Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Huyo Mungu aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kukataa uwepo wake?Kukataa uwepo wa Mungu ni ugonjwa wa akili na kiburi kilichoshindikana.
Thibitisha uwepo wa huyo Mungu na si mawazo yako ya kufikirika tu.Akili kushindwa kujua Mungu ni nani, ni nini, alitoka wapi, anafanana je, aliumbaje ulimwengu - haimaanishi kuwa hayupo -
Au kufosi imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.
Huyo Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.ujinga sio sababu ya kukataa ukweli. Binadamu tutahangaika sana, tutajitutumua sana, tutaamini sana hizo bongo zetu ambazo mwisho wa siku zitaoza..lkn ndani mwetu kila mtu anajua Mungu yupo. Hata kitendo cha kuanza kupata mawazo kinzani kuwa yupo au hayupo ujue tayari yupo...asingekuwepo pasingekuwa na mawazo ya kujustfy kutokuwepo kwake.
Kila mtu angejua kwa uhakika na uthibitisho kabisa kwamba kuna Mungu.
Wala tusinge hitaji imani ya kujua uwepo wa huyo Mungu.
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua kwa uhakika na uthibitisho kabisa Mungu yupo?
Kama hiyo nguo nyeupe ipo na inaonekana kabisa ipo, Wala haihitajiki maswali ya kuanza kuhoji rangi yake.Mtu huwezi ukaanza kudebate whether nguo ni nyeupe wakati unaona kabisa na nyeupe...watu mtaanza kubishana nguo ni nyeupe sababu wote hamjui rangi nyeupe ni ipi au hiyo rangi mnayoibishia hamuielewi na hakuna mtu abayeijua..room ya ubishi inaanza pamoja na kuweka misimamo ya kujitia matumaini.
Maana tayari kila mtu anaiona kwa uthibitisho na uhakika kabisa kwamba kuna nguo nyeupe.
Huyo Mungu hayupo, ndio maana kuna maswali ya kuhoji uwepo wake.
Na wewe unayedai huyo Mungu yupo, Utoe uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.
Ili utu prove wrong sisi ambao tunasema hayupo.
Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayedai yupo, Ni kwamba hayupo.
Na madai yako ya uwepo wa huyo Mungu ni madai ya UONGO na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.