Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Kama story ya kijiweni vile. Haingii akilini.
Kwa hiyo baada ya hapo waislamu wakasusa kupeleka watoto wao shule za serikali? Au Nyerere aliwakataza pia?

Inaelekea mwenzetu bado mchanga sana wa historia ya Tanzania kwa waislam na elimu, BAKWATA na EAMWS. Sijui kama hata unaelewa kirefu cha EAMWS.

Ila ninachokushari usiwe mvivu wa kusoma vitabu, kakisome kwanza kitabu cha Abdul Sykes (1998). Hiki kitabu kitakupa picha nzuri sana na kuelewa kwanini Nyerere alifanyiwa mpango wa kuwa Saint na kanisa katoliki.
 

Walioleta mifarakano ni hao watawala waliopanga mipango mibovu ya ugawanyaji wa madaraka. Kama wao walikuwa wanalifikiria hilo wangekuwa tayari kutafuta suluhu.

Wewe na hao watawala mpo chungu kimoja. Msipoyaona haya mtaiingiza nchi matatani.
 
Walioleta mifarakano ni hao watawala waliopanga mipango mibovu ya ugawanyaji wa madaraka. Kama wao walikuwa wanalifikiria hilo wangekuwa tayari kutafuta suluhu.

Wewe na hao watawala mpo chungu kimoja. Msipoyaona haya mtaiingiza nchi matatani.
Hebu nieleze ni watawala gani unaowazungumzia hapa, maanake sikuelewi.

Katika haya uliyoandika hapa, nakuona wewe huna ufahamu wowote mbali ya kuimba tu unayolishwa.
 
Mzee wangu Mohamed Said,Nakubaliana na wewe kwamba mimi sio msomi wa Historia ya Waislam na huwa naheshimu sana jitihada zako za kutaka kuweka sawa historia ya nchi yetu mintarafu nafasi ya "Uislam" Sitaki kusema kwamba kuna ukweli au hamna ukweli katika maelezo yako na ya wengine ila nataka mimi na wewe tukubaliane kwamba Islamic radicalization ni tatizo hata ndani ya uislamu wenyewe.

Na hili ndilo tatizo kubwa linalokabili jamii nyingi duniani za kiislam yaani Religious extremism.

Pili mimi na wewetukubaliane kwamba wasomi wengi wa kiislamu hawautendei haki uislamu hasa katika eneo la kuhamasisha dhidi radical sentiments ndani ya uislam.Adui mkubwa wa uislamu na waislamu wenyewe kwa kushindwa kutenganisha harakati za kidini,harakati za kisiasa na harakati za kimaisha.Lazima tukubali kwamba zama zimebadilika na utamaduni wetu lazima ubadilika.

Hebu tutafakari kwa pamoja ni kwa nini nyerere alikosana na wale waislam waliompokea Dar es Salama?Je aliuchukia uislamu au kulianza kuibuka kwa radical sentiments na Nyerere hakuwa Tayari kuruhusu hilo litokee kwamaslahi makubwa ya taifa?Najua unaweza usikubali lakini maandiko yako yanaonesha kabisa kwamba hicho ndio chanzo."Nyerere alihofia radical sentiments ndani ya uislamu na akachukua hatua kudhibiti"Binafsi nafikiri ulikuwa uamuzi sahihi kwa kuzingatia mazingira.

Mzee wangu wewe umebahatika kupata ilimu kidogo ya kutosha,nafikiri kwa kiwango chako cha elimu tunaweza kusema ulikutana na mengi katika safari yako ili sidhani katika yote uliwahi kunyimwa elimu kwa sababu ya dini yako.Naamini kabisa ungebaguliwa wakati ukitauta elimu yako usingekuwa hapa ulipo.Nina hakika uliweka jitihada ndio maana uko hapa leo.Na hata maanikio yako uliyo nayo katika taaluma yako ni matokeo ya jitihada zako na bahati kidogo.

Jaribu kufikiri wakristu uliosoma nao tangu msingi na waislamu uliosoma nao halafu uangalie kwa kina kabisa kama kuna sehemu wakristo walibebwa zaidi ya waislamu(Achilia mbali zile personal connection ambazo ni kawaida katika maisha)Nazungumzia nyakati ambazo yupo muislam na mkristu wenye vigezo vyote sawa na mwislamu akaachwa mkristu akachukuliwa.Kama hayo matukio yapo ni machache sana kuweza kuwa kielelezo cha ubaguzi.

Ambianeni ukweli kwamba lazima muweke jitihada ya kupatia wanenu hamasa pamoja na elimu ya kutosha.Haitoshi tu kuwa mazamifu katika elimu akhera,elimu dunia pia ina nafasi yake.

Religious extremism ni tatizo sio tu kwa waislam bali kwa dini zote.Yote kwa yote Tanzania hatuna kiwango cha ubaguzi wa dini kama mnavyotaka kutuaminisha ingawa kuna weza kuwa na changamoto hapa na pale lakini haziwezi kufika kiwango cha kuitwa ubaguzi wa kidini tena "Systemic"
 
Ondoza,
Wanaotakiwa kujibu haya ni serikali si wewe kwani uhusiki.

Mimi si mtu wa kubishana huingia pale ninapoona kuna watu hawaujui ukweli.

Shura ya Maimamu imetoa waraka tuwe na subira.
 
mbona kwenye quran haijaandikwa kwamba waislam ndo walipigania uhuru wa tz?? quran yenyewe inakukana, hizi dini ni chanzo cha watu wengi kwenda motoni
 
Duh!!Hatari sana hii!!
 
Ondoza,
Wanaotakiwa kujibu haya ni serikali si wewe kwani uhusiki.

Mimi si mtu wa kubishana huingia pale ninapoona kuna watu hawaujui ukweli.

Shura ya Maimamu imetoa waraka tuwe na subira.
Hapana, sio kubishana,Waraka umeshawekwa mbele ya umma,nimependa maudhui yote ya waraka huu isipokuwa msingi wake tu wa kwamba hao walotendewa au yanayotendwa ni ya kuwalenga waislamu kwa sababu ya uislamu wao.Hapana sidhani ni sahihi kuliweka swala hili kwa namna hio.

Kama utaratibu ulikiukwa basi tudai haki kwa msingi wa haki bila kujificha nyuma ya mwamvuli wa dini kukataa kukubali kwamba hata sisi tuna makosa fulani au mapungufu.

Hakuna mja asiye na mapungufu.Serikali itajibu kwa namna yake ya kawaida ila halitamaliza mjadala kuhusu tabia hii isiyo njema ya kujificha nyuma ya mwamvuli wa udini pale tunapokiuka taratibu za nchi katika utendaji au tunaposhindwa kutimiza wajibu wetu wa kiraia
 
Soma kwanza kwa furaha wacha jaziba
Gavana eee shaykh Kundecha kawaumbua na UONGO WENU...
Waongo Kama TUMBA MBICHI....

Haya Sasa Mambo ngw'enyuu halitaki HATA tochi....

WARAKA ule feki......
WARAKA ule Koko....
WARAKA ule haujapitia kwa masheikh wenu aaaagh "innal baatwila kana Zahuka"

Kul ul Haq Lau Kanna mura,rudini kumheshimu na kumtii kiongozi wetu wa kiroho na kiimani Tanzania kwa BARAZA letu mtambuka BAKWATA, Ashaykh ul Muadhama Mufti Zubeir Bin Ally.

Ametusisitizia Mara elfu KIDOGO;


1.TUJITAMBUE
2.TUBADILIKE
3.TUACHE MAZOEA
 
Walitolewa waislam 11 na msikiti kuvunjwa, hivi umelisoma bandiko tunalolijadili kweli?
Nimelisoma vizuri sana, kuandikwa na kithibitisha ni vitu viwili tofauti, Mtu anaweza kuandika chochote

Hebu nitajie hao Wakristo waliohusika kuvunja msikiti.
 
Content moja maridadi kwelikweli..
 
Wewe .hivyo vitabu tulishavosoma tangu 2010 kariakoo. Kumbe vitabu vya MS ndio unavyovijua tu vinavyoongelea Uhuru wa Tanganyika? Poor you

East African Muslim Welfare Society ya kuanzia 1945 kiuhalisia haikuuliwa na Nyerere na wala Vatican haikuweka mkono, tatizo ilikuwa Management. Mbona hata baada ya kucolapse 1968 kule Uganda ikasurvive?

Mbona Uislam ukaspread zaidi Rwanda?

Mbona ni Mombasa tu na Bongo ndio tatizo likaendelea? Nyerere alikuwa na influence gani Mombasa?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…