Wassira: Mkapa alikopa trillion 23, Jakaya alikopa trillion 20, Magufuli alikopa trillion 29

Wassira: Mkapa alikopa trillion 23, Jakaya alikopa trillion 20, Magufuli alikopa trillion 29

Dr Mwinyi Rais wa Zanzibar atakopa lini ili naye agawie mkopo kwa Bara, ili tuweze kuenzi Muungano?
 
Kila mwaka tunalipa trillion 10 kupunguza deni lakini tangu Magufuli alipoingia madarakani deni limekuwa likipaa!
Miaka yote deni linapaa halijawahi kushuka ila kipindi kile tulipofutiwa baadhi ya madeni.
 
Mzee Wasira yupo Star TV Hivi sasa katika kipindi cha the Big Agenda anasema kwa miaka 10 kila mmoja cha Mkapa na Jakaya walikopa trillion 23 na 20 mtawalia.

Magufuli kwa miaka 5 alikopa trillion 29.
hivi ile sheria ya takwimu iliishafutwa?
 
Mzee Wasira yupo Star TV Hivi sasa katika kipindi cha the Big Agenda anasema kwa miaka 10 kila mmoja cha Mkapa na Jakaya walikopa trillion 23 na 20 mtawalia.

Magufuli kwa miaka 5 alikopa trillion 29.
Duuh!
Afu tukawa tanapangwa kuwa zinazotumika ni fedha za makusanyo ya ndani 🙄
 
Who the hell ameleta haya mambo ya kijinga na wanasiasa nguli wanajiingiza katika mtego wasioelewa...huyo mkapa,kikwete na magufuli walikopa kupeleka fedha mifukoni mwao?tunaingia katika mijadala feki ambayo haina msaada wowote...serikali ni moja na inakopa kama serikali.Kwani awamu hazikukopa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya awamu zilizopita?kwa hiyo Mama anapokopa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya kimkakati utasema amekopa yeye?au mnataka asite kukopa miradi isimame?Kitu muhimu cha kujadili ni kuibua kama ipo mikopo ambayo imechukuliwa ambayo haina tija kwa nchi.CCM wanaingia kwenye mtego ili mama akwame.Ni ukweli kabisa ili kukamilisha miradi mkakati yote iliyopo na mingine mipya awamu ya sita lazima itakopa zaidi kuliko awamu nyingine zote kama ambavyo itaongoza kwa kuwa na miradi mikubwa mingi ya kimkakati na mahitaji ya ilani ya ccm.
 
Mfano mradi wa DRT, mbagala ulisimama kabisa, na mwaka huu ulikuwa ukabidhiwe, yule DC wa tmk, Gondwe alikuwa kila mala anakwenda anapigwa mkwara wapi eti mbona kazi haiendi, wao wanasema pesa hakuna, waki issue certificate, hakuna pesa, nenda sasa hivi ukaone kazi inavyokimbia, hiyo sgr kawaulize ma sub contractor walikuwa na hali gani, hadi ma bank yaliwakataa!!kulikuwa na kampuni la kireno pale, kaulizie lilienda wapi?hiyo barabara ya morogoro,
USA, mwenyewe anazingatia bajeti , wewe KIDUDU MTU, hutaki kufuata utaratibu kwa kuendesha nchi, unaendesha kwa mizuka tu, lazima u fail tu, Cha ajabu jana Ndugai ndio ana kili kuwa serikali ilikuwa inaendeshwa ki ugumu sana, kwani pesa iliyotengwa huku inapelekwa kule, mwaka wa fedha unaisha wizara imepata 16% ya bajeti yake iliyotengwa, halafu unakuja kumlaumu waziri!!kutokana na kila leo kuja na mambo ambayo hayako kwenye bajeti.
Wewe bana. Nchi haijengwi lwa siku moja.

Kila kitu kinaenda kimpango. Ujenzi unaweza ukaipanga sasa hivi hafu pesa ikaingia badae.
Uzuri unajua kabisa kwamba; Mzee alikufa akiwa anakabidhi miradi iliyokuwa imekamilika kwa asimia kubwa.. mfano.. Ubungo, Mbezi na Kisutu. Barabara ya Morogoro ilikuwa hatua nzuri. Miradi ya Maji ndo usiseme. REA, sasa hivi tumebaki na SGR na bwawa la nyerere tu na kele ni nyingi sana.

Usiwasikilize sana wanasiasa wanalinda tonge. Ndugai wa kusikiliza ni aliyezungumza mara ya kwanza maana alikuwa yeye kama yeye; Yule Ndugai wa jana likuwa kwenye mbano wa hari ya juu.
 
Lakini Magufuli alituambia anajenga uchumi kwa pesa za ndani na sio mikopo ya pesa za mabeberu.
Kwa kiingereza imperialist organs....IMF and WB ..mikopo yenye masharti...Ukienda bank ya maendeleo ya Afrika unakopa kama mteja tu kwa kuaminika utarejesha.Hupangiwi matumizi ya hiyo fedha.Kuna miradi kama wa umeme wazungu hawawezi kukukopesha fedha kulinda maslahi ya makampuni yao ya kuuza umeme na gesi...
 
Serikali ya mapinduzi Zanzibar ni sawa tu na serikali ya mtaa! Tofauti ni ukubwa wa eneo na kupewa mamlaka ya ndani!

04EF2C4A-F2F1-4DDB-8175-AC55D3F5C59F.jpeg
 
Wewe bana. Nchi haijengwi lwa siku moja.

Kila kitu kinaenda kimpango. Ujenzi unaweza ukaipanga sasa hivi hafu pesa ikaingia badae.
Uzuri unajua kabisa kwamba; Mzee alikufa akiwa anakabidhi miradi iliyokuwa imekamilika kwa asimia kubwa.. mfano.. Ubungo, Mbezi na Kisutu. Barabara ya Morogoro ilikuwa hatua nzuri. Miradi ya Maji ndo usiseme. REA, sasa hivi tumebaki na SGR na bwawa la nyerere tu na kele ni nyingi sana.
Sasa kama miaka 5, tu amekopa karibia trilioni 30, hata kama angemaliza muda wake cjui miaka 15 mbele, kwa mwenendo huo nchi isingekuwa ina kopesheka tena!ndio maana huwa ina sisitizwa utaratibu wa CASH BURGET, miradi yote ipo kwenye hatua tofauti tofwuti, ila hilo la bwana na SGR, ndiko kuna balaaa!!
Uamuzi wa kujenga reli ya umeme kwa umbali huo, hilo ni jini ambalo litawasumbua sana viongozi wanaokuja hata mama hata limaliza na yeye atamuachia mwingine!!kwani sio kazi ndogo ifike mwanza, kigoma , katavi, congo, Rwanda, burundi hahaaa!!!
 
Back
Top Bottom