RESILIENT KATO
JF-Expert Member
- Aug 21, 2024
- 1,472
- 2,766
Uzi wa hovyo sana huu mkuu!panda kama hausomi Duri ya nini kinaendelea!Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election" haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
View attachment 3213528
Akizungumza leo, Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira alieleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, CHADEMA wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.
"Kauli ya 'No Reform, No Election' haina nafasi kwa sasa. Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wameonyesha utayari wa mazungumzo, na bunge linakaribia kuvunjwa, hivyo hakuna muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria yanayohitaji muda mrefu," alisema Wasira.
Aliongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio.
Wasira aliwataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu. "Ni muhimu kushiriki uchaguzi na kuwa sehemu ya demokrasia badala ya kupoteza muda na kauli ambazo hazina tija kwa wananchi," alisisitiza.
Jiulize nani kalinda demokrasia ya chadema Hadi kufanikisha Lisu anashinda dhidi ya mapesa na suti nyeusi upande wa mama na Mbowe!!?
Ukiweza ku decode hapo utajua mission inayoendelea Kwa sasa ambayo ni Katiba mpya kaboa ya uchaguzi la sivyo 1.Tunarudi chimwaga kuteua mpya mgombea 2.upinzani unashika 3.mgombea mwenza alieteuliwa anaula utia nia!!