Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Pambana tuu mkuu haupo peke yako
Vita ni vikali sana hakuna kukata tamaaa.... Mitindo ya maisha nayo sometime imetuleteleza huku.... Nikikumbuka mitonyo nilivyokuwa natapanya nikiwa peke yangu Sina majukumu.....natamani kurudisha miaka nyuma lakini hakuna namna ndio maana nasema kipindi Cha Kwanza nimepoteza.... Nna kazi ya kusawazisha na kushinda hili pambano hakuna kukata tamaa .... Vita vitapiganwa hivyohivyo hata Kwa kombeo kama Daudi.....
 
Mkuu hivi..
Mda sahihi wa kupambana na upi..?
 
Usijali kijana, life starts at forty , wewe endelea kutembea kifua mbele .
 
Ww siyo masikini,shida unajilinganisha na wngine,maisha siyo ushindan kaka utapoteza focus na unachokifanya utaanz kutamani vya watu!!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Siyo usipojilinganisha na wenzio au kuwa na wivu na mafanikio ya wenzio huwezi kupata hasira na munkari wa kupambana ili na wewe utoboe...
 
huwezi mfosi mtu. ila kuna mmoja kaniachia suti ya kuvaa
 
Utakufa Kwa kihoro ...hapo ulipo ndio mtafuto wako ...jichanganye Sasa kuiga kunya Kwa tembo yakukute.... Ridhika na unachopata kama unaamini Mungu ..wakati wa Mungu ndio wakati sahihi ilifika zamu yako utajipata .
Acha kumdanganya mwenzio, yeye ameshajua tatizo lake kuu na hilo tayari ni jambo kubwa... Huwezi kukaa kwenye maisha bila ya kujitathmini na kuona uko wapi ukilinganisha na wenzio mliokua wote.
 
Hivi haka kamsemo huwa kana maana gani...?
Ndio kipindi Cha pili hicho Cha mchezo /Maisha.....life expectancy inacheza 60-65.. hapo nusu ya uhakika wako wa kuishi umesha uishi na bado unajitafuta ...utajitafuta uzeeni ?? Hapo ndio una 10 yrs ya kuweka sawa mambo. Ukizingua hapo ndio ntolee ... Usharithisa umaskini Kwa kizazi chako.... Unawapa kazi ya kujitafuta na wao.
 
Bilashaka Mungu amekuonyesha na umekiri kuona..
Anataka utumie marifa yako na uwezo alokupa, ufanye bidii uwe kama hao ulowaona wako tinted za black na migari ya maana.....
Wakati ni wako
Hakikasha mwaka 2025 haupiti bila kupokea muujiza wako...
 
wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.

> Kubarikiwa kuwa na wazazi tuu mpaka hapo ulipo ni utajiri usio fananishwa na chochote mkuu.
 
Kama mimii tu kak tujifariji kaka never give up
 
Acha kumdanganya mwenzio, yeye ameshajua tatizo lake kuu na hilo tayari ni jambo kubwa... Huwezi kukaa kwenye maisha bila ya kujitathmini na kuona uko wapi ukilinganisha na wenzio mliokua wote.
Ndio ungesoma nilichondika Kwa kunielewa .... Ila naona umesoma kujibu. Unachosema ndio nimesema .... Afanye mambo yake Kwa utaratibu wake "asiige tembo" .... Hao wenzake anajua michongo Yao!!! Watu Wana michongo ya hatari kupitia vijiframes tu na vikampuni vya mfukoni...ukicheki uhalisia Wana michezo ya hatari sana ... Ndio nimemwambia afanye Kwa uwezo wake na wakati wa Mungu ni sahihi sijamwambia aache kupiganisha ... Awe makini na mapambano yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…