Mbona hatujaona hiyo idhini ya UAE kwenye wale signatories wala power of attorney........wamesaini wahuni wasiojulikana.
Hayo ni makubaliano ya UAE na Dubai, na mkataba mzima ni wa siri, hata huu mkataba wa IGA hukutakiwa kuuona, umeuona kwa kuvuja tu.
Emir wa Dubai ni Waziri Mkuu na Makamu wa Emir wa UAE.
Unafikiri kuna idhini ya UAE ambayo Dubai itaitaka na kukosa hapo?
UAE na Dubai wanafanya deals pamoja.
Unafikiri wale wanasheria wapigaji wa kimataifa wa DPW wataingia mkataba mkubwa kama huu bila ku clear this very obvious item?
Pelekeni mahakamani hii hoja ya "Dubai si nchi" muone itakavyotupwa.
Halafu ikitupwa mje hapa niwape pole.
Mkataba una mambo mengi ya ovyo, soma review ya TLS wameyaandika mengi, hamna haja ya kutunga mambo ambayo hayana msingi.
TLS wenyewe katika review yao wamesema hili la "Dubai si nchi" hawawezi kulisemea wanahitaji mtu aliye ndani ya mifumo ya Dubai awaeleze. Kwa sababu haya ni makubaliano ya UAE na Dubai, na makubaliano yanaenda kwa usiri, kama mkataba ulivyotakiwa uwe.
Sasa sisi tumepata kimkataba tu kwa ku leak, tushaanza ku form conclusions kuhusu mambo meengi.
Yani mnafikiri mtawakamata DPW kwa technicality ndogo hii?
Mimi mwenyewe mkataba siupendi, natamani ingekuwa that simple kuubatilisha.
Lakini, sipendi kufanya mental masturbation na kuwa na fantasy kwamba it is going to be that easy.
"Dubai si nchi, mkataba ni batili" is not going to work.