Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Wengine wako kazini hao mkuu
 
Hizi kasumba ndo zinashusha hadhi ya elimu.

Halafu chunguza Mara nyingi Hawa wasio na sifa za kuajiriwa, kwa kukosa vigezo ndo wanakimbilia kuinajisi Elimu. Unakuta mtu kweli kamaliza chuo na Ana degree Sawa, lakn Sasa ufaulu wake (GPA) alipata ndo unamkwamisha kupata Ajira, matokeo yake ndo anakimbilia huku na kujinadi kuwa yeye kasoma lakini amejiajiri, kumbe ukweli anaujua mwenyewe.

Mwisho wa siku usishangae mwanao akakwambia sitaki kusoma, naomba uninunulie Boxer nipige kazi. Je wewe kama mzazi mwenye malengo utakubali?.

We unafikiri mzazi wake aliemsomesha elimu ya Awali angejua kama anakuja kuendesha Bajaji angekubali kulipia Ada yote hiyo hadi kufika kuendesha Bajaji. HIYO SIO SIFA. Angalau angekuwa mwanaume.

Kwanza si kazi ya kujivunia maana Ana Risk, maana ni mtoto wa kike anashawishi kuibiwa Bajaji au kubakwa, Na pia anytym anaweza kupata ajali, akatekwa au kuvamiwa na wahalifu. halafu Hao watoto Wataangaliwa na nani, na yeye ndo mama.

Sio kila jambo la kuunga mkono, mengine ni ya kushauri au ikiwezekana kupinga kabisa. Anapaswa ajitafakari, kwanza yeye anaona sifa kupata publicity huyo kwenye magaazeti, kumbe ndo amewapa watu fursa ya kumtafuta, maana hata walikua hawamjui.

Ni kheri hata angeenda kuuza chakula, matunda au juice. Lah, kama Anapenda mambo ya usafirishaji ni kheri angekuwa Dereva wa maroli au konda wa maBus ya mikoani, Risk yake sio kubwa kama hiyo kazi.

We Ngoja tutakuja kuskia mwisho wa hiyo kazi yake kama utakuwa wa kheri .
 

Ngoja wengine wapitie maoni yako !
CC:
The Happiness
madam cute
Lady nancy
my girl
Aunt Cash
BAK
Numbisa
 
sasa ajira atakayoomba ni ya kudumu...biashara ina kitu kinachoitwa exist strategy kila unapoingia...na hii ni rahisi sana...ukipata fungu flani unaiuza biashara unafanya nyingine ni vigumu kudumu na wateja miaka mitano...watu wanakuwa wanabadili marafiki na life style wengine wanatajirika wananunua vyombo vyao....simshaurikutafuta kazi ya kuajiriwa asonge mbele...
 
Makjuisi je
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Hata hivyo, viwango/aina ya kuiajiri haviwezi kufanana. Wengine wanajiajiri pakubwa wengine padogo. Jambo la muhimu anapata kipato ambacho hakitokani na mshahara.
 
Utopolo mtupu.
Hivi unajua kuwa kuna kazi zingine za serikali matangazo yake huishia ofisini ndani kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa Wilaya na ndani ofisi ya mkuu wa kitengo mkoa au wilaya?
Na ifahamike wengine huajiriwa na hawakai ofisini.
Kuna mama muuza mihogo barabarani VETA dar , yule mama ile kazi ya kuzurura juani haitegemei, yupo pale kwa mission.
Kama hadi wengine hujifanya machizi ili wapate info mtaani unakuja kushangaa huyo dada na shahada zake 2 kudrive bajaji?
Unamjua mmiliki wa hiyo baiaji?.
Kabla hamjaja juu kuhusu habari za mtu yeyote tafuteni nature yake mtajua ukweli.
 
Angeenda veta
 
Umenasa kwenye propaganda za ujamaa enzi zile kwamba, kila watu 10 basi mmoja au wawili kutoka kitengo. Kwenye maelezo yake amepata Bajaji kwa mkopo wa CRDB kama ilivyo makampuni yanayokopesha na unalipa kwa wiki au mwezi na chombo kinakuwa chako.
 
Tungekuwa tunajua future zetu wengi tusingehangaika na Chuo Kikuu. Usomee uhandisi hadi upate degree halafu uiweke pembeni uanze kilimo cha matikiti?? 5 good years wasted!!! Bora mtu ungejua mapemaaaaa na kuanza mara tu baada ya kumaliza form 6
 
Tungekuwa tunajua future zetu wengi tusingehangaika na Chuo Kikuu. Usomee uhandisi hadi upate degree halafu uiweke pembeni uanze kuliko cha matikiti?? 5 good years wasted!!! Bora mtu ungejua mapemaaaaa na kuanza mara tu baada ya kumaliza form 6

Sio mzigo kwa mtu tuu.. serikali nayo inapoteza kumsomesha mtu asiwe productive baadae.... hela iliyotumika kumsomesha mtu huyu ingetumika eneo lingine labda ingekua na faida maradufu, we all lose, sisi na serikali pia.... tatizo tukiwashauri humu wanajifanya hawaoni.
 
Kuwa na masters si ishu kubwa. Ulicho nacho kichwani baada ya masomo ndio habari kamili.
Sasa huyu dada na masters alikuwa analipwa chini ya laki 4 na institution gani hiyo?
Pengine hiyo masters yake ni cheti tu ila yuko empty!
Some people are not meant for greatness, the universe serves what's best for the kind of person you are.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…