Jidandanye utaenda mbingu ya maboksi
Mungu ni Mungu wa taratibu
KUTOBADILIKA KWA SHERIA YA MUNGU.
Soma Mathayo 5:17, 18; Zaburi 111:7, 8; Mhubiri 12:13, 14; 1 Yohana 5:3; na Mithali 28:9. Je, vifungu hivi vya Biblia vinafundisha nini kuhusu uhusiano wa Mkristo na sheria?
Waadventista wa Sabato wanafuata nyayo za wanamatengenezo wa Kiprotestanti ambao walitetea utakatifu wa sheria ya Mungu. Zingatia uthibitisho huu mzito wa John Wesley: “Kaida au sheria ya kiibada iliyotolewa na Musa kwa wana wa Israeli, ikijumuisha Sheria zote za makatazo na kaida zilizohusiana na dhabihu za zamani na huduma ya hekalu, Bwana wetu kwa hakika alikuja; kuharibu, kufuta na kukomesha kabisa... . Lakini sheria ya maadili iliyomo katika Amri Kumi na kutekelezwa na manabii, hakuiondoa. Halikuwa kusudi la kuja kwake kubatilisha sehemu yoyote ya hii. Hii ni sheria ambayo kamwe haiwezi kuvunjwa, ambayo 'inasimama imara kama shahidi mwaminifu mbinguni. ' ... Kila sehemu ya sheria hii lazima iendelee kutumika, juu ya wanadamu wote na katika enzi zote; pasipo kutegemea wakati au mahali au hali nyingine zozote zinazoweza kubadilika, bali juu ya asili ya Mungu na asili ya mwanadamu na uhusiano wao usiobadilika kati yao wenyewe.— “Upon Our Lord's Sermon on the Mount,” Discourse V, John Wesley's Sermons: An Anthology (Nashville, TN: Abington Press, 1991), uk. 208, 209.
Linganisha Kutoka 34:5-7 na Warumi 7:11, 12; Zaburi 19:7-11; Zaburi 89:14; na Zaburi 119:142, 172. Vifungu hivi vinatuambia nini kuhusu uhusiano kati ya sheria ya Mungu na tabia ya Mungu?
Kwa kuwa sheria ya Mungu ni nakala ya tabia Yake, msingi wa kiti Chake cha enzi na msingi wa maadili kwa wanadamu, Shetani anaichukia. “Hakuna mtu ambaye angeshindwa kuona kuwa ikiwa hema ya duniani ilikuwa mfano au nakala ya hekalu la mbinguni, sheria iliyohifadhiwa katika sanduku la agano la hema ya duniani ilikuwa ni nakala ya sheria iliyoko katika sanduku la agano la mbinguni; na kuwa kukubali kwa imani ukweli kuhusu hema ya mbinguni kulijumuisha kutambua madai ya sheria ya Mungu na madai ya Sabato ya amri ya nne. Hapa ndipo kulikuwa na siri ya upinzani mkali na wa makusudi dhidi ya ufafanuzi wenye mwafaka wa Maandiko yaliyofunua huduma ya Kristo katika hekalu la mbinguni.” — Ellen G. White, Pambano Kuu, uk.360.
Je, ni sababu zipi ambazo watu hutoa mara nyingi kama hoja kwamba hatulazimiki tena kuzishika Amri Kumi? Unafikiri ni nini hasa kiko nyuma yake?
🙏🙏🙏🙏