Wasanii wa Bongo Fleva heshimuni dini za watu

Duniani Dini moja tu ya Rastafalaaaa haina shida na mtu, hizo nyingine ni upuuzi tu mnawindan
 
Muziki ni ushetani mtupu. Uwekezaji uliofanywa na shetani kwenye muziki ni mkubwa mno na unamlipa. Sasa hivi hadi kwenye injili nako kuna uchafu wa kutosha.
Ule mziki unaoimba
Tanzania ya sasa mamaaa🎶1
Ya mama samia mamaa🎶

Ni ushetani au siyo ushetani?
 
Muziki utakuwaje haramu wakati kina Musa na Daudi na Solomon wote walimwimbia Mwenyezi Mungu na wakatunga mashairi ya kumsifia? Muziki unapaswa kuwa sehemu ya ibada ya dini yeyote ya kweli. Kama dini haina muziki au mashairi ya kumsifu Mwenyezi Mungu, basi inatia shaka sana
 
Kati yako na Pope Francis aliesema mashoga wabarikiwe ni nani anaujua ukristo?
Mzee ukristo hauendi hivyo hata kidogo, kujua ukristo na kutojua ukristo hatuangalii nafasi yako kanisani au umesoma biblia nzima mara ngapi, tunaangalia unachosema na unachokifanya, kama pope Francis kafanya/katenda yasiyoendana na ukristo bac tunamhesabia hajui ukristo kabisa.
 
Au Buddhism, wale jamaa hawana habari na mambo yasiyoonekana sijui Mungu, shetani uchawi hawana mda navyo , pia hawana zile mambo za eti miujiza sijui mbinguni na motoni
 
Uislamu sio dini ya mzaha Wala kukurupuka ina misingi yake katika hukumu na sio kama unavyosema ambazo ni stori za kuokoteza.

Yaani mtu apigwe tu je kama Tahira au hafahamu kitu ? Kuna kisa Enzi za Mtume Muhammad (Peace and blessing be upon him) alikojoa kwa makusudi ndani ya Msikiti akaelekezwa Kisha akaachwa bila kupigwa.
 
Wewe ndo haujui ukristo yani umezaliwa kuzuramimba kigoma alafu uujue ukristo kuliko pope francis?
 
Dini ya kweli haiwezi kupimwa kama ulivyoandika...
 
Una jaribu kujustify uovu wa dini unayoitaka
Hapana, huwezi kupima ukweli wa dini kwa kuingia ibadani na kukashifu waumini Kisha uone kama utapigwa au la?....huo ni ugonjwa wa akili
 
Hata wasanii wa kikiristo bongo wengi wanaongoza kufanyia mzaha ukiristo ni wengi tu Baddest ,Rosalee nk.

Huko Ulaya ndio usipime kanisani linageuka disco watu na vichupi, mabangi pombe wanacheza kifuska Kanisani mfano nyimbo Moja ya Shaggy na nyinginezo.
 
Hata wanaofanya comedy hasa Hawa stand up comedians wanaudhalilisha ukristo hasa madhehebu ya kilokole,ila wakristo wapi kimya maana wanafundishwaga amani na upendo ila Hawa wa upande wa pili wanawazaga mabomu na kuchonjana
 
Dini gani iheshimiwe ikiwa wenye dini zenu hamjiheshim kabisa?
 
Hatujiheshimu! dini nyingine wataanza vipi kutupa heshima?

Mfano mzuri ni video ya Zuchu ft. Diamond Mtasubiri kanisa la Pugu wamepewa hela wakawapa kibali cha kuigiza bongo fleva kanisani.
Heshima haitupeleki mbinguni, tuishike imani kwa imani, hizo kejeli watahukumiwa wao
 
Yes, ndo maana nimesema wasanii, sija-generalize.

Pia, huu uzi ume-base kweny bongo fleva ambao ni mziki wetu, hao wakina shaggy achana nao.
 
alijaribu salman rushdie kwenye kazi yake inayoitwa satanic verse. Upo dunia gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…