Nikusaidie tu mkuu, hapo kwenye namba weka vidoti au alama tofauti na namba ama alfabeti kwakuwa, nimeshindwa kuelewa huo mtitiriko.
Pili, kana hawana kazi na wameweza kwenda ulaya kutafuta kazi, ni wazo zuri na inaonesha wana shughuli nje ya uimbaji/wanalipwa kwakuimba ndio maana wakapata nauli ya kwenda ulaya ba vibali (hata kama si vyote) UKUMBUKE ULAYA SIO SAWA NA MWENGE-UBUNGO kwamba utatembea kwa miguu.
Tatu, usipende saana kuwahukumu wenzio kwakudhani wewe dhambi ya kudhania/kuhukumu ni ndogo kuliko hao unaowaita wazinzi (kama wewe sio muimbaji hapo, nashindwa kuamini kama kweli wanakwaya wawe wanapigana kila siku kugombea bwana na bado wakaendelea kuwa wamoja. Mkuu mimi nimefundisha kwaya sana, ikitokea tu ukaanzisha mahusiano na wanakwaya wako, kwaya inakufa haraka sana ama nidhamu haitokuwepo kabisa.
Nne, kama kwaya haitambuliki, najiuliza huko wanakoimba nani anawapa nafasi (maana lazima wanaonekana kanisani na watu wanavutiwa nao kisha kuwaalika