Wasanii toka Arusha acheni kujibagua na kupigania mkoa badala ya taifa

Acheni wivu Arusha tumewazidi Sana kimaendeleo....acha tujitenge
 
Ukiona mtu analalamika kubaguliwa ujue amechoka kujipendekeza. Watu wa Arusha wanajikubali na life style yao, wala siyo ubaguzi haiwzekani mtu wa Arusha na Mzaramo wakakaa wakafanya dili ni michosho tu
 
Wenye akili ni kina nani huko, labda siwajui.

Furu na Udaga ndio chakula sahihi cha kuwafanya watu na Afya na ukakamavu.

Arusha na Moshi kuna nini ?

Ndizi na Kitimoto ???

Una ushahidi na hili ?

Au ushapiga Kiwingu ??
Wanaokulaga ma udaga na ugali hawanaga akili, kazi Yao kutumia nguvu badala ya kuwa smart
 
Washamba wakishavaa mamitumba yale wanajikuta wanajua wabaguzi huko maofisini sana
Mimi ni mzaramo, kuna biashara moja naifanya hapa Morogoro mjini, mtu aliyenipa wazo la kufanya hiyo biashara ni dada mmoja wa kichaga japo ni mkazi wa Arusha, sasa sijui kwanini upuuzi wa mtu mmoja au wawili unaujumuisha kwa watu wote wa Arusha.
 
Mwanasiasa yupi ?
Godbless Lema au ?
 
We mtu wa Tanga?
 
Arusha nako Kuna Wasanii....? Toka lini?
Wamewai kutikisa Wapi..!
Huko Ukisema Choir upo Sahihi....Kwaya zao zilipata umaarufu sana ... baada ya Kupigwa jeki na ile studio ilijiita sijui Radio Maalum.
 
John makini alitoa ngoma na a.k.a akiisifu dalaja mbili na ngareloo, nahisi alitegemea ile ngoma isikike Arusha tuh... ile collabo ilikuwa ya International a.k.a yeye aliiwakilisha SA hku ndugu yetu ameng'ang'ania ngareloo
haya mambo yanaturudisha nyuma sana...
 
najaribu tu kuwaza kwa arrogant, aggressiveness and ego ya vijana wa arusha na ubaguzi wao kwa vijana wengine wasio wa arusha, mkoa wa arusha ndio ungekuwa the main commercial city of tanzania, sisi wengine wangetufurusha na mapanga turudi tulikotoka.

nyerere aliona mbali sana kuufanya mkoa wa dar es salaam uwe jiji kubwa la kibiashara tanzania likikusanya watu wa makabila yote wanaoishi kwa upendo bila kubaguana.

pongezi za dhati ziende kwa wazaramo, wakwere na wandengereko kwa namna walivyo loyal kwa watu wengine ambao sio wa asili ya pwani.
 
Jay z mbona kasifia New York
 
Tatizo majamaa hata kwenye maisha ya kawaida wao hujitenga. Diamond ukitoa haya mabifu yake na kina kiba & harmonize lakini lazima tukiri hana haya mambo ya ukanda. Harmonize from Mtwara, Rayvany from Mbeya ambao chini ya Diamond wamekuwa wakubwa. Lakini ukija Weusi wanaojiita kampuni ni kwamba wote wametokea sehemu moja na ni ngumu kusikia hata wanasajili msanii toka kwingine.
 
Hawana tofauti na wasauzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…