Hapana,ni tafsiri yako,Tafsiri yangu ni rahisi tu kwamba hakuna teuzi zinazopatikana kwa kuonewa huruma wala kupendelewa bali ni jitihada za mtu kujionesha uwezo wake,kusimamia anachokiamini na kutafuta fursa.Hii keki ya taifa kila mtu anataka kuila na kama Waislamu katika msingi wa kidini mnaona kwamba mnamegewa kipande kidogo ni jukumu lenu kujitazama ni wapi mnakwama kabla ya kuanza kutafuta wa kumsingizia.
Mimi binafsi nimeanya kazi na Waislamu pamoja na Wakristu.Nimeishi na Waislamu pamoja na Wakristu,Nimesoma na Waislamu pamoja na Wakristu.Na kote huko sijaona popote ambapo kigezo cha uislamu wa mtu kinamkosesha mtu fursa.Nimeona watu wakikosa fursa kwa sababu hawana connection,hawana uwezo wa kujiuza,Hawana wa kutetea wanachokiamni,
Hili sio tatizo la Waislamu ni Tatizo la Watanzania wengi.Ndio maana hata ukitazama wanaokula mema ya nchi ni zile jamii ambazo ziliamka mapema na kutafuta kujikomboa bila kusubiri huruma za watawala.
Kama tutaendekeza fikra za namna hii za kuaminisha umma kwamba watu wanafanyiwa figizu kwa sababu ya uislamu wao bila kuweka Facts za pande zote mezani basi itakuwa ni tatizo.
Tusijifanye hatuoni tatizo la Radical Islamism katika jamii,Elimu ya dini imepewa kipaumbele ila sio kwa ajili ya kujenga misingi ya utu na ubinadamu bali zaidi ni katika kuwa brain wash watu.
Wapo vijana wa Kiislam ambao wanafanya vizuri na ambao wamepewa nafasi,wengine mjifunzo humo mjue walifikiaje hatua hio.Hakuna sababu ya kufikiri kwamba mabadiliko yatakuja kwa neema.
Ni dhahiri shahir kwamba hata mkipewa mamlaka na nafasi mtaanza kupendeleana kama kilichotokea UDOM mpaka wakahamishwa hao wote ni kwa sababu ya kuanza kuonesha ubaguzi wa wazi wazi.Penye ukweli tuambiane ukweli.Sisi ni Watanzania kwanza kisha Waislam baadae.Hizi imani zilikuja na Jahazi,wenye nazo wamekaa wanajenga nchi zao sisi tunalumbana kutaka vyeo kwa msingi wa udini?Mmesikia utumishi wa umma ni sawa na Uimamu au kuwa Mwalimu wa dini?Kama mnao uwezo jitokezeni,Gombeeni,Toni sera zenye mashiko zisizokuwa na udini bali maendelea mpewe nchi then mkifanya vyema tutawachagua tena na tena na tena.