Pre GE2025 Wasira awatetemesha akina Tundu Lissu na Wenzake: "Kauli Mbiu ya "No Reform, No Election" Haina Maana Kwa Sasa"

Pre GE2025 Wasira awatetemesha akina Tundu Lissu na Wenzake: "Kauli Mbiu ya "No Reform, No Election" Haina Maana Kwa Sasa"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election" haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
View attachment 3213528
Akizungumza leo, Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira alieleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, CHADEMA wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.

"Kauli ya 'No Reform, No Election' haina nafasi kwa sasa. Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wameonyesha utayari wa mazungumzo, na bunge linakaribia kuvunjwa, hivyo hakuna muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria yanayohitaji muda mrefu," alisema Wasira.

Aliongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio.

Wasira aliwataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu. "Ni muhimu kushiriki uchaguzi na kuwa sehemu ya demokrasia badala ya kupoteza muda na kauli ambazo hazina tija kwa wananchi," alisisitiza.
Uzi wa hovyo sana huu mkuu!panda kama hausomi Duri ya nini kinaendelea!

Jiulize nani kalinda demokrasia ya chadema Hadi kufanikisha Lisu anashinda dhidi ya mapesa na suti nyeusi upande wa mama na Mbowe!!?

Ukiweza ku decode hapo utajua mission inayoendelea Kwa sasa ambayo ni Katiba mpya kaboa ya uchaguzi la sivyo 1.Tunarudi chimwaga kuteua mpya mgombea 2.upinzani unashika 3.mgombea mwenza alieteuliwa anaula utia nia!!
 
Lissu sasa aachie hiyo nyumba Oysterbay na arudishe watoto st kayumba ili twende sawa…
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election"
haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
View attachment 3213528
Akizungumza leo, Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira alieleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, CHADEMA wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.

"Kauli ya 'No Reform, No Election' haina nafasi kwa sasa. Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wameonyesha utayari wa mazungumzo, na bunge linakaribia kuvunjwa, hivyo hakuna muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria yanayohitaji muda mrefu," alisema Wasira.

Aliongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio.

Wasira aliwataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu. "Ni muhimu kushiriki uchaguzi na kuwa sehemu ya demokrasia badala ya kupoteza muda na kauli ambazo hazina tija kwa wananchi," alisisitiza.
 
Shhhhh, nyamazeni makamu kapumzika please
118a8d88-45a7-4037-a60a-c352fe3e1a90.jpeg
 
Kifungu cha 10 . 1 C cha Sheria ya Tume huru ya uchaguzi ya mwaka 2024, ndicho kilichoipa Tume jukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji Tanganyika.
Tuambie sasa Sheria iliyotungwa na bunge ni ipi? Inayohusu uchaguzi wa serikali za mitaa

1737829850978.png
 
Takwa la kikatiba sio la chadema ni la dola iliyompa mama urais!!na aliambiwa atekeleze mchakato wake tangu 2022!!kwakua hajatekeleza ni too late kwake hata ule mtandao was Tanzania leaks una sapot hii kitu kwamba hatoboi oktoba!!

Sio takwa la Lisu na chadema!na mzee wasira katolewa kafara kupinga mchakato was katiba mpya na time huru!!Mzee kaingizwa mkenge na ameshindwa kuchagua maneno ya kusema!!

Namuonea huruma wasira!!

Tujifunze kufuata maelekezo ya dola !urais ni taaasisi sio mtu!
Ibara ipi unayoiongelea ya Katiba ya JMT?
 
Uzi wa hovyo sana huu mkuu!panda kama hausomi Duri ya nini kinaendelea!

Jiulize nani kalinda demokrasia ya chadema Hadi kufanikisha Lisu anashinda dhidi ya mapesa na suti nyeusi upande wa mama na Mbowe!!?

Ukiweza ku decode hapo utajua mission inayoendelea Kwa sasa ambayo ni Katiba mpya kaboa ya uchaguzi la sivyo 1.Tunarudi chimwaga kuteua mpya mgombea 2.upinzani unashika 3.mgombea mwenza alieteuliwa anaula utia nia!!
Wenye akili Timamu tu ndio watauelewa uzi huu
 
..Ndio nimekwambia Raisi/Bunge/CCM wamefanya makusudi kutokutekeleza hicho kifungu ulichopigia mstari ili kuwezesha Ofisi ya Raisi[ Mwenyekiti wa CCM ] kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa.
Acha kuruka ruka. Weka hapa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Acha kupotosha umma kwa maslah ya Lissu 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
..Ndio nimekwambia Raisi/Bunge/CCM wamefanya makusudi kutokutekeleza hicho kifungu ulichopigia mstari ili kuwezesha Ofisi ya Raisi[ Mwenyekiti wa CCM ] kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hii hapa Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za mitaa. Ambayo wewe hutaki kuisoma

1737832512016.png

Hii hapa Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za mitaa. Ambayo wewe hutaki kuisoma

View attachment 3214010

..Raisi hataki kuandika sheria itakayowezesha Tume Huru kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

..Raisi hataki kuteua Makamishna wa Tume Huru ili wapitie usaili, badala yake anataka kuendelea na makamishna wa tume ya zamani.

..Raisi analazimisha Wakurugenzi waruhusiwe kusimamia uchaguzi ili kupata upenyo wa kuiba na kuharibu uchaguzi.
 
..CCM mmeshauriwa kuhusu Tume Huru toka mwaka 1991 wakati Jaji Mkuu Francis Nyalali alipowasilisha taarifa ya Tume ya vyama vingi.

..Tangu Mama Samia aingie madarakani amekuwa akitahadharishwa, akishauriwa, akililiwa, akibembelezwa, ili arekebishe Tume ya Uchaguzi.

..Sasa leo hii Makamu wa Mwenyekiti wa CCM akijitokeza na kusema hakuna muda wa kurekebisha Tume hakuna anayeweza kumtilia maanani. Wenye akili timamu wataona kwamba Mzee Wassira analeta dharau, na kiburi.
Huyo ni kiburi na dharau tu.
 
Unajua watoto wa Wasira, Kinana nk walipo? Nitajie mmoja anayefanya kazi tz.

Watanzania bana ni watu wa ajabu sana, naita ni special specie yani, huwezi kupata akili za hivi dunia nzima, ndio maana tunasindikiza tu. Yani ccm ilishagaona tupo bado kwenye evolution ndio maana inafanya inavyotaka na wanajua kila kitu na opposite yake sisi tutasifia tu, eti mtoa mada ananiuliza umri wangu ili tu kujustify haya madudu, mkongwe huyu kuwa mpya mwaka 2025 kuliko kizazi chote cha 70s, 80s na 90s cha ccm. Eti kizazi cha AI mnaleta hii midudu ambayo haijui hata kucompose email!

Wasira nimeanza kumsikia nikiwa chipukizi wa chama miaka ya mwisho ya 70, akiwa ndani ya mfumo, kimsingi ni ana mchango mkubwa sana kutufikisha hapa tulipo, then leo kateuliwa eti "atatetemesha mtu" huyu huyu?

Kwamba ccm ikiteua mtu basi waimba mapambio wanakuja kujaza server hapa kwa misifa kama vile kaja mtu kutoka "sayari" ingine kaleta miujiza sasa, na kwamba tutegemee mambo ya kasi na viwango, si ajabu ndio maana tumesikia wanapima shirika lao mfu la ndege kwa performance za makampuni mengine, badala ya "revenue na profits" wabongo tunahesabu wazungu walioletwa na Air France, KLM, Swiss, Lufthansa etc.

Ni nini kipya wasira atakuja nacho zaidi ya ucngz? Kwenye vikao mtampa energy drink ili awe alive? Eti mtu mzima msomi (I presume kwa kuwa yupo jf though) anauliza Lissu ana mchango gani kwa taifa? Kwani lini alikuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi? Kaanza uenyekiti juzi tu hapa watu wanaugua matumbo! Kwa level yake kama mpinzani na mwanasheria kafanya vitu tangible vingi tu na hata ukideny na kukwepa ukweli utabaki unaujua na unaimba hapa ili ukumbukwe, tunawajua wengi tu hapa mlichonga na mkakumbukuwa.

Ukitaka compare na contrast Lissu against wasira kwe kugoogle tu, wasira zaidi ya kuwa kwenye mfumo wa kushiba nini tangible unaweza kusema kafanya? Zaidi ni mwanasiasa wa ajira tu akikosa kazi ccm au serikalini anatafuta maslahi popote tu kama waganga njaa wengine. Kama ambavyo alikosa kazi akaenda kuomba kazi NCCR Mageuzi wakati kijana venus upo nursery school.

Lissu hakutetemeshwa na wanadiplomasia mahiri kama kina Mkapa na waliotangulia aje kutetemeshwa na hiki chuma chakavu? You are doomed sister! Ni simba yule, mama kamkubali anatetemeka yeye
 
Si ndio ukafanye sasa?

Ni very sad when smart people sit here na ku undermine power of state machinery of oppression ccm has on its disposal

you cant undermine that

the question is,how do you mitigate them na kumbuka they have real effects like deaths?

una watu wa kutoa kafara wauwawe?HUNA

Kenya wapo,sio TZ!

Reality ni kwamba,Lissu and his bunch of lunatics will have to seat down with ccm and talk things out with no conditions whatsoever!

watarudi njia ile ile ya Mbowe
Umerudi pale ale et ku seat bila conditions .mm ndo maana wanangu nimeruhusu wabadili uraia tu
 
..Raisi hataki kuandika sheria itakayowezesha Tume Huru kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

..Raisi hataki kuteua Makamishna wa Tume Huru ili wapitie usaili, badala yake anataka kuendelea na makamishna wa tume ya zamani.

..Raisi analazimisha Wakurugenzi waruhusiwe kusimamia uchaguzi ili kupata upenyo wa kuiba na kuharibu uchaguzi.
Kwani sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa haipo?
 
Kwani sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa haipo?

..Bunge limeelekeza iandikwe upya ili kuwezesha Tume Huru kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

..kwasababu Mama Abduli alilenga kuiba uchaguzi wa serikali za mitaa ndio maana maelekezo ya Bunge hayajatekelezwa.
 
..asante.

..lakini hebu jipime kama kauli zako zinalikatisha tamaa, au zinalipa uhalali, genge la mauwaji.

..pima kama kwa kauli zako unaonekana kukwera zaidi na Lissu, au unakerwa na genge la wauwaji.
Nauzika zaidi na muonevu government,Tena sana!

Nataka njia za kweli na practical kufanikisha hili si kutujaza upepo

Shida ni Lissu anapotudanganya as if sisi ni watoto wadogo

Ametuaminisha yeye ndio muarobaini wa huu uonevu tukampa status ya Mesiah,cha ajabu anakuja na hizi alinacha ambazo tushazisikia na kujaribu huko nyuma

Akae chini afikirie practical way to get around CCM and its machinery to promised land,na awe mkweli asife kitu

Aache kutudanganya na kutupotezea muda

Muongo tu,sana sana kutokana na ujanja finyu wake atapelekea hadi ACT ku-collude na CCM kutupita kua chama kikuu rasmi nchini maana anampa CCM option,hapo we will be officially burried!

Haoni hata hili kabisa!
 
Back
Top Bottom