Wasabato mnadai Kanisa Katoliki ni alama ya mpinga kristo lakini bado mnaamini Biblia waliyoindaa Karne 16 zilizopita?!

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Nimekuja na mada kama ifuatavyo

Mabaraza ya Makadinali wa Kanisa Katoliki kwenye Mtaguso wa Roma (382) na Trento (1546)
walisimamia mchakato wa kuchambua, kupangilia pamoja na kuidhinisha vitabu 73 - 46 katika Agano la Kale na 27 katika Agano Jipya - ambayo ilijumuisha. kanuni ya Biblia ya Kikristo.

Kimsingi kazi ya kuamua Vitabu gani viwemo kwenye Biblia ilifanywa na Kanisa Katoliki pekee.

Mchakato huo ulifanyika miaka zaidi ya 1,600 kabla ya dhehebu la Wasabato Duniani halijaanzishwa

HOJA YANGU kwanini Wasabato wanaiamini na kuitumia Biblia iliyoandikwa na Kanisa Katoliki huku wakifundisha kuwa Kanisa hilo kuwa la mpinga Kristo?

Yaani Papa ni alama ya mnyama aliyenenwa kwenye kitabu cha Ufunuo lakini Kanisa analoongoza likaandaa Biblia iliyo sahihi? Je upi ni uhalali wa Biblia husika huku Kanisa husika likikosa uhalali?

Naombeni enyi wenye elimu ya theolojia na wenye hekima mtupe majibu.
 
Sasa hivi wasabato wameongezewa jingine la kuwararuria wacatholic

Ushoga

Miaka kadhaa mbele watakaokuwepo watanukuu kauli ya pope Francis kama ambavyo Huwa wanawanukuu maaskofu wa catholic kuhusu siku ya ibada. Bahati MBAYA, kipindi hicho mapenzi ya jinsia Moja yatakuwa sawa na inavyochukuliwa sabato kwa sasa. Watu wataambiwa kauli kama "Uoane na jinsia yako au ya tofauti Haina madhara" na mafungu ya kusapoti yatakuwa lukuki mfano like Yesu alilosema "kuna matowashi waliozaliwa hivyo".
 
Biblia Ina vitabu 66 Sio 73
Hao wa 66 ndo wa mwisho kabisa kugusa biblia wakatoliki vinaanzia 70, orthodox ya Ethiopia wanavyo kwenye 80
Screenshot_20240604-153603_Samsung Internet.jpg
 
Hao wa 66 ndo wa mwisho kabisa kugusa biblia wakatoliki vinaanzia 70, orthodox ya Ethiopia wanavyo kwenye 80View attachment 3008300
Agano la kale ni.la wayahudi Jewish Bible Ina Ina vitabu 39 agano jipya Lina vitabu 27 jumla 66

Kanisa Katoliki na Orthodox waliongeza vitabu vyao Kwa kuokoteza majalalani ambavyo kwenye Jewish Bible havimo

Jewish Bible ndio Biblia ya kale kabla hata Yesu kuzaliwa au kanisa Katoliki kuwepo

Makanisa mengine yote Wanaamini Jewish Bible yote kama ilivyo na vitabu vyake 39 ambavyo hivyo Sio kazi ya kanisa Katoliki uongo.Kanisa Katoliki hivyo vitabu walivikuta walichofanya ni kuongezea vyao ambavyo makanisa mengine hayajakubali waliwemo wasabato.
 
Kwakweli kila mtu anywe mataputapu yake
Screenshot_20240604-164101_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20240604-164045_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20240604-164301_Samsung Internet.jpg
 
Agano la kale ni.la wayahudi Jewish Bible Ina Ina vitabu 39 agano jipya Lina vitabu 27 jumla 66

Kanisa Katoliki na Orthodox waliongeza vitabu vyao Kwa kuokoteza majalalani ambavyo kwenye Jewish Bible havimo

Jewish Bible ndio Biblia ya kale kabla hata Yesu kuzaliwa au kanisa Katoliki kuwepo

Makanisa mengine yote Wanaamini Jewish Bible yote kama ilivyo na vitabu vyake 39 ambavyo hivyo Sio kazi ya kanisa Katoliki uongo.Kanisa Katoliki hivyo vitabu walivikuta walichofanya ni kuongezea vyao ambavyo makanisa mengine hayajakubali waliwemo wasabato.
Na pia hata hao wayahudi maandiko mengi pia wamebeba kwa wengine hasa babylon walipokua utumwani,,,misri pia.....
 
Agano la kale ni.la wayahudi Jewish Bible Ina Ina vitabu 39 agano jipya Lina vitabu 27 jumla 66

Kanisa Katoliki na Orthodox waliongeza vitabu vyao Kwa kuokoteza majalalani ambavyo kwenye Jewish Bible havimo

Jewish Bible ndio Biblia ya kale kabla hata Yesu kuzaliwa au kanisa Katoliki kuwepo

Makanisa mengine yote Wanaamini Jewish Bible yote kama ilivyo na vitabu vyake 39 ambavyo hivyo Sio kazi ya kanisa Katoliki uongo.Kanisa Katoliki hivyo vitabu walivikuta walichofanya ni kuongezea vyao ambavyo makanisa mengine hayajakubali waliwemo wasabato.
Hivyo Vitabu 39 unavyodai vya Wayahudi ni vya agano jipya au agano la kale?
 
Agano la kale ni.la wayahudi Jewish Bible Ina Ina vitabu 39 agano jipya Lina vitabu 27 jumla 66

Kanisa Katoliki na Orthodox waliongeza vitabu vyao Kwa kuokoteza majalalani ambavyo kwenye Jewish Bible havimo

Jewish Bible ndio Biblia ya kale kabla hata Yesu kuzaliwa au kanisa Katoliki kuwepo

Makanisa mengine yote Wanaamini Jewish Bible yote kama ilivyo na vitabu vyake 39 ambavyo hivyo Sio kazi ya kanisa Katoliki uongo.Kanisa Katoliki hivyo vitabu walivikuta walichofanya ni kuongezea vyao ambavyo makanisa mengine hayajakubali waliwemo wasabato.
Tube bible ya Jewish ambayo ina agano jipya
 
Ukristo na Uislam ni projects za Ukatoliki...hutaki jinyonge.

Ndio maana hata mtukane vip wanakaa kimya huku wakinywa mvinyo na kucheka hihihihiiiiii
 
Tupe bible ya Jewish ambayo ina agano jipya
Jewish Bible Haina agano jipya

Agano jipya makanisa yote yanakubaliana ni vitabu 27

Tofauti ya Biblia ya kanisa Katoliki na mengine Iko kwenye agano la kale

Kanisa Katoliki lilichukua Jewish Bible kama ilivyo wakaongeza vitabu vya vingine ambavyo walikoviokota wanajua wenyewe

Agano jipya wakristo wote vitabu vinafanana wakiwemo wakatoliki
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kimsingi bible ipo kabla ya wakatoliki kuwepo.

Orthodox ni imani ya Kikristo kongwe kuliko Ukristo uliosimamiwa na Warumi.

Kilichofanywa na wakatoliki ni kuchukua maandiko ambayo yalikuwepo na kuyaunganisha tu kama ambavyo hata hao wengine kama Hebrews, Ethiopian Orthodox, Protestants na wengineo walikusanya maandiko ya kale wakaunda bible (katiba) yao.

Hivyo hoja kuu kwenye bible zote ambayo ni ya msingi, bible hizo kwa ujumla wake zinaangazia kuacha dhambi, makosa na maovu na kutenda mema huku tukimuabudu Elohim, kitu ambacho ni sahihi kwa ajili yetu.
 
Ukristo na Uislam ni projects za Ukatoliki...hutaki jinyonge.

Ndio maana hata mtukane vip wanakaa kimya huku wakinywa mvinyo na kucheka hihihihiiiiii
Ukristo upo kabla ya ukatoliki.

Orthodox Christians ni imani kongwe ambayo imeshika hatamu mpaka kesho maeneo ya Ethiopia, Russia, Ukraine na kwingineko.

Pia kumbuka wana bible yao ambayo ni kongwe kuliko bible ya Warumi.

Bible yao ina vitabu zaidi ya 80 wakati hizi nyingine zina vitabu 73, 66 na 24 kutegemea na imani iliyochambua na kuunganisha maandiko hayo.

Hivyo si sahihi kusema Ukristo umeasisiwa na Warumi.
 
Agano la kale ni.la wayahudi Jewish Bible Ina Ina vitabu 39 agano jipya Lina vitabu 27 jumla 66

Kanisa Katoliki na Orthodox waliongeza vitabu vyao Kwa kuokoteza majalalani ambavyo kwenye Jewish Bible havimo

Jewish Bible ndio Biblia ya kale kabla hata Yesu kuzaliwa au kanisa Katoliki kuwepo

Makanisa mengine yote Wanaamini Jewish Bible yote kama ilivyo na vitabu vyake 39 ambavyo hivyo Sio kazi ya kanisa Katoliki uongo.Kanisa Katoliki hivyo vitabu walivikuta walichofanya ni kuongezea vyao ambavyo makanisa mengine hayajakubali waliwemo wasa
Jewish Bible Haina agano jipya

Agano jipya makanisa yote yanakubaliana ni vitabu 27

Tofauti ya Biblia ya kanisa Katoliki na mengine Iko kwenye agano la kale

Kanisa Katoliki lilichukua Jewish Bible kama ilivyo wakaongeza vitabu vya vingine ambavyo walikoviokota wanajua wenyewe

Agano jipya wakristo wote vinafanana wakiwemo wakatoliki
Sasa huo uhalali wa hivyo Vitabu vya agano jipya vinapataje uhalali wakati Kanisa husika hazikubaliki? Hebu jibu hiyo hoja kwanza
 
Ukristo upo kabla ya ukatoliki.

Orthodox Christians ni imani kongwe ambayo imeshika hatamu mpaka kesho maeneo ya Ethiopia, Russia, Ukraine na kwingineko.

Pia kumbuka wana bible yao ambayo ni kongwe kuliko bible ya Warumi.

Bible yao ina vitabu zaidi ya 80 wakati hizi nyingine zina vitabu 73, 66 na 24 kutegemea na imani iliyochambua na kuunganisha maandiko hayo.

Hivyo si sahihi kusema Ukristo umeasisiwa na Warumi.
Asante kwa kuniongezea elimu mkuu.
My bad_i draw my comment back.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom