Waraka wa Baraza la Maaskofu (TEC) kuhusu uendeshaji Bandari utasomwa kila Jumapili kwa wiki 6, utasomwa pia kwenye vigango

Mkuu unamaanisha ni agizo kwa kanisa takatifu la mitume,kuwa huo waraka usomwe kesho Hadi vigangoni sio? Itakuwa safi Sana!
Waraka WA tamko la maaskofu 37 unakiuka maadili ya Taasisi kubwa na yenye kuheshimika ya wakatoliki. Tamko hili hatutakosea tukiliita la kichochezi. Mkataba umesainiwa, Bunge ambao ndio wawakilishi WA wananchi wameuridhia, Leo inatokea Taasisi kubwa na yenye heshima inapinga, hii haingii akilini, hapo sasa naanza kuamini yanayoongelewa, yakuwa, Baraza la wakatoliki wanalengo kingine kikubwa kuliko Bandari, nalo NI kumchafua Rais Samia, wkilenga uchaguzi WA 2025 agombee mkatoliki.. Mnayemkusudia NI mtu mahiri lakini njia mnazopita mtamuharibia. Taassisi NI kubwa, na imejijengea heshima kubwa Duniani, lakini Kwa Hilo mmeteleza.
 
Kama watausoma basi tutakuwa na bahati mbaya ya kuwa na Serikali dhaifu. Binafsi nitaenda Kanisani kama kawaida yangu. Wakianza kuusoma huo Waraka, nitatoka nje!
 
Unazungumzia habari za magaidi wa kibiti,tuache kidogo tupo kwenye bandari,huu ni urithi wa Watanzania na watoto wao na wajukuu wao.
 
Mkataba unakurudishaje utumwani? Kwa nini huongelei mafanikio ya DP World Southampton Uingereza?
 
Mkuu kama umekula hela ya Dubai,jiandae kulipa au kuolewa na Mwarabu,nenda kanisani labda watakusamehe.
Waambie wausome huo waraka miaka 5 mfululizo ila watanzania watawajibu kuwa mbona DP World kaja na tunachoona ni mafanikio na mapato kuongezeka?
 
Waambie wausome huo waraka miaka 5 mfululizo ila watanzania watawajibu kuwa mbona DP World kaja na tunachoona ni mafanikio na mapato kuongezeka?
Thubutu kwani Kwenye Madini tumepata nini na kwenye gesi je?

Hayo mapato mtajaza nyie chawa na waarabu tu
 
Yaani watu wanabadili sheria za Nchi kwa sababu ya kumkabidhi Mwarabu urithi wa Taifa? Watu wakae kimya? We kweli unajielewa?
 
Kwa namna mambo ninavyo yaelewa,Roman Catholic wakikataa jambo lolote kwa uwazi Hivi hakuna namna zaid ya kukubaliana nao au uliache jambo Hilo.Hawa jamaa Huwa hawazungumz kwa kukurupuka Hadi hapo walishaisoma Raman yote kuhusu jambo hili!Roma Catholic ni kanisa lililopgana vita nyingi sana za kimwili.Kumbuka Baraza hili ndilo huamua kiongozi wa nchi awe nani pia Kumbuka Maalim Seif alipo nyang'anywa ushindi na Jecha 2015 aliandika barua kwa Papa kuomba amsaidie kuupata Uraisi pale Zanzibar
 
Je aliupata?
 
Hakuna sehemu wamesema samia muislam, akili visoda ndo wameamua kuweka hitimisho kwa namna hiyo, kwan samia ndo rais wa kwanza muislam Tanzania?
 
Waraka huo una vipengele vingi.

Nashauri baada ya hizo wiki sita, waanze kuwa wanasoma kipengele kimoja tu cha waraka kwa kila jumapili hadi itakapofika 2025
 
Waulize vizuri waliokuleta watakwambia.., na ikibidi kama unaweza kutumia akili yako vizuri fuatilia history ya Nchi hii utajuwa hao ni nani, na ikiwezekana walinganishe kama wanaendana na wale.
 
Wamezoe kuingiza magari Yao pale bandarini Bure, bila Kodi, Sasa wamekutana na mwarabu amewadai Kodi wameshaanza kulalama

Hii bongo Kila mtu anachunga maslahi yake
 
Hata tusiokuwa Wakristo, tutaenda makanisa ya karibu kujumuika na wenzetu kwenye kutengeneza historia hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…