Unasema wakatoliki walichukua maandiko na kuyaunganisha? Je waliyachukua kutoka wapi? Kwa vigezo vipi? Unaweza nitajia Idadi ya hayo maandiko ambayo kimsingi ndiyo Vitabu?
Kwa ufupi;
Imani kongwe hapo mashariki ya kati ni "Uyahudi".
Hivyo basi baadhi ya vitabu walichukua toka kwenye "Uyahudi" hususani vitabu vya agano la kale.
Maandiko mengine walichukua kutoka kwenye kumbukumbuka za kale za kiyahudi ambazo ziliandikwa miaka kadhaa huko nyuma.
Mfano Yesu aliletewa gombo (chuo cha Nabii Isaya) ili alisome, hicho ni kitabu kipo miaka mingi kabla ya Ukristo. Pia hata alipojaribiwa na Shetani alisema imeandikwa (akimaanisha vitabu vilivyokuwa vinatumika kwa ajili ya mafundisho ya imani ).
Chanzo kikuu cha biblia za imani zote ni marejeo ya maandiko ya kale yaliyoandikwa kwenye mbao, mawe au gombo pamoja na maandiko yaliyoandikwa baada ya Yesu.
Hivyo basi kila imani ilichukua huko maandiko yake kulingana walivyoona inawafaa, wengine walichukua vitabu 83, wengine 72, wengine 66, wengine 24 n.k.
Wayahudi wao wanatumia TALMUD ambayo ina mkusanyiko wa vitabu vya agano la kale.
Mpaka sasa kuna mkusanyiko wa marejeo mengi ya kale yaliyoandikwa kwenye mbao, mawe au gombo yanayozungumzia habari za kale juu ya Imani ya Mungu hususani Uyahudi ambao ndio mama wa Imani zote za mashariki ya kati ambayo hajaingizwa kwenye hizi imani zilizopo.
Hivyo basi, Ethiopian Orthodox wao walichukua maandiko toka kwenye vitabu vya kale vilivyokuwepo kabla ya Yesu na Warumi, kisha wakachukua vingine vilivyoandikwa baada ya Yesu (Injili, nyaraka na ufunuo) wakaunganisha wakaja na biblia yao yenye vitabu 83.
Kwenye Orthodox bible wanatumia jina halisi la Muumba wa vyote ambalo anaitwa ELOHIM badala ya MUNGU.
Kumbuka Mungu ni cheo sio jina, hivyo kwa mfano utakuta wanasema " Hapo mwanzo Elohim aliumba mbingu na nchi .....", na siyo Mungu aliumba mbingu na nchi.
Kwa uchache umepata chanzo kikuu cha maandiko yote yanayotumiwa kama marejeo ktk hizi imani tukianza na Uyadi kisha ikafuata Orthodox, ikaja Romans, ikaja Protestant ndo wakaja Wasabato.