Iselamagazi
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 6,020
- 6,161
Hii inaleta sense!Kuna tafsiri nyingi,ninayoielewa Mimi,ni kwamba,kwenye kifungu hicho,Anayezungumziwa ni ngamia mnyama,ila sindano sio hii tunayoifshamu,hapa sindano,kwa nyakati zile ni miti miti miwili imesimikwa chini Kama milingoti ya viwanja vya mpira,miti hii,ilitumika kussfishia Ngamia,Ngamia anapitishwa Kati Kati ya hii miti miwili,inakuwa inambana mbavuni,sasa anavyokuwa anapita kwa shida,uchafu,uliopo kwenye ngozi yake,unapaluliwa na hii miti,chukulia mfano wa mwiko wa kusongea ugari,unapotumia kisu kutoa Mabaki ya ugari,
Hii miti miwili ndio sindano,kwa kipindi kile,
Binadamu kujinyenyekeza (humbleness), kama ngamia anavyopita ktk mlango mdogo (eye of the needle) wa ukuta wa Yerusalemu. Ngamia huondolewa mzigo mgongoni mwake na kukunja miguu yake (kupigishwa magoti) ili aweze kupita katika mlango huu mdogo wakati wa usiku. Ni rahisi ngamia huyu kupita ktk mlango huu mdogo na kuingia ktk mji wa Yerusalemu au ni rahisi ngamia kupita katikati ya miti miwili inayobana ili aweze kusafishwa uchafu ulio ktk ngozi yake.
Kumbe metaphor hii ni kwa ajili yetu sisi binadamu. Kama tunaweza kujishusha na kupitia mlango mdogo/njia nyembamba baada ya kushusha mizigo yetu ( viburi, majivuno, husda, visasi, wizi, uzinzi ...), tunaweza kuingia ktk Yerusalemu mpya.
If we humble ourselves and pray on our knees, we can approach the kingdom of heaven.