Wasafi Festival Mbeya hali imekuwa tete. Zuchu akimbia Jukwaa

Wasafi Festival Mbeya hali imekuwa tete. Zuchu akimbia Jukwaa

Video inaonesha Zuchu akirushiwa chupa na wakurungwa. Hawataki aendelee naye aamua kuzila kurusha mic na kuondoka.

Wanaonekana wamechafukwa sana. Mbaya zaidi kuna mwimbaji ambaye alikuja lalamika kuwa jamaa wa huko ni wajeuri hawataki kuimbishwa. Wanasikika wakisema wanamtaka mke wa P.Diddy. Hawa ni wendawazimu yaani mke wa P.Diddy aje kuperform Tanzania? tena Mbeya? hawapo serious. kesho na keshokutwa watakuja kudai apelekwe Mke wa Dr. Dre au wa Jay Z au hata mke wa Justin Timberlake.

View attachment 3110354
Ujinga mtupu, kama msanii humtaki si ulale kwako
 
😁😁😁 Sawa Ila aliyepata hasara ni nani hapo kati ya aliyelipa kiingilio na kufanya vurugu na aliyelipwa na haku-perform

Then hii sio Mara ya kwanza kutokea
Nchi hii wajinga ni wengi sana, ajabu mtu anafanya upuuzi kuna watu wanafurahia , bahati mbaya hao hao wanao furahia huo upuuzi, wengine wakifanya wao wanachukia
 
Kilichotokea kwa Zuchu ni matokeo ya malezi mabaya kwa watoto
1. Kuna show alifanya ya kumkaribisha Biteko baada ya kuwa Naibu Waziri Mkuu, wakati MC anamwambia muda wake umeisha, atampatia muda tena baada ya Biteko kumalizq hotuba yake, yeye akamjibu anatakiwa kuwahi Mwanza kupanda ndege, hivyi amuongeze dakika 10 amalizie nyimbo zake. Haikuwa sawa kabisa.

2. Kuna kipindi alikuwa anapost kuhusu matatizo ya kukatika katika umeme, mtu ambaye anabenefit na system ya serikali, analipwa 50mil kwa show, ela ambayo ingeweza kwenda kujenga shule, hospital, etc wenzake wote wanakaaga kimya, yeye kuongea haikuwa sawa kabisa.

3. Kutupa mic chini Mbeya ni utovu wa nidhamu.
 
Burudani zibaki kuwa burudani na siasa zibaki kuwa siasa.

Nakumbuka hata wakati wa Yanga Day Harmonize aliingia na T-shirt yenye picha ya Samia kifuani alizomewa hadi akaivua.

Hili liwe fundisho kwa wasanii wengine wenye tabia hizo kwa vile mashabiki wao ni waumini wa vyama mbalimbali na itikadi tofauti.

Mbeya wameanza bado Mwanza, Ar Chuga, Mara, Kagera, Singida, Iringa, Moro nk.

Wasipojirekebisha wataendelea kupigwa mawe na kuzomewa kila mkoa watakaoenda kufanya matamasha yao na kuharibu brand zao.
 
We msaniii anapanda jukwaani , mwanaume mzima umekaa pale mbele una watoto nyumbani na mke halafu anaanza kuimba...

Kuna kitu kimoja
Kwa jina sitokitaja
Ah! Kipo kidude hiko
Kwa jina sitokitaja
Ukiona cha simama
Jua kinataka kinyama
Ukiona kimelala lala hakikuachi.....?

Halafu anawaacha mmalizie... Hivi hata kama ni wewe utafanya uamuzi gani?😂😂

Hata kama ni kiti utarusha...
 
Burudani zibaki kuwa burudani na siasa zibaki kuwa siasa.

Nakumbuka hata wakati wa Yanga Day Harmonize aliingia na T-shirt yenye picha ya Samia kifuani alizomewa hadi akaivua.

Hili liwe fundisho kwa wasanii wengine wenye tabia hizo kwa vile mashabiki wao ni waumini wa vyama mbalimbali na itikadi tofauti.

Mbeya wameanza bado Mwanza, Ar Chuga, Mara, Kagera, Singida, Iringa, Moro nk.

Wasipojirekebisha wataendelea kupigwa mawe na kuzomewa kila mkoa watakaoenda kufanya matamasha yao na kuharibu brand zao.
Misukule ya mzee Mbowe ni shida
 
Back
Top Bottom