitumia vichwa vyenu ipasavyo.

Ila mjue afya haihitaji siasa.
 
Siamini katika viongozi wa dini hata Siku moja. Wakitoa tamko kuna masilahi yao yameguswa mahali. Hawa wasiooa hata kutunza familia hawajui siamini kama wanaweza kuwa na uchungu na watu.
 
Wakuu
Mimi kama mkatoliki mwenye imani thabiti naahidi kufuata maelekezo ya kanisa na hasa viongozi wangu mapadre na maaskofu waliosema tujikinge kuvaa barakoa, kunawa mikono na sabuni na maji tiririka, kamwe kwenye hili sitowasikiliza wanasiasa au viongozi wa serikali maana sioni kama wanaushauri mzuri juu ya ugonjwa huu
Natoa wito kwa wakatoliki wote tuusome waraka ule kwa umakini na tuhakikishe tunafuata maelekezo ya kanisa takatifu katoliki
Afya ni mali na utailinda mwenyewe na tujikinge huku tukiendelea kuomba.
Unapoteza muda tu Mkuu kuandika maana tokea Corona imeanza mpaka sasa hakuna Padre aliyekufa na corona.Kingine kuna Mungu siyo mawazo ya Padre ndiyo yanayoaminiwa maana kama Mungu aliweka tumboni kwa mwanamke kutoka kwa majimaji wa Mwanaume mpaka ukazaliwa atashindwaje kukulinda na Corona Pole kwa kutafuta kick isiyokuwa na mashiko.Kumbuka alichofanya Askofu ni kutekeleza maagizo ya Vatcan ambako huko Corona iliwatafuna hasa .
 
Sisi tushike moja la Mheshimiwa Rais la tusitishane hamaanishi corona haipo, hata kama Tanzania haipo inaweza kuingia mda wowote toka kwa majirani lakini siyo tishio kama taarifa za majirani zinavyotolewa, pia corona haijaondoa visababishi vingine vya vifo na hata ukiugua malaria haimaanishi huwezi kupatwa na ugonjwa mwingine wakati huhuo, hivyo unapougua malaria haimanishi corona inakuondolea malaria na kubaki yenyewe, tunakoelekea hata vifo vya ajari tutasema ni corona.
 
Back
Top Bottom