Wasabato mnadai wanaoabudu jumapili wamepotea, siku hiyo ni Alama ya Mnyama, Je wanaoabudu ijumaa badala ya jumamosi nao wamepotea?

Wasabato mnadai wanaoabudu jumapili wamepotea, siku hiyo ni Alama ya Mnyama, Je wanaoabudu ijumaa badala ya jumamosi nao wamepotea?

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Niende kwenye hoja

Huwezi ona msabato akimsema muislamu kuwa ati anafanya dhambi kuabudu siku ya ijumaa ila ni kawaida kumsikia akimuhesabia dhambi Mkatoliki kwa kuabudu jumapili badala ya jumamosi

Kwa msabato siku ya jumapili ambayo ndiyo aliyofufuka Bwana yetu Yesu Kristo ni Alama ya Mnyama!

Swali langu kwa Wasabato siku ya Ijumaa ni Alama ya nini hasa kimaandiko?

Kwanini kuabudu jumapili ndiyo dhambi lakini ijumaa sijawahi sikia au kusoma sehemu yeyote kuwa ni dhambi?

Why? Why?

Nasubiri elimu kutoka kwa wajuzi
 
Dini ni kifungo katika ubongo wa mwafrika, kupata elimu ni bora zaidi lakini sio kuikumbatia kiasi hicho.

amini kuwa wanadamu ataonja umauti hivyo kuwa mwislam au msabato au mkatoliki hakuna aliye bora kila mtu atabeba mzigo wake mwisho wa siku.

usiamini katika dini kwa maana ni upofu machoni pa waafrika. Washa Nuru katika ubongo wako.
 
Wasabato NJOONI upesi mtuambie hapa Ted wilson alikuwa anafanya Nini Kwa papa?

Maana mnatuhubiri yakuwa hatupaswi kumpigia mtu magoti yaani kumsujudia je rais wenu hapa anafanya Nini?

Kwanini mkiwa na mikutano papa mnamsimanga sana kumbe nanyi kisiri Siri mnaenda kwakwe kutibu madhambi yenu?
 
Attachments

  • FB_IMG_1718688996177.jpg
    FB_IMG_1718688996177.jpg
    36.3 KB · Views: 5
Jibu lako, msabato anaamini katika agano la kale zaidi na ame base katika torati ya nabii mussa, kwahiyo mfumo ambao umebadilishwa na nabii Al Masih issa ibn Maryam ambao madhehebu mengine wanatumia kama Lutheran, angelican, roman catholic, morovian, pentecostal, na kadhalika...

1. Kusali jumapili, jumapili ni siku ya kwanza katika juma kulingana na kalenda ya ulimwengu.

2. Wasabato hasa wanawake hawatoboi sikio, pua, mikufu, shanga za kiuno, au vikuku, Wala nywele zao hawaweki dawa Wala kusuka Rasta hii ilikuwa agano la kale lakini agano jipya ameruhusiwa mwanamke kujipamba hasa mbele ya mumewe.

3. Wasabato wengi wanapatikana kaskazini wapare waarusha na kadhalika hii pia inategemeana na ukabila hasa tabia ya uchoyo

ANGALIZO.
usiamini katika dini kwa sababu ni utumwa hasa katika ubongo wa mwafrika.
 
Wasabato NJOONI upesi mtuambie hapa Ted wilson alikuwa anafanya Nini Kwa papa?

Maana mnatuhubiri yakuwa hatupaswi kumpigia mtu magoti yaani kumsujudia je rais wenu hapa anafanya Nini?

Kwanini mkiwa na mikutano papa mnamsimanga sana kumbe nanyi kisiri Siri mnaenda kwakwe kutibu madhambi yenu?
Siku nyingine kabla hujashare pic unatumia google picture search.
Huyu sio Ted Wilson Huyu ni Jesuit James Martin, Muariri wa gazeti kubwa la majesuit huko NW na mwanaharakati wa yale mambo ya upinde.
Screenshot_20240627-204649_Samsung Internet.jpg
 
Yani mkisemwa nyie hadi mgeukie waislamu, acheni shobo
 
1. Kristo alifufuka Jumapili; kwamba, "Kristo asingalifufuka imani yetu ingalikuwa bure; ila Kristo amefufuka limbuko lao waliolala". Itoshe kusema, ukombozi wa mwanadamu ulithibitika Jumapili.

2. Nitawapelekea msaidizi mwingine ndiye yule Roho wa Kweli; siku ile kuu ambayo Robo wa Mungu aliwashukia wanafunzi wake; siku ile ya 50 yaani Pentekoste ilikuwa Jumapili. Kila mmoja akampokea Roho Mtakatifu kanisa la kwanza likazaliwa siku ile.

Tuendelee kuabudu siku, miandamo ya miezi, na kuzitazama nyota badala ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli.
 
  • Thanks
Reactions: K11
2. Wasabato hasa wanawake hawatoboi sikio, pua, mikufu, shanga za kiuno, au vikuku, Wala nywele zao hawaweki dawa Wala kusuka Rasta hii ilikuwa agano la kale lakini agano jipya ameruhusiwa mwanamke kujipamba hasa mbele ya mumewe.
Hawapendi kachumbari 🤣🤣🤣
 
Sabato ya kweli ni Kila siku ,mtu anatakiwa akae ndani ya uwepo wa Mungu.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Niende kwenye hoja

Huwezi ona msabato akimsema muislamu kuwa ati anafanya dhambi kuabudu siku ya ijumaa ila ni kawaida kumsikia akimuhesabia dhambi Mkatoliki kwa kuabudu jumapili badala ya jumamosi

Kwa msabato siku ya jumapili ambayo ndiyo aliyofufuka Bwana yetu Yesu Kristo ni Alama ya Mnyama!

Swali langu kwa Wasabato siku ya Ijumaa ni Alama ya nini hasa kimaandiko?

Kwanini kuabudu jumapili ndiyo dhambi lakini ijumaa sijawahi sikia au kusoma sehemu yeyote kuwa ni dhambi?

Why? Why?

Nasubiri elimu kutoka kwa wajuzi
Wakristo ambao Si wasabato wanaabudu Siku ya Saba ya juma, JUMAMOSI,

Wao Wana comment wapi?
 
"Sijui nianze wapi Maana kifuani nimebeba mengi na sitatenda haki nisiposema hiki napenda kile sipendi, kile sitaki mambo ya kishenzi"
Dini ni tatizo
Dini ni shida
Dini ni njiapanda
Dini ni kichaka.
Ukienda mbio kwa kukariri utajikuta nje ya mchezo huku ukikomaa na mtu tatu ndani ya track moja.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Niende kwenye hoja

Huwezi ona msabato akimsema muislamu kuwa ati anafanya dhambi kuabudu siku ya ijumaa ila ni kawaida kumsikia akimuhesabia dhambi Mkatoliki kwa kuabudu jumapili badala ya jumamosi

Kwa msabato siku ya jumapili ambayo ndiyo aliyofufuka Bwana yetu Yesu Kristo ni Alama ya Mnyama!

Swali langu kwa Wasabato siku ya Ijumaa ni Alama ya nini hasa kimaandiko?

Kwanini kuabudu jumapili ndiyo dhambi lakini ijumaa sijawahi sikia au kusoma sehemu yeyote kuwa ni dhambi?

Why? Why?

Nasubiri elimu kutoka kwa wajuzi
Wasabato hawana sababu ya kukujibu maana Waislam hawadai kumwabudu Mungu yule anayeabudiwa na Wakatoliki na Wasabato.

Wasabato wanawajibu Wakatoliki kwa sababu wote wanadai kuabudu Mungu mmoja
 
Back
Top Bottom