Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

wengine hata hio mifumo kuingia hatuipati.

ukosahihi chief,wengi husema kuwa subra wakati wako upo.
 
Hapana pambana mkuu umasikini ni wakuuchukia kwa nguvu zote mastaaa, ukiwa huna kitu unakuwa na mawazo magumu magumu tu yani unakuwa na hasira, kisiran yan kila aina ya upuuzi, mzee bado hujachelewa pambana, nakumbuka kuna mwaka me hadi ndugu wote tuligombana nlikuwa sina hili wala lile wao wakawa wanaona kama nakosea yan mtu unapitia magumu alafu ndugu wanaona unakosea, nlikuwa mkali nlikuwa nawachenchia mpaka nlivyofanya revolution ndio nikarud nikawa normal, nikubali kabisa nilikuwa nimevurugwa aisee acha kabisa mkuu. Hakuna kukata tamaa mkuu jichanganye masta utakuja kujipata tu one day kila kitu kitakuwa poa aisee
mkuu unataka kusema niridhike na hali ya ufukara?
umas
 
Noted chief
 
Jizabe shaba ya kichwa. Manake kweli huna maana kabisa
 
Uko pale Mkwanaboo nini bro!? 😲 Au Uswaa, Mkwarungo?.…. 🤔
 
Binidamu tumeumbwa kuhangaika na kuzoea. Wewe ndugu yangu hauna umasikini bali umeizoea hali uliyonayo. Ukikizoea kitu au hali unaiona ya kawaida sana na mwishowe haina thamani. Na akili yako ikikosa kuchangamka inatafuta changamoto mwishowe unatafuta kasoro kwenye mahali ambapo hamna kasoro. Unachotakiwa kufanya ni kuamka na kupambana mpaka uzoee kupambana na ubadilike. Kuna watu wamezoea ku hustle mpaka wakikaa siku moja tu nyumbani wanaumwa. Ukishazoea kupambana hautochoka maana utakuwa umeshazoea hali ya kutafuta na kuwajibika. Maana akili zetu zimeumbwa zichakarike na zizoee vitu vipya kila siku. Jilinganishe na wewe wa jana yako usijilinanishe na mtu mwingine. Jiulize kama Bakhresa angekuwa anajilinganishe na wapemba wenzie angekuwa tajiri mkubwa leo hii. Maana kumiliki mjengo Masaki tu angeridhika na si kuongeza boti za Azam au kumiliki timu za mpira wa miguu. Jizoeshe kujifunza kitu kipya kila siku na pia jikubali na usikate tamaa. Pambana ukipiga hatua kidogo jiüpongeze kidogo then rudi katika kupambania ugali. Usibweteke ukapiga hatua kidogo halafu ukajiachia. Pumzika kidogo halafu rudi kupambania ugali. Mungu akubariki na akulinde katika upambanaji.
Namuunga mkono kwa asilimia mia moja huyu mwanajamii maana amenisaidia kuifafanunua pointi zangu hapo juu.
 
Akiacha huo ualimu si atakufa njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…