Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

kweli hata mimi sijamtambua huyo M2,ila nahisi atakua mbunge wa ufipani kwani haishi kulalama eti MM alionewa
 
huu waraka sasa uaze kutumika rasmi ACT - Wazalendo.
 
Katika sakata la kuvuliwa uanachama kwa Zitto, Mkumbo na Mwigamba. Kulikuwepo na MM1, MM2, MM3 na mpaka akina Zito wanaondoka MM2 hatukuambiwa ni nani. Kwa hapa tunamlaumu mwenyekiti wa chama kwanini hakututajia MM2 ni nani? Mbowe alimvumilia bila kumtaja akiogopa chama kingesambaratika. Kumbe alijidanganya mwenyewe leo tunayaona madhara ya MM2.

Malengo yao ilikuwa Zitto na wenzake watangulie halafu yeye atafuata. Mtakumbuka Zitto alisema Wabunge wengi wa CHADEMA wataondoka na alikuwa na uhakika sana. Kwa wana CHADEMA ni kumshukuru Mwenyekiti Mbowe kwa kumpokea Lowassa. Ingawa alikosea kutomtaja MM2 mapema Imekisaidia chama kwa baadhi ya Wabunge wasimfuate Zitto na MM2 SLAA.

CCM walicheza hii deal muda mrefu mno bila CHADEMA kujua. Walijua Lowassa akiingia CHADEMA na jinsi alivyotukanwa na CHADEMA chama kitasambaratika. MM2 aliwategeshea wenzake kwa kuanzisha mazungumzo na Lowassa, kwa sababu alijua kwa vyovyote Lowassa angekuja CHADEMA lakini asingekubali kutokugombea urais. Hivyo yeye lengo ilikuwa kuhamia ACT ili agombee urais na kugawa kura za Urais.

Tatizo ilitokea kwa kuchelewa kwa Lowassa kuja CHADEMA mapema. Na wakati huo MM2 ndie alikuwa ameshapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya
CHADEMA hivyo akawa anashindwa atahamaje. MM2 alikuwa anajua fika kuwa CHADEMA hawatashinda hata wakimweka yeye, hivyo yeye alikuwa anaangalia maslahi ambayo angeyapata ndani ya CCM.

Wengi hamwezi kuamini haya lakini nafikiri mumeweza kumwelewa Slaa tangu ametoka
CHADEMA alipotangaza pale Serena. Na kwa waliomtizama alipoongea jana kwenye Star TV huyo ndio Slaa mliyekuwa mnamtegemea kuwa ni mpinga ufisadi. Jiulize, je Lowassa ndio fisadi peke yake katika nchi hii? Kama Lowassa ni fisadi mbona hata kesi haikupelekwa mahakamani hadi leo?

Najua wengi mnazo simu za smart phone naomba muingie Youtube na kutype "Maneno Mazito ya Mhe. Lowassa alipojiuzulu". Najua baadhi yenu mumeshaisikiliza. Jiulize baada ya kuisikiliza, ilikuwaje kamati ya Mwakyembe iende mpaka Marekani kuchunguza Richmond na wakarudi na kuwakilisha ripoti bungeni pasipo kumhoji mtuhumiwa?

Mafisadi wengi wamebaki CCM lakini Slaa jana anasema Magufuli ni Mwadilifu na ndie anayefaa kuwa rais na kwa kuwa amesema atafungua mahakama ya mafisadi akiingia madarakani wakati mahakama hizo zipo eti ataweza kuwafunga mafisadi wote wa CCM.

MM2 anataka kutuambia kuwa Lowassa tangu ameingia
CHADEMA WanaCHADEMA wote ni mafisadi na CCM wote ni wasafi. Jiulize Je Lowassa kaja CHADEMA na sera, katiba zake? Au atafuata katiba za chama. Ina maana huyu MM2 anapohamia ACT atahamia na katiba, Sera zake?? Huyu huyu Slaa miezi mitatu nyuma alikuwa akiimba kuwa CCM hata ukimpeleka Malaika hawezi kudumu mle ndani(CCM) atabadilika na kuwa fisadi.

Jana hiyo akiwa Star TV aliendelee kumsifia Zitto kuwa yeye na chama chake ndio wamechukua ajenda ya
CHADEMA ya ufisadi. Muulizeni MM2 Slaa kama anasema ACT wamechukua ajenda ya CHADEMA inakuwaje mgombea urais wa ACT asiwe bora kuliko Magufuli?

Magufuli mwenyewe jana ripoti iliyotoka mliona katika wizara yake ya ujenzi ilivyolipa watu hewa mabilioni, Magufuli huyu aliyeuza nyumba za serikali mpaka kwa mahawara zake leo hii anakuwa mwadilifu kwa DR WILBROD SLAA! Muulizeni zile 4.5bilions alizotunza Uingereza ndio zimembadilisha?

Bora ya Zitto yeye za kwake alikuwa anazirudisha kwa njia ya Western Union kutoka Ujerumani zilisaidia Watanzania. Huyu MM2 ndie aliewachonganisha Mbowe na Zitto, mpaka wakagombana na kukosa kuaminiana wakati walikuwa marafiki/Ndugu, mtu na mdogo wake wa kuzaliwa kabla ya kuja MM2. Kwani Zitto aliona hasikilizwi, anayesikilizwa zaidi ni MM2.

HUYO NDIYE DR WILBROD SLAA MPAMBANAJI WA UFISADI. MSICHEZEE SIASA, SIASA NI MCHEZO WA AKILI, KAMA HUNA AKILI HUWEZI CHEZA SIASA.
 
JET SALLI

Huna hoja, ila umejitahidi kuandika maneno mazuri yasiyo na hoja, pole sana
 
Last edited by a moderator:
JET SALLI

Huna hoja, ila umejitahidi kuandika maneno mazuri yasiyo na hoja, pole sana
 
Last edited by a moderator:
JET SALLI
Kamanda huna hoja unalia lia tu. Dr Slaa awe MM0 ,MM1, MM5, MM6 you name it! Bado anabakia ni kamanda na champion wa vita juu ya ufisadi.! Fullstop! Mtakuja vizuri kujieleza mara baada ya uchaguzi pale mtakapoona maajabu ya wananchi.

Msidhani wananchi hawana akili mnawapelekapeleka tuu. Anakuchekea usoni lakini kwa siri anaenda kukuchinja kama hana akili nzuri vilee.
 
Last edited by a moderator:
Usipingane na viongozi wako wamesema Jamaa siyo ila huko ni kama kanisa atatubu Kisha kuwa msafi tafsiri rahisi akiwa kule nishetani ila akiwa kwetu ni malaika SHAURI yao wwalishindwa wenyewe sasa kimya.
 
of course hata mwigamba alisema anayefata kufukuzwa ni slaa.
 
JET SALLI

Presha presha presha,
Mawazo mawazo mawazo....
Mbowe kachemsha.
Kama hayo unayosema ni kweli Mbowe naye kwshakuwa kama wanaccm, anaficha siri na kukumbatia waovu kwa manufaa yake binafsi.

Kwa maneno haya huoni kuwa ngome ya chadema imedhoofu?
Na wa kuilaumu ni chadema yenyewe?
Na huoni unamshusha hadhi Mbowe kuwa kapigwa chenga kizembe
 
Last edited by a moderator:
Chadema imeshauzwa...

Ni mwendelezo wa kambi ya mgombea wa CCM, asiye na ugomvi na chama bali uchu wa madaraka...

Chadema mwaka huu haina mgombea, isubiri 2025 labda...
 
Back
Top Bottom