Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Teuzi na upandishwaji vyeo lazima vifanyike kwa kuangalia sifa na vigezo vya mtu husika.
Lazima viwe 'based on merits' siyo sifa ya udini au ukabila.

Uteuzi wa DAS juzi kule Kisarawe hawajauona? Alihamishwa UDOM na serikali, serikali hiyo hiyo ndio imemteuawa.

Kuna pointi za msingi za kutilia maanani, ila mengine waulizeni waislamu wenzenu walioko serikali nafasi za juu.

Hilo ni wazi hawajafanya consultation ipasavyo, mfano tu ktk majina yaliyoandikwa kuna mtu ni ME kapewa KE, na KE kapewa ME.

Mzee Kikwete na Mwinyi wapo wangewasaidia vizuri taratibu za uajiri, upandishwaji madaraja na uhamisho kwa mtimishi wa umma zikoje.

Pia, suala la ugaidi ama kujihusisha na viashiria au vitendo vya ugaidi hata kupelekea watu kupelekwa rumande/gerezani hili liko wazi. Kuhusu kufungwa ama hata kuuawa hata wakristo wengi wako jela hata kesho na wengi ni marehemu sasa.

Pongezi kwa shura kutoa mawazo yenu, mmetimiza haki yenu kikatiba na kwa ujasiri mkubwa.
 
Sheikh Mkuu siyo Mufti tafuta maana ya Mufti
 

Ni kweli huenda ajira nyingi wako wakristo, ila kuna kitu ambacho hamtaki kukubali juu uwiano wa kielimu baina ya sisi na wao. kundi moja lilizingatia elimu dunia na lingine elimu ya dini, sasa linapokuja suala la utaalamu mwenye elimu dunia anaonekana kapendelewa.

Kwa mfano, leo tuanze kujilinganisha na makabila kama wachaga, wahaya na wanyakyusa kielimu tutapotezana maana wenzetu mazingira yao yaliwafovour wakoloni na kuweka huduma ikiwapo mashule
 

Hiyo propaganda kuwa wakiristo ndo wanaothamini elimu zaidi kuliko waislamu imepitwa na wakati
Waislamu waliosoma ni wengi sana siku hizi hata Nyerere kabla hajang'atuka alikiri hivyo
 
Hahaha, nilijua utaleta hayo majigambo...!

Leta na zile picha zako za nchi za Nje mbali na Tanzania, pia usisahau vitabu vyako vinavyosomwa Duniani kote.

Sasa ukiijua hiyo historia...then what?
Azarel,
Ningetaka kujigamba nisingeweka hayo ambayo hakika ni yangu kweli.

Ningeweka vitu hapa hujapata kuviona kutoka kwangu.

Ndiyo hiyo "so what," najua vitu hivi kwa utafiti na kuandika na mimi kuandikwa na wengine.
 
Hebu tuwekee na uwiano wa dini zote mbili katika safu ya viongozi mbambali wa Sirikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) halafu uonyeshe asilimia(%) kwenye mabano mkuu. Maana tunaambiwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
 
Tupunguze jazba na mzaha. Tujadili hoja kwa kufuata uhalisia wa mambo.
 
Azarel,
Ningetaka kujigamba nisingeweka hayo ambayo hakika ni yangu kweli.

Ningeweka vitu hapa hujapata kuviona kutoka kwangu.

Ndiyo hiyo "so what," najua vitu hivi kwa utafiti na kuandika na mimi kuandikwa na wengine.
Mohammed Said tunakujua na kazi zako tunazifahamu pia
 
Hakuna mahali popote au kifungu chochote kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo panamlazimisha Rais kuzingatia dini ya mtu yoyote wakati wa kufanya teuzi mbalimbali.

Hivyo Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania anateua kulingana nasifa au vigezo vinahitajika kulingana na nafasi au mazingira ya wakati huo.

Anaweza kutea mtu yeyote asiye hata na dini au mwenye dini yoyte maana dini hakijawahi kuwa kigezo cha mtu kuteuliwa. Kama ni masuala ya udini kafanyieni miskitini au makanisani srikali haina dini. VINGINEVYO BADILINI KATIBA IWEKE HAYO MATAMANIO YENU LA SIVYO MTAPIGA KELELE BURE.
 
Mimi naijua ya Mtume Muddy yule jamaa wa Mecca
Azarel,
Hiki ufanyacho si kitendo cha uungwana.
Sisi Waislam Allah anatuasa katumbia kuwa tusiwatukanie wasiokuwa Waislam miungu yao wasije wao wakamtukana Mungu wa kweli.

Mara myingi nimekuona ukifanya mjadala na mimi utamdhihaki Mtume Muhammad nami hukukanya nikikueleza kuwa haifai.

Nafikiria kuku-block.
 
Teuzi na upandishwaji vyeo lazima vifanyike kwa kuangalia sifa na vigezo vya mtu husika.
Lazima viwe 'based on merits' siyo sifa ya udini au ukabila.
Bila shaka yoyote, hivyo ndivyo vigezo halisi kabisa.
Vigezo hivyo pia vinaanzia chini kabisa, kuhakikisha kwamba mTanzania yeyote anapewa fursa sawa ya kuinua maisha yake bila upendeleo unaohusiana na ukabila, udini au uchochote, hii inaanzia katika huduma za elimu katika maeneo yote nchini.
 

Nikwambie kitu kimoja ambacho unatakiwa kukifahamu - (Tena umegusa kwenye shina; Elimu) suala la kuiandaa jamii ya kesho ni ya serikali. Hii ikiwa pamoja na elimu ambayo ndio dira ya kupata ajira. Ni ujinga baada ya miaka 60 ya uhuru tukaendelea kulia na makosa aliyoyafanya mkoloni, huku ni kukosa akili. Sasa tulidai uhuru ili iweje? Au unafikiri ili tuendeleze utaratibu ule ule wa mkoloni, tukibadili rangi tu ya mtawala.

Tena umetaja Mmakabila kama wachaga - Huwezi amini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unashule nyingi za sekondari kuliko Dar es salaam ambapo uwiano wa wakazi wa mikoa hiyo hata haikaribiani. Tena shule nyingi zaidi zimejengwa baada ya uhuru na mkoloni mweusi. Usishangae kwani hii ndio sera ya serikali ikiwalipa walimu na kuendesha shule hizo kwa kodi za wananchi wote.

Kifupi utaratibu wa maandalizi ya mwananchi yamefanywa kimakusudi kabisa huku wakijua kuwa wao watashikilia tu kuwa hawa hawana elimu.

Kwa ufahamu zaidi soma kitabu cha muandishi Sykes, ndio utaona mpango halisi. Ni lazima mwenendo huu ubadilike toka kwenye elimu, hakuna vipofu sasa hivi. Mambo yote yapo hadharani, humfichi mtu kitu.

J. K. Nyerere amewekwa kama candidate na kanisa katoliki ya kupewa U- Saint, si kwa bahati mbaya. Ni kwa vile katekeleza mpango mahsusi wa kuhakikisha kuwa kuna kikundi fulani kinapata upendeleo. Tunachosema ni kuwa yaliyopita ni ndwele tugange ya sas na yajayo.
 
Jibu ni Rahisi,Ni kwa sababu ya watu wenye fikra kama hizi za kusema wanaonewa bila kuchukua hatua kubadili hali halisi.Somesheni watoto wenu,Jitangazeni watu wawajueni kwamba mnaweza,Onyesheni umahiri wenu katika kufanya mambo.Badala ya kutumia muda mwingi kutaka kubebwa wakati hata mkibebwa hambebeki wekezeni katika ilimu ya watoto wenu.

Acheni kuwaaminisha kwamba hawana haki katika nchi yao na badala yake wajengeeni uwezo wa kitaaluma,kimaadaili na kimtazamo.Mkiweza kufanya hilo mtaitendeahaki dini yenu na taifa letu kwa ujumla. Ili kutumia mwamvuli wa dini wa kuficha uzandiki,uzembe na uovu ni jambo ambalo haliwezi kubebwa na mtu yoyote timamu.

Takwimu hazioneshi ubaguzi dhidi ya Waislamu zinaonesha kiwango cha uzembe wa Waislamu katika kutatafuta na kutumia fursa katika ujenzi wa taifa.Tusifiche uzembe wetu kwa kisingizio cha ubaguzi.Tuhimizane tuweke bidii katika kila jambo ili tuweze kupiga hatua kubwa a maendeleo kama taifa.Tusilete fitina na ramli chonganishi bali tuoneshe weledi wetu na Mwenyezi Mungu atatubariki.
 
Hata kama shule ni moja tu.Inatosha kuleta mabadiliko kama ikitumika vizuri.Jaribu kufuatilia kwa karibu.Utaona kabisa kuna desturi kwa waislamu wengi kutohimiza ilimu kwa watoto wao,hasa wa kipato cha chini.Ukifuatilia zaidi utaona kuwa waislam wengi hutoa hadi majengo ya nyumba zao kuwa madrasa ya kufundisha elimu ya dini lakini hata kuwafundisha watoto elimu ya kawaida hakuna.Watoto wanafundishwa Juzuu lakini hata kujiongeza na kuwafundisha kidogo hesabu na mamao mengine ya muhimu katika dunia mnaona tatizo.

Jiongezeni.Msitake kubebwa.Kama shule zinajengwa lakini hamleti watoto wenu wasome basi bora zikajengwe kwa wale ambao wana mwamko wa kupeleka watoto shule.Fuatili takwimu za ndoa za utotoni,na takwimu za uduni wa elimu kwa kuliunganisha jamii za kiislamu na jamii zisizo za kiislamu utaona tofauti.Tuambieni ukweli hata kama unauma.Lazima kabla ya kutaka kubebwa muoneshe uelekeo.Jijengeeni heshima kama wanajamii wapenda maendeleo na sio watu duni wasipopenda maendeleo na maendeleo yatawafuata.
 

Nilifikiri utajibu kwanini shule za sekondari Kilimanjaro ni nyingi kuliko Dar es salaam. Kwa vile umeshindwa kujibu hilo, nachukulia kuwa - meseji sent.

Pili. Elimu hii tunayoisoma leo darasani tumeletewa na wakoloni, hata hao unaosema wanapenda kwenda shule leo hawakupenda wakati huo inaletwa. Soma kitabu cha Ngugi wa Thiongo " The river between". Ninachotaka kusema ni kwamba hata hao unaosema hawapendi kwenda shule, ni jukumu la serikali kuwawekea utaratibu na mikakati ya kuijenga jamii hiyo kwa ajili ya kesho yao.

Wakoloni walifanya hivyo kwa wachaga, wanyakyusa, wahaya nk. ni zamu ya serikali kuwa na utaratibu wa kuwainua huko ambako mkoloni hakufika au hakukuwekea utaratibu. Kama serikali iliendelea kule kule ambako mkoloni alikutengeneza, basi huo ni udhaifu mkubwa wa serikali iliyoongoza kwa miaka 60. Na ndio maana ni vigumu kujivunia uhuru wetu. Na ndio maana matabaka bado yanaendelea. Na ndio maana wahanga wataendelea kulalamika.
 
UDOM mkaamua mtoe waislam muweke wakristo! Hongereni nchi yenu hii wengine tupo kwa bahati mbaya
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…