Wasifu wa Naibu Waziri wa Ajira Eveline Munisi

bro mimi ni retired man,nimefanya kazi nyingi tu nje ya nchi hii,nimezaliwa na mzazi mmoja mtanzania na wa pili sio mtanzania.Nina makazi nje na ndani ya nchi,nineoa nje ya ya nchi na tanzania pia.Sio mtu wa siasa,sina chama cha siasa na sihitaji mtu wa kunipa kazi.Siandiki kujikomba kwa mtu naandika kutoa mawazo yangu huru kabisa
Siasa ndio MAISHA, ukisema hushiriki kwenye siasa maana yake u mfu..Siasa huamua ajira n ujira wako,Siasa huamua huduma za Jamii kama Afya ,Maji na Shule...Siasa huamua bei ya PETROL, kuwahi kulala or kuchelewa...unaweza usiwe kwenye kundi la Wanasiasa( active) lakini lazima ushiriki kwenye uwanja huu wa Siasa..Hata kukemea Maovu na huduma mbovu kwa Mama Tanzania( Tanganyika) ni Siasa...
SIASA ni MAISHA, Siasa ni UHAI, SIASA ni MAENDELEO
 
Sishiriki siasa kwa kuwa na chama wala kushabikia siasa hadharani,napiga kura ya siri na kuondoka,huo ndio uamuzi wangu,wewe huwezi kunipangia nishiriki siasa kwa njia ipi,kama ambavyo wewe sikuingilii wala kukushauri juu ya njia ya kuifata
 
Hiyo kupiga KURA nayo ni SIASA..pia tunajaribu tu kuelekezana ,wala usichukulie hasira, relax..nchi ina mengi mazuri yanakuja
 
Watu wenye mtazamo wa kizamani, wanatangulia kuangalia vyeti vya mtu ili wampe heshima na nafasi. Lakini dunia ya leo inaangalia nini umefanya kwenye jamii
Nenda katafute taarifa sahihi kuhusu Elon Musk, kielimu na kwa vitu vingi hawezi kufanana na mtu ambaye hata form four alifeli.

Elon Musk hana masters wala PhD! Ana degree ya Physics na Uchumi. Hapa bongo zimejaa PhD na Masters za Physics na Uchumi lakini zimeishia tu kuwa kwenye bahasha zikitembezwa mitaani kutafuta ajira! Elon akiandika profile yake wala huwa hazitaji hizo degree zake lakini anataja vitu alivyofanya! Wengine wakisema wasifu wake ndio wanaotaja degree zake.
 
Huwezi amini, Elon Musk alisajiliwa aanze program ya PhD lakini baada ya siku mbili tu aliona anapoteza muda akaamua KUACHA!!
 
ELIMU MBALIMBALI zinaendelea kuongoza NCHI yaan samia anataka ahakikishe nchi inaongozwa na mandez
 
Bill Gates yeye hata degree hana! Aliondoka chuoni kabla ya kuhitimu degree yake! Akajikita kwenye kufanya vitu!! Leo hii hakuna mtu asiyemjua Bill Gates!!
 
Watu wenye mtazamo wa kizamani, wanatangulia kuangalia vyeti vya mtu ili wampe heshima na nafasi. Lakini dunia ya leo inaangalia nini umefanya kwenye jamii

Elon Musk hana masters wala PhD! Ana degree ya Physics na Uchumi. Hapa bongo zimejaa PhD na Masters za Physics na Uchumi lakini zimeishia tu kuwa kwenye bahasha zikitembezwa mitaani kutafuta ajira! Elon akiandika profile yake wala huwa hazitaji hizo degree zake lakini anataja vitu alivyofanya! Wengine wakisema wasifu wake ndio wanaotaja degree zake.
Wewe huelewi mada umekazana kuja na study cases kibao! Huyo evelyne cheti chake kimeandikwa vibaya na vyuo ambavyo haviexist, discuss! Nyie ndio mnafeligi kwa kujifanya mna maarifa mengi kichwani! Mada iko wazi discuss acha kutishia watu elimu ya elon musk mara bill gates we inakusaidia nini? Cheti chake kakianika mwenyewe lazima kijadiliwe hutaki tuone makosa tuongee? Kitu kikionekana kitajadiliwa tu hata kama sio hapa, mnasemaga waTz hawajitambui sasa kitu kimeonekana wazi hamtaki pia kiongelewe, unajisikia kweli?
 
Wewe huelewi mada umekazana kuja na study cases kibao! Huyo evelyne cheti chake kimeandikwa vibaya na vyuo ambavyo haviexist, discuss! Nyie ndio mnafeligi kwa kujifanya mna maarifa mengi kichwani! Mada iko wazi discuss acha kutishia watu elimu ya elon musk mara bill gates we inakusaidia nini? Cheti chake ve mwenyewe lazima kijadiliwe hutaki tuone makosa tuongee? Kitu kikionekana kitajadiliwa tu hata kama sio hapa, mnasemaga waTz hawajitambui sasa kitu kimeonekana wazi hamtaki pia kiongelewe, unajisikia kweli?
Moja wapo ya hoja ambayo watu wanasema ni kiwango cha elimu cha Eveline Munisi kuwa ni kidogo kulingana na nafasi aliyopewa. Wanadai kiwango cha form four halitoshi. Mimi nimejikita hapo kuzungumzia hoja ya kiwango cha elimu " in general" na si kwa Eveline tu!
Hoja yangu ni kwamba kiwango cha form four si kigezo cha kumkataa mtu kuwa hawezi au hafai, bali tutazame amefanya nini!! Wala kiwango cha masters au PhD si kigezo cha kumwona mtu anafaa au anaweza bali tutazame amefanya nini kwenye jamii!! Elimu ya mtu haitutushi bali tutatishwa na mambo ambayo ameyafanya kwa kusaidiwa na elimu yake! Kusapoti hoja yangu ndiyo nikaja na case ya Elon Musk na Bill Gates ambao kusema kweli si wasomi kwa mujibu wa vyeti vyao vya kitaaluma. Elon Musk ana degree ya Physics na Uchumi, na kwa dunia ya leo mwenye degree moja hahesabiwi kama ni msomi aliyebobea. Na Bill Gates yeye ndo kabisa hana hata degree moja. Lakini hawa wanaheshimika duniani kwa mambo waliyofanya na siyo kwa elimu yao!
Turudi kwa Eveline, yeye siyo Msomi lakini ni FOUNDER & CEO wa taasisi iliyomwezesha kujulikana kimataifa na kugusa jamii hasa upande wa wanawake! Amesafiri sa na duniani, ameendesha makongamano ya kimataifa nk, vitu ambavyo vimempa heshima katika jamii si Tanzania tu bali kimataifa! Kwa msingi huo vitu alivyofanya vinambeba!
Labda kama unatilia mashaka hata hiyo form four yake kuwa amedanganya! Kwa taarifa yako Eveline alisoma Kibaha Sekondari kipindi kile ambacho ilikuwa inachukuwa pia wasichana, baadaye iliacha kuchukua wasichana ikawa ni boys pekee. Kubalini exposure ya Eveline ni kubwa!! mpeni nafasi aonyeshe uwezo wake kwenye nafasi aliyopewa!
 
Ndio aandike cv ya uongo? Hivi hata mnaelewa mada inahusu nini?
Unathibitishaje kuwa CV yake ni ya uongo? Je hana elimu ya form four? Udaktari wa heshima anapewa mtu si kwa msingi wa elimu yake bali kwa msingi wa yale aliyoyafanya kwenye jamii kuwa yana mchango chanya kwenye jamii yake!!
 
Wewe una mahaba tu na huyo evelyne basi! Hiyo exposure unayotuandikia hapa uliluwa naye? All in all elimu ina nafasi yake hata ukiwa mbishi vipi matokeo yake tunapata aibu ndogo ndogo endapo proffesionalism ikihitajika katika jambo husika! Unaweza hata kubishana na mainjinia wakikuletea bajeti ya uongo au ndio umesimama na kina bill gates bado? Unalinganisha uwezo wa matajiri ya kibepari na mtu wa form four? Tena ya kibaha! Are you serious??
 
Utanichosha na michango yako chanya kwenye jamii nani ana michango hasi? Hata mwenyekiti wa mtaa na balozi wana michango chanya!

Rudi mwanzo ukasome vizuri mada sio kutetea tu ujinga na kuingiza points zisizohitajika!
 
Daaah sasa huyu atanishauri nini mimi na masters yangu mjini tukiitisha mdahalo utoki .

View attachment 3583132
Tuambie wewe na masters yako umeifanyia nini jamii ya watanzania! Watanzania tutakuthamini si kwa masters yako bali kwa mchango wako unaoshikika kwenye jamii. Kwa elimu umemzidi hata Bill Gates kwa mbali sana maana yeye hata degree moja hana! Lakini kama Bill Gates angekuwa mtanzania halafu ikaitishwa kura ya maoni nani anafaa kuwa waziri kati yako wewe mwenye masters na Bill Gates ambaye hana hata degree moja, unadhani watanzania wangemchagua yupi? Hiyo masters haijaweza kukusaidia hata wewe mwenye nayo, je itaweza kuwasaidia watanzania?
 
Wewe una mahaba tu na huyo evelyne basi! Hiyo exposure unayotuandikia hapa uliluwa naye? All in all elimu ina nafasi yake hata ukiwa mbishi vipi matokeo yake tunapata aibu ndogo ndogo endapo proffesionalism ikihitajika katika jambo husika! Unaweza hata kubishana na mainjinia wakikuletea bajeti ya uongo au ndio umesimama na kina bill gates bado? Unalinganisha uwezo wa matajiri ya kibepari na mtu wa form four? Tena ya kibaha! Are you serious??
Sijasema kuwa elimu haina nafasi bali nasema elimu si kila kitu! Na elimu kidogo si kikwazo kama pamoja na elimu ndogo mtu anaweza kufanya vitu chanya vya kuishawishi jamii! Watanzania tumeshuhudia wenye PhD wakifanya madudu!! Lazima tuone impact ya mtu kwenye jamii yetu, je ameonesha uwezo wa kufanya vitu? Hatukubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia!
Nimeleta case ya Elon na Bill Gates kama general case na si kuwalinganisha na Eveline na nilisema hivyo! Nia ni kusapoti hoja kuwa vyeti na ku-deliver ni vitu tofauti! Kuna wasiokuwa na vyeti vya juu lakini wamefanya vitu vikubwa kuliko mara milioni ya wale wenye makaratasi ya masters na PhD!!
Kuhusu Eveline na yeye ame-deliver! ni CEO & FOUNDER wa taasisi inayojulikana kimataifa, hata watu na akili zao wakashawishika kumpa udaktari wa heshima! Udaktari wake haukuja from nowhere!
 
Sijasema kuwa elimu haina nafasi bali nasema elimu si kila kitu! Na elimu kidogo si kikwazo kama pamoja na elimu ndogo mtu anaweza kufanya vitu chanya vya kuishawishi jamii! Watanzania tumeshuhudia wenye PhD wakifanya madudu!! Lazima tuone impact ya mtu kwenye jamii yetu, je ameonesha uwezo wa kufanya vitu? Hatukubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia!
Wewe utamtetea uwezavyo anachokifanya hata wewe unaweza kufanya ila elimu ina nafasi yake! Aibu ndogo ndogo kama kuandika wasifu wa namna hiyo ni jibu tosha yukoje kichwani! Kama ingekuwa haina maana tusingetumia cv kutafuta kazi au tusisome kabisa kwa sababu tu na wao hawakusoma au kwa sababu kuna vitu tunaviweza kuvifanya kwenye jamii!
 
Back
Top Bottom