Watangazaji Clouds Media wapendekeza siku ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu ingizwe kwenye kalenda ya kusheherekea

Nyerere day tunaadhimisha siku ya kufa kwake. Huyu mh siku akifa tutakuwa tunaadhimisha sherehe zake mara 2 kwa mwaka?!
Siku ya kufa huadhimishwa moja tu kwa kiongozi wa kwanza wa Taifa (hii desturi ya mataifa mengi) viongozi wengine wakifariki siku yao ya kufa haiwekwi kwenye kalenda ya kitaifa.
 
hii nchi uhuru umezidi😉😉😉😉😉😉😉
 
Kwa kazi gani aliyofanya?
Watangazaji wa clouds Media kwa niaba ya media imependekeza siku ya kuzaliwa ya mhe Raisi Mama Samia Suluhu ingizwe kwenye calendar ya kusherekea siku ya kuzaliwa kama ilivyo Nyerere day n.k iwe sehemu ya siku ya kitaifa
 
Wewe una stress home ndio maana huzipendi sikukuu
Japan na China hawana masherehe mengi ya kijingajinga kama huku kwetu. Kila siku sherehe mara Karume day mmeweka kitako chini hakuna kazi. Sijui 88 mara 77 sijui Nyerere day. Sikukuu zingekuwa tatu tu. Uhuru, Idd na Xmas. Au tano na Maulid na pasaka.
 
Siku ya kufa huadhimishwa moja tu kwa kiongozi wa kwanza wa Taifa (hii desturi ya mataifa mengi)
Marekani mwezi huu waliadhimisha siku aliyozaliwa Martin Luther King. Hakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa lao. Unasemaje hapo!
 
Watangazaji wa clouds Media kwa niaba ya media imependekeza siku ya kuzaliwa ya mhe Raisi Mama Samia Suluhu ingizwe kwenye calendar ya kusherekea siku ya kuzaliwa kama ilivyo Nyerere day n.k iwe sehemu ya siku ya kitaifa
Wamenogewa na uteuzi.

Mpaka sasa wawili wameisha lamba ukurugenzi wa wilaya wakitokea kwenye hayo makochi matatu.
 
Wapuuz wale bas nae mam kamtaja mwijaku ndio wakamfanyia sheree siku iliyofata
 
Watangazaji wa clouds Media kwa niaba ya media imependekeza siku ya kuzaliwa ya mhe Raisi Mama Samia Suluhu ingizwe kwenye calendar ya kusherekea siku ya kuzaliwa kama ilivyo Nyerere day n.k iwe sehemu ya siku ya kitaifa
Chawa hao
 
Japan na China hawana masherehe mengi ya kijingajinga kama huku kwetu. Kila siku sherehe mara Karume day mmeweka kitako chini hakuna kazi. Sijui 88 mara 77 sijui Nyerere day. Sikukuu zingekuwa tatu tu. Uhuru, Idd na Xmas. Au tano na Maulid na pasaka.
Uko sahihi boss
 
Watangazaji wa clouds Media kwa niaba ya media imependekeza siku ya kuzaliwa ya mhe Raisi Mama Samia Suluhu ingizwe kwenye calendar ya kusherekea siku ya kuzaliwa kama ilivyo Nyerere day n.k iwe sehemu ya siku ya kitaifa

itafika sasa kuanzia januari mpaka desemba na viunga vya tarehe zote kila ukiamka ni sikukuu ya viongozi tusiende kazini
 
Marekani mwezi huu waliadhimisha siku aliyozaliwa Martin Luther King. Hakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa lao. Unasemaje hapo!
Kwani hapa hoja ni Marekani au Tanzania? MLK anapewa heshima kote ulimwenguni ni miongoni mwa watu waliopambana sana dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Mkapa alivyofariki uliambiwa kuna Mkapa day kama Nyerere day? Hutokaa uone maadhimisho ya kifo cha kiongozi mwingine hapa nchini tofauti na Nyerere.

Tukipata marais 80 ina maana kwa mwaka tutakuwa tuna siku 80 za mapumziko kisa vifo vya viongozi?
 
Watangazaji wa clouds Media kwa niaba ya media imependekeza siku ya kuzaliwa ya mhe Raisi Mama Samia Suluhu ingizwe kwenye calendar ya kusherekea siku ya kuzaliwa kama ilivyo Nyerere day n.k iwe sehemu ya siku ya kitaifa
Kituo kilichojaa wanafiki na upumbavu mwiingi.
 
Back
Top Bottom