WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Zitasikika sauti zikisema "Wametumwa" au "Wanatumiwa" etc. tumsubiri "Comical Ali" atakuja kukanusha yaliyomo kwenye waraka huo. Nina hamu pia kumsikia ule Profesa wa sheria na katiba labda atalipa lecture kanisa kuhusu hali ya demokrasia nchini.
 
Nilikuwa nimekata tamaa hata kuhudhuria ibada baada ya ku note baraza la maaskofu wapo kimya, nikajua wameamua ku mute kwakuwa Mkatoliki mwenzao yupo ikulu.

Kwa huu waraka kwakweli imenibariki, jumapili ijayo ntakuwa wa kwanza kuingia ibadani na fungu langu la kumi juu.

Asante baraza la maaskofu asante kanisa katoliki.

Ila hapo namchungulia mnafiki moja atakavyojikana mwenyewe hahaha.... Pengo Mungu anakuona ujue
 
mkuu Mungi si wewe Mwenyewe Hata sisi wana habari tulikuwa tumekata tamaa
 
Ni waraka wa kwaresima 2018 tuusome una mafundisho makubwa kwa maisha ya kila mmoja wetu, Mimi nimeumaliza na nitaurudia tena na tena kujifunza "neno la mababa" tusiushushe kwa kujadili point moja tu, na kimsingi hatupaswi hata kujadili bali kuishi yale tuliyoaswa kutenda wakati huu wa "Neema".

Kwaresima ni " kuishi moyoni" sio "kuishi mitandaoni"

Nawatakieni kwaresima njema, tukutane baada ya siku 40, kwaherini.
 
Je wanalipa kodi? TRA wana kazi ya kufanya hapa.
 
Ni upuuzi uliopindukia kutenga siasa na imani/Dini za watu. Siasa zikivurugukika, amani hakuna na kuabudu hakuna! Tusidanganyike-Hongera Askofu Kakobe, hongera kanisa Katoriki. TANZANIA ni yetu sote.
Nini ni msimamo wa BAKWATA katka hili?
Je Askofu Pengo anaunga mkono tamko la maaskofu wenzake?
 
Nimeupenda sana maana umeeleza ukweli na hauna hata tone la unafki.

Nanukuu baadhi ya mistari UK 11 ambayo imegonga mulemule..
"Maana yake ni kwamba shughuli za vyama vya siasa kama vile mikutano ya ndani ambayo ni haki ya kila raia zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba na sheria za nchi.

Vilevile baadhi ya vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, na hivyo kupunguza wigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari maoni na kujieleza.

Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambamba na kuminywa kwa uhuru wa mahakama na bunge kwa njia ya kuminya haki za wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi kikatiba"

Mwisho wa kunukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…