Mahakaka gani inagawa Mali kwa taratibu za msahafuni na sio The law of marriage Act
Kwanza kabisa kwa mujibu wa sheria za mirathi..Mahakama haina jukumu wala uwezo wa kugawa mali za marehemu. Mahakama ina uwezo na mamlaka ya kumchagua msimamizi wa mirathi kwa kumpa mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria.
Msimamizi wa mirathi ya marehemu ndiye mwenye jukumu la kugawa mali za marehemu kwa warithi, kulipa madeni yoyote ya marehemu, yaani kwa kufupi ndiye anaruhusiwa kufanya chochote halali kwa manufaa ya warithi.
Mali ya marehemu inaweza kugawiwa kwa kufata miongozo mingi kulingana na marehemu alìkuwa mtu wa dini gani?, mtindo wake wa maisha ulikuwaje? Tamaduni za alikoishi zikoje..?
Kama marehemu alikuwa muislamu na aliishi kulingana na dini hiyo basi akifariki mali zake zitagawiwa kwa mujibu wa Quran tukufu. Quran imeweka viwango vya ugawaji wa mirathi ya marehemu...imetaja warithi na viwango wanavyostahili kupata.
Ndiyo maana hata kama muislamu akiandika wosia hauzidi ⅓ ya mali zake, ⅔ itagawiwa kwa mujibu wa Quran tukufu. Hivyo msimamizi wa mirathi ya marehemu aliyekuwa muislamu, lazima agawe mali kwa mujibu wa Quran.
Hivyo kwanza kwa mujibu wa andiko lako, si sheria ya ndoa inayotumika kwenye mambo ya ugawaji wa mirathi. Kuna sheria mahususi za mirathi nchi hii kama, Probate & Administration of Estates Act na kanuni zake, Magistrates Court Act na kanuni zake, Indian Succession Act, Local customary declaration Order, Mohammedan Law, etc. Pili, mahakama haina mamlaka ya kugawa mali za marehemu bali ni msimamizi wa mirathi tu ndiye mwenye hayo mamlaka.