Wasichokijua Wengi Kuhusu Marko 10: 25 katika Biblia

Imagine wewe ndio umepewa kazi ya kutafsiri biblia kutoka lugha ya kiingereza, unakutana na neno CAMEL.

Wakati huo neno hilo linamaanisha mnyama na kamba, je kulileta katika lugha ya Kiswahili si itabidi uangalie kati ya hizo mana mbili ni ipi ilinaanishwa?

Je neno NGAMIA si ndio neno unaloamua kuliweka?

How possible nalo liwe linamaanisha maana ile ile ya kingereza na kiyunani? Kwani kabla ya utafisiri lilimaanisha nini? [emoji23][emoji23][emoji23]

Ndio mana nina wasi wasi, huenda kati ya kamba au mnyama kimoja hakiitwi ngamia, lakini kwa kuwa neno limeshaandikwa basi tena inabidi tubatize.
Labda umeelewa.
 
Kwani waliotafsiri Bible ya Kiingereza kuja kwenye Kiswahili ni akina nani mkuu? Pengine unawa-overate kwamba hawawezi kukosea! Unapotafsiri, huwezi kuwa unatafsiri neno kwa neno ndiyo maana unashauriwa kusoma kwanza na kukielewa kile unachotaka kukitafsiri ili kupunguza makosa ya kimantiki kama hili!
 

No. Neno NGAMIA halijatoka kwenye lugha ya Kiingereza, sijui unatumia kigezo kipi, huenda neno ngamia lilikuwepo kabla hata neno camel halijaja kwenye muktadha wetu. Je lilikuwa lina maanisha kitu gani?


Kama TUKI wanasema ni mnyama, basi kimsingi ngamia ni mnyama, kama Biblia ina maanisha kamba ya nanga, je ile kamba haina neno lake kwa kiswahili?


Tazama bro, 36% lugha ya Kiswahili ni kiarabu, huenda tukisema kwa lugha ya kiarabu hii kamba ipo since hawa watu ni NAVIGATORS, ile kamba ya kufunga mashua zao baada ya safari ama uvuvi iliitwaje? [emoji16][emoji16]


Na wenyeji wa Ustaarabu wa Kiswahili waliitaje? [emoji16] ikipatikana inaitwaje basi Biblia inapaswa kuondoa neno NGAMIA na kuweka neno la hii kamba, japo utakuwa hujawatendea haki wanao maanisha TUNDU LA SINDANO as mlango wa Kuingilia mji wa Yerusalemu
 
Hiyo metaphor ya Ngamia inamaanisha kitu kile kile.

Whether mtu atamaanisha Ngamia ni kamba, ni mnyama, jiwe.

Na sindano ni sindano.

Maana ya hiyo metaphor inabaki kuwa MOJA.
 

Sisemi hawajakosea, namaanisha wanakosea, neno ngamia linabeba asili ya Mnyama, maana ambayo kwenye neno camel pia ipo, je neno hilo hilo lina maana ya kamba? [emoji16] kama sio, basi ibadilishwe
 
Biblia imeandikwa kwa lugha mbili tu
Agano la kale(Kiebrania
Agano jipya (Kigiriki)
Sasa ili kujua maana hasa ya maneno hayo lazma uanze kwenye Kigiriki kwanza. Angalia tofauti ya hata maneno
kaʹme·los=ngamia
kaʹmi·los= kamba

Sasa kupitia muktadha huo fanya utafiti utapa jibu vizuri achana Kilatin kilichoaribu kabisa maandiko matakatifu
 
Hujaweka hitimisho mkuu japo umefafanua vizuri kabisa!
 
Kuna tafsiri nyingi,ninayoielewa Mimi,ni kwamba,kwenye kifungu hicho,Anayezungumziwa ni ngamia mnyama,ila sindano sio hii tunayoifshamu,hapa sindano,kwa nyakati zile ni miti miti miwili imesimikwa chini Kama milingoti ya viwanja vya mpira,miti hii,ilitumika kussfishia Ngamia,Ngamia anapitishwa Kati Kati ya hii miti miwili,inakuwa inambana mbavuni,sasa anavyokuwa anapita kwa shida,uchafu,uliopo kwenye ngozi yake,unapaluliwa na hii miti,chukulia mfano wa mwiko wa kusongea ugari,unapotumia kisu kutoa Mabaki ya ugari,
Hii miti miwili ndio sindano,kwa kipindi kile,
 
Duh! Hii kali! Ndiyo nasikia kitu kama hiki kwa mara ya kwanza
 
Hata sindano zina ukubwa tofauti pia. Ila pale alimaanisha ngamia ukifuatilia mistari inayoendelea mbele

Ila haimanisho ukiwa lofa kabisa choka mbaya ndio njia yako kwenda peponi ni rahisi imenyoooooka.
 
  1. a large, long-necked ungulate mammal of arid country, with long slender legs, broad cushioned feet, and either one or two humps on the back. Camels can survive for long periods without food or drink, chiefly by using up the fat reserves in their humps.

  2. an apparatus for raising a sunken ship, consisting of one or more watertight chests to provide buoyancy.
 

[emoji16][emoji16] basi sio kamba, mana hapa ni ile apparatus, so ni nanga, not kamba
 
ndio na mimi naona maana ni nyingi kila dictionary inaelezea kivyake lkn sijaona hii ya mleta mada

Kuna kitu hakipo sawa na mtafsiri ww Biblia kwa lugha ya Kiswahili, sitaki kabisa eti itokee coincidence kwamba. Neno

Camela- kwa kilatini limaanishe kamba na mnyama

Camel- kwa kingereza limaanishe kamba na mnyama

Na NGAMIA- limaanishe kamba na mnyama [emoji1][emoji1] hapana, kuna kimoja hapa kinalazimishwa kuitwa ngamia.
 
Ndio hivyo mkuu, ni kamba. Shida imekuja kwa miaka ya karibuni kuibuka 'Viongozi wa dini' wasiopitia chuo cha theolojia kazi kubwabwaja tu kuhusu miujiza na mafanikio!
Ukisikia "mtumishi" wa namna hii ujue ni nabii wa uongo
 
Sure, wengi huwa hawalijui hilo, wanakariri vifungu vya Bible bila utafiti hongera mtoa mada

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…