KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,893
- 3,145
Hata kabla ya hilo Bunge la Katiba kuanza vikao,sheikh Ilunga alikuwa kaisha weka wazi kuwa Katiba mpya haitapatikana kwa kuwa KANISA ndiyo litaupinga mchakato huo.Mwaka 2014 Tamko la Maaskofu Wakatoliki TEC,Tasisi ya Waadventist Wasabato na Baraza la Kikrito Tanzania lilisitisha Bunge la Katiba Mpya baada ya kuona CCM imepora mjadala na kutaka kufanya wanavyotaka wao huku wakipuuza maoni ya wananchi.
Rais Kikwete akatumia busara za Walaka ule akaachana na mchakato ule uliokuwa unaenda kinyume na Malengo.
"...... Sisi tunaona mchakato wa mabadiliko ya katiba unapokwa na wanaccm wenye wabunge wengi huku Spika akitumia nguvu na uhabe kupitisha maoni binafsi nje yanwaliyotoa wananchi,. Pia tunaona vijembe na matusi yakiendelea bungeni na serikali kufunga tovuti ya Kamati ya kukusanya maoni ni dalili mbaya kuwa serikali haina nia njema.....". Ilisema sehemu ya Walaka huo.
Rais Kikwete alitumia busara kuusitisha mchakato huo wa Katiba Mpya Mwaka 2014,tukumbuke nani alikuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo la kutafuta Katiba Mpya,ni Rais wa Sasa,Mh Samia Suluhu Hassan.
Video yake akiyasema hayo hipo YouTube hadi leo.