WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Kanisa Katoliki Tanzania limetoa waraka kwa ajili ya kuwaandaa waamini wake kwa ajili ya kipindi cha Toba, kinachoanza rasmi Jumatano ijayo tarehe 14 Februari 2018 [ambayo ndiyo siku ya wapendanao, Valentine. tusherehekee kwa Toba eeeh tafadhalini!]. Kipindi hicho hujulikana pia kama KWARESIMA, ambacho kinahitimishwa na JUMA KUU na kisha sikukuu ya PASAKA.

Kama una haraka sana, soma ukurasa wa 11 na 12 (kurasa orijino) au ukurasa wa 14 na 15 kwa kurasa za PDF. Naambatanisha waraka huo.
Karibu! Ni nondo Kali!

Rais anasema Eti anaomba muendelee kumuombea ili Urais usimpe kiburi na jeuri
 
Sawa wale wanaopenda kusifia nguvu ya usalama wa TAIFA na waje sasa walishambulie Kanisa Katoliki.
 
Kanisa Katoliki Tanzania limetoa waraka kwa ajili ya kuwaandaa waamini wake kwa ajili ya kipindi cha Toba, kinachoanza rasmi Jumatano ijayo tarehe 14 Februari 2018 [ambayo ndiyo siku ya wapendanao, Valentine. tusherehekee kwa Toba eeeh tafadhalini!]. Kipindi hicho hujulikana pia kama KWARESIMA, ambacho kinahitimishwa na JUMA KUU na kisha sikukuu ya PASAKA.

Kama una haraka sana, soma ukurasa wa 11 na 12 (kurasa orijino) au ukurasa wa 14 na 15 kwa kurasa za PDF. Naambatanisha waraka huo.
Karibu! Ni nondo Kali!
dokta Slaa njoo huku....ona sasa Wakatoliki wenzio wanamletea chokochoko partner ako bana!
 
Page 12
"Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeainisha utaratibu wa kazi na shughuli za vylma vya siasa. Ili kuhakikisha hvamba ka'"'ina shughuli z vyamavya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vlgezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. Hata hivyo, shughuli za, sirsa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola. Maana yake ni kwamba shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa, kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila rua, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi.

Vile vile baadhi ya vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, na hivyo kupunguza uwigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari, maoni na wa kujieleza. Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambaba na kuminya uhuru wa mahakama na bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya Kikatiba.

Katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Kumekuwapo pia hali ya vurugu katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi hizi zinaacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine. Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Tukiiachia hali hii izoeleke tushishangae huko mbeleni kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa."
Duh!
 
Mara nyingi nyaraka za wakatoliki huwa zinatetemesha sana serikali
Hahaaahaaaa mkuu hasa ukitilia maanani kuwa mkulu ni mshirika huko asije tu akaghaili au kususa kwenda kusali.
 
Hahaaahaaaa mkuu hasa ukitilia maanani kuwa mkulu ni mshirika huko asije tu akaghaili au kususa kwenda kusali.
Kwanza akatubu ndipo mambo mengine yafuatie!

Sijui Kwanini Yule askofu mkubwa wa kanisa anashindwa kumshauri Swahiba wake atubu!
.msimamo wa TEC sometimes huwa unatofautiana na msimamo wa kanisa!
 
Hapa kadinali pengo sijui atasema nn maana yeye kila jambo hujiweka upande wa serikali utafikiri kanisa katoliki ni tawi la CCM kama ilivyo UVCCM au jumuiya ya wazazi.

Pengo atasema nini wakati sahihi yake kwenye waraka ni jina la tatu.
 
Hahaaahaaaa mkuu hasa ukitilia maanani kuwa mkulu ni mshirika huko asije tu akaghaili au kususa kwenda kusali.

Alishaghairi na kanisa halisumbuki na watu kama yeye. Si unamuona huwa wanaenda kwa TB Joshua.
 
Inatia moyo sana kuona Baraza la Maaskofu nchini limeanza kulaani na kukemea huu UdU wa kutisha unaoendelea nchini katika awamu hii.

Waliokuwa wanaikosoa Serikali hii dhalimu walitusiwa majina mbali mbali ikiwemo wasaliti, majizi, wapiga madili na matusi mengine chungu nzima.

Sasa hata Baraza hili la Maaskofu limechoka kuendelea kukaa kimya huku UdU nchini ukizidi kushamiri kwa kasi ya kutisha na hivyo kutishia amani ya nchi yetu.

DU apingwe kwa nguvu zote za Watanzania wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu ili aheshimu katiba, Bunge, mahakama, sheria za nchi, sheria za manunuzi ya Serikali, sheria za kutoa fedha hazina etc.

Naendelea kusema huyu jamaa ni janga kubwa sana la Taifa letu na ni mtu hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu.

Nzi Elli Tetty Sky Eclat Salary Slip zitto junior MENGELENI KWETU tindo Saint Ivuga Erythrocyte lusungo Retired
 
dokta Slaa njoo huku....ona sasa Wakatoliki wenzio wanamletea chokochoko partner ako bana!
Yeye ameshauri upinzani upitie njia ya mahakama kupinga huu udhalimu. Nafikiri mkakati huu ni wakutilia nguvu. Najua mwanzo walisema wangeenda mahakamani sijui iliishia wapi?
 
Wananchi tuusomeni huu Waraka unaujumbe mzito, jitaidini kuusoma wote... naona Kanisa limeamua kugeuzwa kichaka cha maficho ya waonezi, wakandamizaji na wasio na hofu kuu ya mungu. Kwa hili nawapongeza sana na kuwasha taa katika hili giza....
 
Back
Top Bottom