Wasioamini Mungu inawahusu

Wasioamini Mungu inawahusu

Kukataa uwepo wa Mungu ni ugonjwa wa akili na kiburi kilichoshindikana.
Huyo Mungu aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kukataa uwepo wake?
Akili kushindwa kujua Mungu ni nani, ni nini, alitoka wapi, anafanana je, aliumbaje ulimwengu - haimaanishi kuwa hayupo -
Thibitisha uwepo wa huyo Mungu na si mawazo yako ya kufikirika tu.

Au kufosi imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.
ujinga sio sababu ya kukataa ukweli. Binadamu tutahangaika sana, tutajitutumua sana, tutaamini sana hizo bongo zetu ambazo mwisho wa siku zitaoza..lkn ndani mwetu kila mtu anajua Mungu yupo. Hata kitendo cha kuanza kupata mawazo kinzani kuwa yupo au hayupo ujue tayari yupo...asingekuwepo pasingekuwa na mawazo ya kujustfy kutokuwepo kwake.
Huyo Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Kila mtu angejua kwa uhakika na uthibitisho kabisa kwamba kuna Mungu.

Wala tusinge hitaji imani ya kujua uwepo wa huyo Mungu.

Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua kwa uhakika na uthibitisho kabisa Mungu yupo?
Mtu huwezi ukaanza kudebate whether nguo ni nyeupe wakati unaona kabisa na nyeupe...watu mtaanza kubishana nguo ni nyeupe sababu wote hamjui rangi nyeupe ni ipi au hiyo rangi mnayoibishia hamuielewi na hakuna mtu abayeijua..room ya ubishi inaanza pamoja na kuweka misimamo ya kujitia matumaini.
Kama hiyo nguo nyeupe ipo na inaonekana kabisa ipo, Wala haihitajiki maswali ya kuanza kuhoji rangi yake.

Maana tayari kila mtu anaiona kwa uthibitisho na uhakika kabisa kwamba kuna nguo nyeupe.

Huyo Mungu hayupo, ndio maana kuna maswali ya kuhoji uwepo wake.

Na wewe unayedai huyo Mungu yupo, Utoe uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Ili utu prove wrong sisi ambao tunasema hayupo.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo, Ni kwamba hayupo.

Na madai yako ya uwepo wa huyo Mungu ni madai ya UONGO na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimeumbwa, Hata huyo muumbaji wa kila kitu lazima awe ameumbwa.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimetoka sehemu fulani, Hata hiyo sehemu fulani lazima iwe imetokea sehemu nyingine fulani.

Hivyo hivyo to infinity...

Yani kutakuwa na waumbaji endless.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza tu chenyewe pasipo kuumbwa, Maana kitazua maswali ya kiliwezaje kuwepo pasipo kuumbwa.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina muumbaji, Hata Ulimwengu Hauna na Hauhitaji Muumbaji.
Ok sawa umeshindwa kujua umbali. Kwa nijuavyo Mimi umbali hauna mwisho ndo sababu Kuna magalax mengi yanaendelea huko.
Umesema Kama tumeumbwa hata muumbaji atakuwa ameumbwa. Sasa Kama ameumbwa wewe kinachokuchanganya Ni Nini? Upande wetu wakristo tunaamini alietuumba naye aliumbwa vilevile. Lakini ndo hivyo katuumba hata Kama aliumbwa.
 
Unajaribu kumuweka Mungu katika hisia za kibinadamu naona.Kwani wewe nani alikuambia kifo ni adhabu??Mtu akifa tunaumia sababu amekufa au tunaumia sababu hatutamuona tena?? Kifo ni nini hata kiingiliane na uwepo wa Mungu.
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu kabla ya kumhusisha na kifo.
Kama ukijua mtu akifa nini kinafuata then unahaki ya kumlaumu Mungu..lkn nina uhakika 1000% hujui kuna nini baada ya kufa , lkn unalaumu watu wanakufa.
Kutokujua baada ya kifo kinafuata nini, Kuna uhusiano upi na uwepo wa huyo Mungu?
Kifo tu kinaonesha how limited human beings are : unampenda mtu l, hutaki aondoke but huna cha kufanya au kuzuia..uwe na pesa usiwe na pesa, tajiri, Rais...HUNA cha kufanya - we are defenseless kabisa.Sasa kama tunashindwa kutatua hilo tatizo dogo tu ndo unafikiri akili hizohizo ndo zitamuelewa Mungu kweli???
Kutotaka mtu asife, kuna uhusiano upi au kuna dhihirisha vipi, na kuthibitisha vipi, uwepo wa huyo Mungu?

Kwanza mimi nasema ndio kuna dhihirisha kabisa kwamba Hakuna Mungu.

Kwa sababu una amini kuna Mungu, Unasali kila siku kumuomba akujalie Afya njema, Uhai na Uzima. Lakini bado, At the end you must die.

Je huoni kwamba huyo Mungu unayeamini kwamba yupo na anajalia uzima, afya njema na uhai, Hayupo?

Ndio maana hata umwamini na kumtumainia vipi huyo Mungu kwamba ndiye anayekupa Uzima na Uhai, Still You must die.

Je bado tu huoni kwamba huyo Mungu anayetoa uhai, afya njema na uzima hayupo?
 
Ikiwa huna uwezo mzuri wa kufikiri na kujenga hoja, nakushauri katu usianzishe mada za namna hii. Nijibu hili pia


Nani Alimuumba Mungu?
 
Ok sawa umeshindwa kujua umbali. Kwa nijuavyo Mimi umbali hauna mwisho ndo sababu Kuna magalax mengi yanaendelea huko.
Umbali hauna mwisho, kwenda wapi?

Maana umbali ni kutoka point moja kwenda point nyingine.

Kama hiyo point nyingine ipo na ndio unajua unakwenda huko, Je huo ni umbali usio na mwisho?
Umesema Kama tumeumbwa hata muumbaji atakuwa ameumbwa. Sasa Kama ameumbwa wewe kinachokuchanganya Ni Nini?
Hakuna Muumbaji aliyeumba Universe na vyote vilivyomo ndani yake.

Universe ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.

Hakuna Muumbaji yeyote yule, Aliyeumba chochote kile.
Upande wetu wakristo tunaamini alietuumba naye aliumbwa vilevile. Lakini ndo hivyo katuumba hata Kama aliumbwa.
Kuamini unaweza kuamini hata uongo na wala hukatazwi kuamini hivyo.

Hata ukiamua kuamini tuliumbwa na ma Aliens 👽 ni haki yako ya kikatiba kabisa kuamini hivyo.

Ila Ukianza kudai kwamba imani yako ina Ukweli lazima uithibitishe na utoe uthibitisho wa hiyo imani yako,

Ili tuhakiki, Je ni kweli hicho unacho kiamini kilituumba kweli au uongo.

Maana imani ni nyingi sana kuhusu kuumbwa kwa ulimwengu na kila mtu ana amini kwamba imani yake pekee, ndio imani ya kweli.

Sasa ili tujue ipi ni imani ya kweli au uongo lazima uwepo uthibitisho usio na mashaka yeyote kila mtu ajue kwa uhakika kabisa ni nini kiliumba ulimwengu.

Na wala sio kuhitaji imani tena, kuendelea kuamini.
 
Umbali hauna mwisho, kwenda wapi?

Maana umbali ni kutoka point moja kwenda point nyingine.

Kama hiyo point nyingine ipo na ndio unajua unakwenda huko, Je huo ni umbali usio na mwisho?

Hakuna Muumbaji aliyeumba Universe na vyote vilivyomo ndani yake.

Universe ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.

Hakuna Muumbaji yeyote yule, Aliyeumba chochote kile.

Kuamini unaweza kuamini hata uongo na wala hukatazwi kuamini hivyo.

Hata ukiamua kuamini tuliumbwa na ma Aliens 👽 ni haki yako ya kikatiba kabisa kuamini hivyo.

Ila Ukianza kudai kwamba imani yako ina Ukweli lazima uithibitishe na utoe uthibitisho wa hiyo imani yako,

Ili tuhakiki, Je ni kweli hicho unacho kiamini kilituumba kweli au uongo.

Maana imani ni nyingi sana kuhusu kuumbwa kwa ulimwengu na kila mtu ana amini kwamba imani yake pekee, ndio imani ya kweli.

Sasa ili tujue ipi ni imani ya kweli au uongo lazima uwepo uthibitisho usio na mashaka yeyote kila mtu ajue kwa uhakika kabisa ni nini kiliumba ulimwengu.

Na wala sio kuhitaji imani tena, kuendelea kuamini.
Hakuna kitu kiliweza kuwepo bila kuumbwa.

Neno la uchambuzi juu ya kuumbwa na maisha ndilo linalotutambulisha kwamba kweli tuliumbwa. Lkn kinachotutambulisha zaidi kwamba alietuumba yupo Ni lile neno kwamba anajidhihirisha baada yakumwamini.
Sasa, hapa nitakueleza baadhi ya matukio ambayo kimsingi yametokea baada yakumwamini na uyatilie maanani; Kuna wakati nikiwa nimeokoka pia nimepanga na jirani yangu pia alikuwa kaokoka.
Lakini nilikuwa namuwazia vibaya sana ananikera kwa kuhisi ananisengenya na mambo mengine mengi sana kiasi Cha kufikia kunuia kumfanyia Jambo baya sana.

Mungu Ni wa ajabu sana! Kesho yake nilikuwa nimepanga ndo nifanye hilo tukio baya. Lkn asubuhi jirani alinigongea mlango kwa maongezi, akaniambia" uwe na amani, Leo nimeonyeshwa na Mungu kwamba unanifikiria haya" yule jirani alinieleza mambo yote ambayo Ni mawazo ya moyo wangu, Jambo ambalo nilibaki nimeduwaa.

Kuna matukio mengi ambayo siwezi kueleza hapa na yote ya muhimu na ambayo naoneshwa na ninawaeleza watu kabla hayajatokea Kisha yanatokea Hadi watu wanadai Mimi Ni mchawi lkn wanashindwa kujua uwezo wa Mungu. Mfano meli ya mv spice ya Zanzibar, lile tukio mi nilioneshwa kabisa kabla halijatokea na likatokea.

Sasa wewe ambaye huamini katika Mungu unaweza kunieleza hayo yanatokea kwa namna gani?
Ujuaji unakuwa mwingi Hadi mnamkosea Muumba anawaacha hivyohivyo na mawazo yenu yaliyopotoka. Haikuwa rahisi kuwepo kwahiyo maisha haya yanagharama kubwa sana ndo sababu yasu aliumia msalabani kwaajili yenu lkn shingo bado ngumu. Mnatumia nguvu nyingi kumtafuta Mungu kwa njia ya ufinyu wa mawazo na hamtamwona kamwe. Lkn wanao mtii wanamwona kila iitwapo leo.
 
Usiwe unakurupuka kujibu tafakari swali kwa umakini then ujibu. Umefikiri kwenye dunia hujafikiri nje ya dunia hii au na huko Ni kwa kufikirika pia?
Nje ya dunia ni mpangilio wa sayari nyingine hana cha mbingu wala nini
 
Sijasema Kuna mbingu hapana nilikuwa namaana yangu kumuuliza vile bahati mbaya hakujibu
 
Hii tunaita myth...mwisho wako wa dunia ni siku utakapokata moto tukuimbie parapanda na kula wali maharage
Hivi Ni nani mtunzi wa maneno malaika, kuzimu, peponi, edeni nk. Na maneno haya kuwa maarufu hivi? Dhambi, amri za Mungu, kuungama, nk. Bila Shaka yupo penda usipende
 
Hivi Ni nani mtunzi wa maneno malaika, kuzimu, peponi, edeni nk. Na maneno haya kuwa maarufu hivi? Dhambi, amri za Mungu, kuungama, nk. Bila Shaka yupo penda usipende
Ni script tu kama mama aliyoigiza royal tour
 
Back
Top Bottom