Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Wao ni Idara ya afya? Wanasemaje pia kuhusu Malaria?
Itakuwa imewagonga watu wao kadhaa ndo maana wameibuka na tamko la tahadhari.

Malaria tayari ilishatolewa matamko mara nyingi sana , sidhani kama ni akili kuibua hoja ya malaria wakati tunadicuss corona.

Ila nakupata , unajaribu kuwa negative, ni mtazamo wako.
 
Mkuu Cannabis ,hizo zote zimefanyiwa utafiti wa kutosha na kuruhusiwa na mamlaka husika!?

Je,GoT haioni umuhimu wa kuwaalika wakuu wa J & J, Pfizer na wengineo Chato ili waweze kukaribishwa kwenye "partnership" ya utafiti zaidi wa "gunduzi" hizi za kizalendo kama tulivyofanya kwa ile ya kutoka kwa DJ AR wa Tana!!?

Kuna kuhusika kokote kwa taasisi zetu za utafiti, usimamizi na tiba kama NIMRI, IHI, MUHAS, AKU, TMDA, TBS na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala!!?
 
Wakotoliki tulisha wazoea hata mala ya kwanza ndio walikuwa wa kwanza kufunga makanisa yao, wanauakika upi kuwa Tanzania Kuna korona wakati shughuli zote zinaendelea kama kawaida?..
Umewazoea kwa lipi! Kanisa Katoliki lina idadi kubwa ya hosipitali ambako hao wanaobanwa pumzi huenda wakatibiwe, wameona idadi imeongezeka ya watu wanataka valvu zao zizibuliwe hewa ipite, hivyo wao wanazo takwimu.
 
Mambo mengine ni kumwachia Mungu tu. Hivi mnadhani USA wanakokufa watu 2000+ Hawana mbinu kama sisi?...
Mkuu nimekuelewa sana, binafsi napingana na serikali inavyowaaminisha watu wake kuwa tz huko hakuna korona, wangekubali kuwa ipo na tunaishi nayo kama tunavyoishi na ukimwi kansa nk, juzi tu tz imetoa takwimu ya wagonjwa wa ukimwi na virusi vya ukimwi kwanini takwimu za korona zinafichwa?
 
Mkuu Quinine,

Umeleta mbio mbio huu waraka ukitarajia kilichoandikwa kitaiudhi serikali, pole sana...
Tanzania hakuna korona, raisi ameshasema tumeishinda hayo mengine ni dhana zenu tu, hata ikija tz haitaweka lockdown bali itafanya kama ilivyofanya mwanzo
 
Ni kweli, lakini kauli uliotumia very controversial kwa kiongozi wa juu wa Kanisa..

Na ofcourse mbona barua au waraka umetoa tu tahadhari na si taarifa kamili kama ugonjwa upo.! Asilimia mia naamini hawawezi 'kuikanusha' hata kama wakiingiliwa na mamlaka.
Waumini wa kikristo hasa katoliki wanajisahau sana na kuona viongozi wao wapo juu kuliko viongozi wa serikali ila awamu ya huyu bwana hadi maaskofu wamesanda, waraka umetolewa kijanja mno wameshindwa kukiri kilichopo tz
 
Thubutu,atawajibu wengine tu,lakini si (Nasadiki kwa Kanisa moja) Anawajua vizuri sana wale jamaa!
Weee, saivi katoliki sio kama zamani hadi maaskofu na mapadri ni mwendo wa kusifu na kuabudu tu, we angalia hadi huo waraka umeshindwa kuandika kilichopo sasa bali wamezunguka zunguka tu ile ingekuwa enzi za zamani wangefunguka live
 
Mkuu Cannabis ,hizo zote zimefanyiwa utafiti wa kutosha na kuruhusiwa na mamlaka husika!?
Je,GoT haioni umuhimu wa kuwaalika wakuu wa J & J, Pfizer na wengineo Chato ili waweze kukaribishwa kwenye "partnership" ya utafiti zaidi wa "gunduzi" hizi za kizalendo kama tulivyofanya kwa ile ya kutoka kwa DJ AR wa Tana!!?
Kuna kuhusika kokote kwa taasisi zetu za utafiti, usimamizi na tiba kama NIMRI, IHI, MUHAS, AKU, TMDA, TBS na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala!!??
Zinauzwa pharmacy na mpaka sasa serikali ipo kimya, labda wameziruhusu. Tunaweza kugeuzwa fursa na wajanja wa mjini, mtu akiweka pilipilo kali, anachanganya na ndimu, tangawizi anaipachika jina kiboko ya CoViDo basi anaanza kupiga hela.
 
Leo vyombo vya ndani na nje vimekuwa mstari wa mbele kupotosha waraka uliotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania ( TEC) kuhusu kujilinda na virusi vipya vinavyosababisha virusi vya corona vilivyogunduliwa Afrika ya Kusini na Uingereza.

Wakati Baraza la Maaskofu likiwaomba watanzania kuchukua tahadhali kwa kuwa Tanzania sio kisiwa, vyombo vya habari vimesema Baraza limesema Tanzania kuna virusi hivyo vipya.

Ukweli ni kwamba ukisoma waraka huo hauna tofauti kubwa na ule walioutoa mwaka 2020 mwezi wa pili ukiwaomba watanzania kuchukua tahadhali.

Ikumbukwe kuwa dini na viongozi wote wa imani wanalo jukumu la kuwakumbusha waumini kutenda na kuishi maisha mema.

Hili ndo walilofanya Baraza la Maaskofu kuwakumbusha waamini wao na watanzania kwa ujumla kutokubweteka na kuendelea kufuata miongozo iliyotolewa na wizara ya afya ya kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuepuka misongamano isiyo ya lazima na mingine mingi.

Ni kwa msingi huo ukisoma waraka huo hakuna popote unaposema Tanzania kuna virusi vipya vinavyosababisha corona au virusi vya zamani.

Hii yote inatokana na tabia iliyozuka siku za karibuni ya vyombo vya habari kuacha misingi ya weledi ya kazi zao ya kusoma mstari kwa mstari kila chapisho litolewalo na kupotosha jamii.

Watanzania waache upotoshaji huu wa vyombo vya habari kuhusu tamko la baraza la Maaskofu waendelee kuchukua tahadhari kama serikali inavyoshauri.

Ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa Tanzania hamna COVID-19, serikali haijawahi kuwaambia wananchi kuacha kunawa mikono, kuvaa barakoa au kuwa katika misongamano isiyo na umuhimu.

Siku zote serikali imesisitiza watanzania kuendelea kutomjaribu Mungu na kuchukua tahadhali zote dhidi ya COVID-19 baada ya Mungu kuiondoa Tanzania.

Kwa mantiki hii watanzania wapuuze vyombo vya habari vya nje na ndani pamoja na mitandao ya kijamii iliyopotosha waraka wa Maaskofu.

Sambamba na hilo, Watanzania wapuuze vyombo hivihivi vilipotosha alichosema Waziri wa fedha Dr. Philipo Mpango wakati akiongea na wafanyakazi wa wizara hiyo.

Dr. Mpango amesema pamoja na kuwa Tanzania hamna COVID-19 wafanyakazi wachukue tahadhali kwani Tanzania sio kisiwa.

Kama kawaida vyombo vya habari vikapotosha na kusema Tanzania kuna COVID-19 kulingana na maelezo ya Dr. Mpango.

Watanzania tuendelee kuwa watulivu na kuisikiliza Wizara ya Afya yenye dhamana ya kulinda afya zetu.

Serikali yetu ni sikivu likitokea lolote itatwambia ila sio porojo zinazochagizwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii isiyofuata maandili ya uandishi wa habari
 
Kuna chombo cha habari cha ndani kilichouripoti huu waraka ?

Vyombo vya ndani utakuwa unavionea kwa kweli.
 
Wakuu
Mimi kama mkatoliki mwenye imani thabiti naahidi kufuata maelekezo ya kanisa na hasa viongozi wangu mapadre na maaskofu waliosema tujikinge kuvaa barakoa, kunawa mikono na sabuni na maji tiririka, kamwe kwenye hili sitowasikiliza wanasiasa au viongozi wa serikali maana sioni kama wanaushauri mzuri juu ya ugonjwa huu
Natoa wito kwa wakatoliki wote tuusome waraka ule kwa umakini na tuhakikishe tunafuata maelekezo ya kanisa takatifu katoliki
Afya ni mali na utailinda mwenyewe na tujikinge huku tukiendelea kuomba.
 
Naapa kuitunza na kuilinda imani ikiwa ni pamoja na kuheshimu maelekezo ya viongozi wangu wa dini.
 
Back
Top Bottom