Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

hivi ubongo mnakuwaga mmepeleka wapi aisee? unajaribu train, mabehewa na kichwa chenyewe umeagiza nje kwa garama kubwa sana, halafu unataka mtu aende speed yote, vikidondoka? hivi maana ya majaribio mnaijua?
 
Mi nimefurahi sana kutumia masaa mawili kwenda moro maana Kwa basi ni zaidi ya masaa 3 mpaka manne. Pia Ile Raha ya treni kuzunguka kwenda kwenye mgahawaha na nafasi kubwa ni bonge la advantage
sio hiyo tu, train unaweza kufungua laptop yako ukaifanya kazi ndani ya masaa hayo 2 na nusu, unaposhuka ushapunguza mzigo tofauti na basi huwezi kufungua laptop ukafanya kazi kwa raha.
 
ndugu, wewe ungetupatia experience yako ni ya wapi, treni unazozijua ulizozipanda ni za wapi ili tujue kama wewe ni wa lupaso au wa mbele. pili, kuweka wahudumu ndio ajira hiyo, dada zetu wanapata ajira, unataka wakale wapi?
 
Kwani umbali wa Dar hadi Morogoro ni kilomita ngapi? Kama treni ingekuwa imekwenda 160 km/h isingechukua hayo masaa 2 na dakika 20 (kama ni kweli ilichukua muda huo).
umbali wa reli au barabara? hapo ndipo mnapochanganya. pili, kama basi linachukua masaa 3.5 hadi moro, treni ikichukua 2.20 si mshukuru? hata hapo mnashindwa kujipongeza kweli?
 
nimepanda treni mara nyingi sana nchi za mbele, tena zenye speed kama hii ya kwetu 160kmh. though zipo hadi zenye 300kmh lakini kama hii ya kwetu zipo. wengi wanaojadili hapa, ndio wanaanza kuiona treni ya aina hii leo na wanaongea kwelikweli.
Hivi wewe unajua high speed bullet [emoji583] train? [emoji848] Kwan huko nje haujawahi kuziona?

Kwahiyo unataka kutuambia kuwa sisi hatujui tunachokisema?

Miaka ya ujuaji sababu umesafiri nje ya inchi ukajiona unajua kushinda ambao hawajasafiri mwisho ilikuwa ni kipindi hakuna internet.

Saa hii internet inakupa kila aina ya taarifa hakuna story ambayo utaongea kusiwe na ushahidi wake mtandaoni.

So kuwa makini sana na swala la kuhisi una exposure kuwashinda watu wote.
 
shida ndio inaanzia hapo, tupo sisi wengine ambao tumeishi na huo ndio umekuwa usafiri wetu kwa miaka mingi tu, na mpo ninyi kama wewe ambao mnajifunzia kwenye internet. ndio maana mnaongea ujinga mtupu. hizo treni zipo za speed tofauti hata huko ulaya, chukua mfano tu Ujerumani, Ufaransa, Italia ambako ni nchi kubwa kubwa na zina usafiri huo sana, zipo treni zinaanzia 155kmh, na zipo zingine zimefika hadi 300kmh. yaani kwa lugha nyingine, hii aina ya treni tuliyonayo sisi hapa hata ulaya zipo na bado zinatumika kwenye SGR zao. sasa shida ni pale mnataka watuletee 300kmh train wakati hata hiyo ya speed ndogo hamjawahi kuwa nayo. kwani shida ni nini? kama tayari miundombinu ya reli mmeshajenga, si jambo la kununua tu za speed mnayotaka? hiyo reli ni barabara ya train kama hujui, za speed zote zitapita kama mtakuwa na hela kununua za speed hizo. kwahiyo kwenye barabara la lami toka dsm hadi moro ikipita lori la speed 80kmh haiwezi pitisha V8 la speed 200kmh?
 
Mi nimefurahi sana kutumia masaa mawili kwenda moro maana Kwa basi ni zaidi ya masaa 3 mpaka manne. Pia Ile Raha ya treni kuzunguka kwenda kwenye mgahawaha na nafasi kubwa ni bonge la advantage
Sawa hatujakataa huduma nzuri ila wasiifananishe na Bullet trains zile tunazojua sababu zile zinaweza ifanya hiyo kazi kwa dakika 70+ baaasi.
 
Na treni za kwenda kwenu Tarime zinatumia mda gani?
 
Umesoma msg yangu vizuri? SGR imeenda 2hrs juzi. Nitajie bus linaloenda Dar-Moro 2hrs hivi karibuni. Dar Moro kwa gari sasa hivi ukijitahidi sana masaa manne.
 
Umesoma msg yangu vizuri? SGR imeenda 2hrs juzi. Nitajie bus linaloenda Dar-Moro 2hrs hivi karibuni. Dar Moro kwa gari sasa hivi ukijitahidi sana masaa manne.
Abood driver Othman tochi analipa Tajiri dadeki 😂

Wanaliita bus la Wafanyakazi

Vyuma vya usiku karibia Vyote Mora saa 2 tu
 
HAlafu mwaka 2022 si walifanya Majaribio ikakimbia kwa 175 Km/Hour
 
Sio kwa kichwa kile cha treni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…