Wataalamu wa sheria: Je, ni kosa kupandisha bendera ya taifa nyumbani kwako?

Wataalamu wa sheria: Je, ni kosa kupandisha bendera ya taifa nyumbani kwako?

Hivi nikishona kwa kuviunganisha vitambaa nikatengeneza bendera yenye muundo na inayoelekea kama ya Tanzania ila sio ya Tanzania,nikapandisha nyumbani kwangu,nitakamatwa kwa kupeperusha bendera au? kwani huyo aliyekamatwa aliwaambia hizo ni bendera za Tanzania?
Nafikiri mahakamani aseme hiyo siyo bendera ya Tanzania, polisi iprove kuwa hiyo ni ya Tanzania, kama ni rangi hata ya Afrika kusini ina rangi kama zetu na ya Jamaica.

fototapety-jamaica-flag.jpg.jpg
 
Sizani kama kuna kosa hapo.
Mtu kaonyesha tu uzarendo na mapenzi ya nchi yake, anakamatwa.

Ngoja wampeleke mahakaman tuone watasema kifungu gan cha sheria kinahusika hapo.
 
Mimi nafahamu kwamba bendera ya Taifa inapeperushwa mahali palipo Serikali, ndiyo maana kwenye ofisi zote za Serikali kuanzia Bungeni, Wizarani, Halmashauri, kwenye Taasisi kwa maana ukienda TANROADS, TARURA, TAWA, EPZA n,k utakutana nazo

Lakini baadhi ya Viongozi wameruhusiwa kupeperusha bendera kwenye magari yao ya Ofisi mfano RC, Waziri, DC na kadhalika

Hiyo bendera pia utaikuta kwenye makazi rasmi ya Viongozi wa Kiserikali mfano anapoishi Waziri Mkuu, Rias, Makamu wa Rais, RC ama anapoishi Mkuu wa Wilaya

Ila kwenye makazi ama shughuli binafsi ya mtu binafsi hairuhusiwi

Kwa maelezo hayo, huyo Bwana amefanya kosa kupeperusha bendera kwenye mashamba yake ama nyumbani kwake
 
Sio kosa kupeperusha bendera ya taifa nyumbani kwako,kosa ni kuiharibu kwa namna yoyote ile kama hivyo...pia hata hivyo bado tupo nyuma sana aisee,kupeperusha bendera nyumbani kwako pia inahitaji kibali maalumu eti
 
Mimi nafahamu kwamba bendera ya Taifa inapeperushwa mahali palipo Serikali, ndiyo maana kwenye ofisi zote za Serikali kuanzia Bungeni, Wizarani, Halmashauri, kwenye Taasisi kwa maana ukienda TANROADS, TARURA, TAWA, EPZA n,k utakutana nazo

Lakini baadhi ya Viongozi wameruhusiwa kupeperusha bendera kwenye magari yao ya Ofisi mfano RC, Waziri, DC na kadhalika

Hiyo bendera pia utaikuta kwenye makazi rasmi ya Viongozi wa Kiserikali mfano anapoishi Waziri Mkuu, Rias, Makamu wa Rais, RC ama anapoishi Mkuu wa Wilaya

Ila kwenye makazi ama shughuli binafsi ya mtu binafsi hairuhusiwi

Kwa maelezo hayo, huyo Bwana amefanya kosa kupeperusha bendera kwenye mashamba yake ama nyumbani kwake
Kama kuna hiyo sheria basi imepitwa na wakati
Wengine wanataka kuonesha tu uzalendo wao na mapenzi

Ova
 
... acha tu likamatwe, yaani linawezaje kuzifanya bendera zetu 'SCARECROWS'?
... Waswahili bwana! yaani jitu lilitumie bendera zetu kufukuzia ndege shambani kwake tuliangalie tuu!!! ’ATA KAMA!
👊😅✌️
 
Back
Top Bottom