WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Sindano imewaingi ee...????
Sasa mtulie mupewe ukweli japo hilo sio dhamira yenu na huwa hamupendi.

Waraka wa Kanisa Katoliki haujawahi liacha Taifa lolote salama pale ulipopuuziwa na viongozi waliojawa Viburi na Dharau kwa maisha ya hapa Duniani na mifano ipo.
Nani atulie?
 
Ila kiukweli hata RC no zinasomeka sasa hivi,sadaka ziko hoi,vyuo vyao wanavyomiliki siku hizi inapita hata miezi 4 wahadhiri hawajalipwa hela zao ni Changamoto pia wanazipitia.
Kama umeusoma huo waraka vizuri usingeandika mambo ya ajabu kiasi hiki...!!!
 
Hivi hapo dawa ni kutokuwa dikteta au kufuatilia wanaolalamika kuminya demokrasia?........kwa phd feki utaona kuanzia kesho kifuatacho Azam TV!!
 
Ndiyo maana wenzao wanasoma miaka 7 kabla hata ya kuupata upadre siyo kina Kakobe na Gwajima. Mtu anaweza kukutukana kwa kutumia maneno mazuri bila kutumia maneno ya Mange maana ndiyo maana ya usomi. Lakini ukianza kutukana kama walevi wa vilabu za pombe za kienyeji elimu yako inakua na msaada gani kwako?

Ukisoma huu waraka hawamsemi Magufuli kama Magufuli wanaisema serikali na watendaji wake. Na ujumbe unawaendea waumini wao ili waelewe jinsi gani mambo yanavyoendelea katika maisha yao ya kila siku. Ukisimama katika mimbali na kumshambulia rais wa nchi unakua kama mwanasiasa kama walivyo kina Lema. Hawa wakatoliki wanajua namna ya namna gani kuishauri serikali siyo kuitukana maana wanajua serikali ipo juu kimamlaka.

Shule ni nzuri sana angalia Dr Slaa alipokua UKAWA na UKAWA ya sasa ya mipango inayoishia kutangazwa magazetini tu bila kufanyiwa mikakati ya maana.

Hawa maaskofu kama wangekwenda katika vyuo vikuu vya kawaida wangetoka wakiwa madaktari. maana falsafa inasomwa miaka miwili, theology miaka mitatu na mwaka mmoja ni juu ya uongozi wa kanisa na jumuiya ya kanisa. jumla miaka saba lakini ma jesuit wanasoma miaka zaidi ya kumi kabla ya upadre. mpaka kuwa na masters degree kabla hujaupata upadre.

ndiyo maana huwezi ona wakatoliki wakijipendekeza pendekeza kama yule aliyetukanwa na Mange ama yule aliyekua mfuasi wa Lowasa.
Unapowalinganisha Kakobe na Gwajima na hao mapadre unakosea sana, they are two different people. Wakati kundi la kwanza wanafuata mafundisho ya Yesu as they are, kama kuponya magonjwa, kutoa pepo, kuhubiri injili ya wokovu just like what Jesus and the disciples did, hawa wengine hawayafanyi hayo na infact wanayapinga.
Hawa watu hawalingani kabisa, usidanganyike.
By the way, Yesu alikaa na wanafunzi wake for only 3 years na baada ya kuondoka waliuwasha moto wa injili vibaya sana mpaka leo hii tunamjua Mungu anayeokoa japokuwa walipingwa na kuuawa sana na utawala wa KIRUMI. So, again hawa hawalinganishwi kabisa na off course wanatumikia deities tofauti kabisa, japo at face value huwezi kulijua hilo, limefichwa machoni pako.
 
Aliye karibu na Kadinali Pengo aniambie yupo katika hali gani

Kardinali Pengo na Maaskafu wenzake wajiandae kuhojiwa Uraia wao na Mapato ya Sadaka!!!Na wasipochukua hatua za maksudi watapotezwa katika mazingira yasiyojulikana na watu wasiojulikana.....!
 
Baraza la Maaskofu siyo wasimamizi wa mambo ya siasa, wao kama "wachungaji" wanao wajibu mkubwa sana katika jamii.

Huwa inashangaza kwamba Serikali huwa zinapenda kuyatumia makanisa kuendeleza ajenda zao. utakuta kiongozi anakwenda kanisani na analitumia kama platform ya kuendeleza ajenda yake. atatoa kauli, ataomba "aombewe". ataomba viongozi wa Kanisa wawaambie waamini wao mambo kadha wa kadha. Viongozi wa Serikali na wanasiasa wanatambua nguvu za viongozi wa dini. lakini hawataki viongozi hao hao waongee mambo ambayo hayapendezi kwa upande wa serikali au wanasiasa, hasa inapoonekana viongozi wa serikali wamekiuka kanuni ambazo wao wenyewe wameapa kuzilinda. Yesu Kristu alipambana sana na VIONGOZI WANAFIKI. Injili ya Mathayo sura ya 23 yote inaongelea Makaripio makali ya Yesu dhidi ya viongozi wanafiki.

Kuhusu mazishi ya Kingunge, nadhani ni vema ukiongea vitu ambavyo una uhakika navyo. Kingunge alianza mchakato wa toba, hivyo kwa kiwango fulani Kanisa limemheshimu japo hakupewa hadhi ya juu kabisa ambayo ni kuzikwa kwa Misa Takatifu ya Wafu, kwa sababu hakukamilisha mchakato wa Toba.
Umefafanua vizuri sana Mkuu! Asante.
 
CHONDE CHONDE BANDUNGU SIZONJE HAJARIBIWI.ATAZIFUNGIA HIZO TAASISI ZENU
 
BARAZA KUU LA MAASKOFU (TEC)

Baraza hilo limesema, “Kwa mwaka huu wa 2018 kipindi hiki ni cha kujitafakari mbele ya Mungu na kufanya toba hususan uhai wa amani yetu kwa njia ya matendo ya huruma, haki upendo na amani kwa jirani zetu.”

ASKOFU MKUU KAKOBE

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu" amenukuliwa akisema Kakobe.
 
Ni waraka wa kwaresima 2018 tuusome una mafundisho makubwa kwa maisha ya kila mmoja wetu, Mimi nimeumaliza na nitaurudia tena na tena kujifunza "neno la mababa" tusiushushe kwa kujadili point moja tu, na kimsingi hatupaswi hata kujadili bali kuishi yale tuliyoaswa kutenda wakati huu wa "Neema".

Kwaresima ni " kuishi moyoni" sio "kuishi mitandaoni"

Nawatakieni kwaresima njema, tukutane baada ya siku 40, kwaherini.
Asante sana mkuu.
 
wata m tundulisu kakobe

hawa jamaaaa damu damu wanashindana kumwaga
 
Unapowalinganisha Kakobe na Gwajima na hao mapadre unakosea sana, they are two different people. Wakati kundi la kwanza wanafuata mafundisho ya Yesu as they are, kama kuponya magonjwa, kutoa pepo, kuhubiri injili ya wokovu just like what Jesus and the disciples did, hawa wengine hawayafanyi hayo na infact wanayapinga.
Hawa watu hawalingani kabisa, usidanganyike.
By the way, Yesu alikaa na wanafunzi wake for only 3 years na baada ya kuondoka waliuwasha moto wa injili vibaya sana mpaka leo hii tunamjua Mungu anayeokoa japokuwa walipingwa na kuuawa sana na utawala wa KIRUMI. So, again hawa hawalinganishwi kabisa na off course wanatumikia deities tofauti kabisa, japo at face value huwezi kulijua hilo, limefichwa machoni pako.
Usilinganishe kanisa katoliki na hivyo vikundi vya kihuni (ministries).
 
Kardinali Pengo na Maaskafu wenzake wajiandae kuhojiwa Uraia wao na Mapato ya Sadaka!!!Na wasipochukua hatua za maksudi watapotezwa katika mazingira yasiyojulikana na watu wasiojulikana.....!
Thubutu..!!!
Hawezi ligusa Kanisa Katoliki kamwe na wenyewe wanalijua hilo.
 
Kwahivyo atubu au maana sijaelewa...awape na watumishi haki zao kama wanavyo stahili
 
Back
Top Bottom