Wataalamu wa Dini tusaidieni kwenye dhambi ya kuzini

Wataalamu wa Dini tusaidieni kwenye dhambi ya kuzini

Malaika hawana jinsia wala hawana hisia za kibinadamu.
Malaika hawali wala hawazaliani hawana undugu wala hawaishi kifamilia .
Malaika ni kama roboti anafanya kile alichoambiwa hana uwezo wa kukataa au kwenda tofauti.
 
Malaika hawana jinsia

Jinsia ni kwa ajili ya viumbe wanaozaliana kwa staili zetu.

Halafuuuu, kushir
Walikwambia hawana hisia? Vip mapepo na mashetan walijizaa wao? Vipi wale malaika walioanguka na waliozaa na biandamu walitumia kichwa kufanya mapenzi?

Tumieni akili na sio stori za vijiweni.

Malaika wana jinsia, viumbe vyote vina jinsia
 
Dini zote duniani zinahubiri kuwa kufanya mapenzi ni dhambi hivyobasi mwanadamu hapaswi kufanya mapenzi na mwanadamu mwezake.
Mwanaume kuwa karibu na mwanamke au kujenga urafiki imekua ikiibua maswali mengi kwa watazamaji.

Kwahiyo swala la jinsia limekuwa likitafsiriwa vibaya sasa tuelezeni kwanini kuna Malaika wa Kiume na Wakike? Kwanini wakawa wa Kiume na Wakike?

Kwanini wasingekuwa jinsia moja kama jinsia haina maana kubwa kama mnavyotudanganya kwamba wanaume tusikutane na wanawake wala wanawake wasikutane na wanaume?

Fanya Uchunguzi Kabla hujaleta Uzi
1.Hakuna Sehemu duniani Inayohuburi Kufanya Mapenzi Ni dhambi Bali Kufanya Ngono Ndio Dhambi.Mke na Mume Hawawezi Fanya ngono Bali Wanafanya mapenzi,Kufanya mapenzi Ni Kwa ajili Ya Wapenzi Halali Waliothibitishwa.

2.Mwanaume Kuwa karibu Na Mwanamke Kunaibua Maswali endapo Uhusiano Wao Ukiwa Hasi.
Haujakatazwa au hatujakatazwa au Sio Vibaya Kuwa Na Uhusiano wa karibu na mwanamke Ila uhusiano wenu Uwe chanya.

3.Jinsia Ya Malaika Hiyo Ni elimu Ya Kiroho(vitu Vya Kusadikika),Kwa sisi wenye Imani Tunaamini wapo Na Kulingana Na Vitabu Malaika Hana Jinsia,Ameumbwa awe Malaika tu,
Jinsia Ni kwa ajili ya Viumbe Visivyo vya Kusadikika Tunavoviona Kwa Macho au tuna ushahidi Navyo.
 
Na pia wana wa kweli wa Mungu waliwatamani wana wa binadamu na kuja kuwafanya wake zao
Swali kumbe pia malaika wana tamaa kingono?
 
mkuu wapi umejifunza kuwa mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa ?

Soma hapo Marko 20:34-36.
Watoto/Wana wa Mungu ni wapi? Soma hapo Yohana 1:12

Kwa nyongeza soma hapo Mathayo 22:30. Na kwa faida yako unaweza kuendelea mpaka mwisho mstari wa 46 ili ujue Uungu wa Bwana Yesu kuwa alikuwa ni Mungu kweli na Mwanadamu kweli ambaye hakuwahi kufanya dhambi.
 
Soma mwanzo 6:1-3 alafu uje kunielewesha mkuu

Haya ni maoni yangu kwa jinsi nilivyo elewa.
Hawa wana wa Mungu wanaotajwa hapo ni malaika walio anguka kwa dhambi ya kutamani mabinti wa wanadamu wazuri. Hivyo basi walivyaa viwiliwili vya uwabadamu wa jinsia ya kiume huu ni ushahidi mwengine kuwa Malaika ni me.

Hata pale bustani ya eden shetani lucifer alipokuja kuwa jaribu Adamu na Hawa alivyaa umbile la nyoka.
 
Dini zote duniani zinahubiri kuwa kufanya mapenzi ni dhambi hivyobasi mwanadamu hapaswi kufanya mapenzi na mwanadamu mwezake.
Mwanaume kuwa karibu na mwanamke au kujenga urafiki imekua ikiibua maswali mengi kwa watazamaji.

Kwahiyo swala la jinsia limekuwa likitafsiriwa vibaya sasa tuelezeni kwanini kuna Malaika wa Kiume na Wakike? Kwanini wakawa wa Kiume na Wakike?

Kwanini wasingekuwa jinsia moja kama jinsia haina maana kubwa kama mnavyotudanganya kwamba wanaume tusikutane na wanawake wala wanawake wasikutane na wanaume?
Hizi sheria zilikuwa na maana binadamu alivyoishi kwenye makabila na sehemu zenye scarcity of resources na ukosefu wa elimu ya minba na magonjwa ya zinaa. Now tupo 21st century, kuzuia mimba unaweza both naturally and artificially, unaweza zuia magonjwa, na mengi yanatiba au Kinga, unaweza zaa mtoto akasurvive mda mrefu kwa sababu ya huduma Bora za ulinzi, afya, chakula, maji na elimu.
Inabidi watu wakue na kuelewa kwamba dini zilianza wakati binadamu alikuwa mchanga katika ukuaji wa maisha, maadili, maarifa na maendeleo so haina maana kuishi Kama mababu wa miaka 3000 iliyopita ambao walijua usiku jua linazama kwenye tope.
 
Kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa tena?
Au ndio mimi sijaelewa?
Mume na mke wanafanya tendo la ndoa,
Mwanaume na mwanamke ikiwa hawajafunga ndoa hapo wanakuwa wanazini/wanafanya uasherati/wanafanya ngono/wanazagamuana/wanadegana/wananyanduana nq miaemo mingine mingi,
Ila kukiwa na ndoa tuu hakuna jina jengine zaidi ya tendo la ndoa,
Hata kujamiiana sio kwa waliooana kwasababau hata wasiooana wanajamiiana,
Lakini waliooana tuu ndio wanafanya tendo la ndoa,
😂 Inaitwa don't sex until you sign a lifetime exclusivity contract and a ceremony with ur friends and family...🤣Ila dini ni kitu Cha kuchekesha...na watu wapo serious wanaamini
 
Back
Top Bottom