Wasanii wamjia juu Fid Q kwa kufanikisha Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Wanamuziki wote Tanzania

Wasanii wamjia juu Fid Q kwa kufanikisha Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Wanamuziki wote Tanzania

ivi kweli industry ya muziki tanzania na manomination ya wasanii wetu kwenye tuzo kubwa bado wanaweza kikao hata kingekua cha koridoni tu kiazimie ile takataka isemee tasnia???

Ooh come on!!!!!
 
Watu mnashangaza sana usifikiri eti waliokuwa bora kuimba watakuwa bora kuwasemea.

Hao ulio wataja ni wako vyema kwenye sanaa ila si usemaji.

Wengine kwenye hiyo list wana elimu na uzoefu wa utangazaji na u-emcee. Sasa usemaji wa fani na kazi waliyochagua utawashinda kweli?
 
Bongo mizengwe mingi aisee, sasa msemaji wa wasanii manaake nini? Au wasanii mabubu?
 
Kama umelifuatilia hili sakata Fid Q wala hana kosa kama mnavyo msakama.

Kuna mjumbe mwingine nahisi anacheo kikubwa pia (Jina nimesahau) amemkingia kifua Stive Nyerere na kusema waje na sababu za kupinga uteuzi wake.

Je, huyo nae ni Fid Q? Watu mnajaribu kumu attack Fid sijajua kama Fid kuwa Fid labda mnachukia.

Anaitwa Ado!
 
Title haiendani na content uliyopost

Maybe wewe ni mtupu zaidi ya huyo unayemponda
Pengine ana personal issues na Fid Q na ndio maana kajikita kwenye uwezo wake wa mashairi kuliko mada aliyokusudia ya shirikisho
 
Wengine kwenye hiyo list wana elimu na uzoefu wa utangazaji na u-emcee. Sasa usemaji wa fani na kazi waliyochagua utawashinda kweli?
Swadakita kabisa lakini kuna wengine hapo wanaweza kuwa bora kwa mitazamo ya Watu lakini wao binafsi wakabolonga.

Sema Steve Nyerere kashaingia gundu kwa watu wengi na ndio sababu ya hayo yote.
 
Halaumiwi kama Fid Q... analaumiwa kama KATIBU.... kifupi Fid katoa Boko
 
Fid Q akiwa kama Katibu Mkuu wa Shirikisho, alionesha wazi ana uwezo mdogo wa kufikiri, kivipi msanii nguli kama yeye alimpa "sapoti nzima" Steve Nyerere 🤓🤓 kuwa msemaji wa wana muziki ??

Hakuna kazi rahisi kama kufanya muziki anao ufanya Fid Q. Anacho kifanya Fid Q ni kutafuta best quotes kuhusu mada anayo taka kuiandikia wimbo alafu hutafsiri kuja kiswahili na kufanya ionekane kama wazo lake, kwa hali hii wasikilizaji wake wengi wanamuona genius kimakosa.

Fid Q huwa anaonekana genius kwa sababu huwa anajipanga na kufanya maandalizi makubwa kabla hajatema mistari kwenye mic, ila sasa likijaga swala linalohitaji uwezo wa kufikiria asilia ambalo halihitaji maandalizi wala kujipanga kwa mfano kwenye maamuzi, hapa ndipo huwa anatuacha midomo wazi.
Kuna jamaa yangu ananiambia Fid ni mtu mwenye jealous na roho mbaya sana tofauti na watu wanavyomchukulia na haya malalamiko yapo mengi sana na ni ya muda mrefu,kuna wasanii waliwahi kulalamika Fid aliwabania kufanya collabo international na ni mtu wa figisu na majivuno sana..No wonder ana ukaribu na mtu kama Steve Nyerere
 
Wasanii wa bongo kwanza wengi hawaendi kwenye vikao,na mishe kama hizo nyingi Steve ameingia baada ya kuona wasanii wanajivuta yeye anajichomeka kushtuka kumbe ni fursa kwa jamaa
 
Hii issue ina siasa, seems kuna kundi huko CCM wanataka kulihodhi then litumike kisiasa! It's shame Rais wa shirikisho ni mtu wa injili.

Hiyo nafasi ya Steve ipo kikanuni na vigezo vimetajwa, Steve kapatikanaje? Wanachanganyikiwa sasa sababu mwenzao Mwanafa amekaza!

Kwasababu linaenda kisiasa sasa acha tulipeleke kisiasa!
 
Hii issue mbona watu mnaikuza sana what's so special??
Ni issue ndogo lakini ina siasa ndio maana inakuwa kubwa! Kama unajua kazi za Steve unajua nini kinafata! Bushoke aligusia jana! Rais wa shirikisho aliongea pia kwamba wanaomkataa Steve ni wanaharakati ambao pia wanaotusi serikali! Sasa hapo kuna mipango ya wasanii au mipango ya kisiasa?
 
Nimemuelewa sana Steve akee komaa achana na wanafiki vikao hawahudhurii umechaguliwa wanaleta nyenyenye..masaa 48 ya bibi yake[emoji1][emoji2][emoji2][emoji1]
 
Back
Top Bottom