Watangazaji waliokuwa wanamuhoji Ruto, Tanzania hatutowapata wa kiwango kile daima

BLACK MOVEMENT kila siku unalalmika kama dent tukiuliza umefanya nini kubalisha hizo changamoto unatoa matusi? Umechukua hatua gani wewe kama wewe au unataka wengine wafanye wewe uwe mpambe tu? Utakua mpambe na mlalamishi hadi lini? Huko Kenya unakokushobokea sana kuna walalamishi madent kama wewe? Either You do the work or suck it up. Change starts with you.
 
Siyo maada ni mada,maada ni yabisi,gesi na kimiminika,tuna waandishi wengi wanaweza muhoji huyo mtu wako vyema,tido mhando,Venus nyota, Charles Hilary,barwan mhuzya nk,tatizo waandishi unaowaona ni akina diva the bawse na WA michezo, pascal mayala hawezi kumuhoji huyo!?
 
Wewe mbona unalia kwenye uzi wangu?
 
Kenya wametuzidi kila kitu
 
Kuna ile interview Makamba senior anaulizwa na muandishi wa habari kwanini anasema mambo yapo vizuri hali ya kuwa mambo sivyo kama anavyosema, aisee yule mzee alipandwa na jazba akaanza kutoa na matusi, mzee wa watu sukari ilitaka kupanda.
 
Wapo wengi lakini mifumo yetu haiwaruhusu kumantain uwezo wao
 
Nimeitazama hii interview mwanzo hadi mwisho hakika waandishi wakenya wanao uhuru na wamebobea kweli kweli!

Na hakika wakenya wanaye Rais wanatakiwa tuu kumuelewa na yuko tayari kuwasililiza hakika Rutto ni humble president ever…kwakweli nimeenjoy kusikiliza na kutazama na nilitamani iendelee na hakika President Ruto alijiandaa kamili kabisa!

Wondefull interview ever …nimepende Mr president alivyokuwa ana kubali kama amekosea au kushindwa na amehitaji mjadala wa kitaifa na vijana waseme wataendesha nchi vipi?

Safi
 
Imagine Hangaya anapigwa maswali kama yale...
 
Ukiuliza maswali ya akili hukawii kuonekana wewe ni mpinzani, ona kilichomkuta Gerald Hando pale E FM.

Kingine ni ule Uchawa kwa kutegemea labda unaweza kumbukwa kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya. Hapa lazima upoteze professionalism Yako.
 
Tanzania kwanza tumekosa watu wenye upeo wa uandishi wa habari maana ni kama tumeamua media zote ziwe ni za mahoka na vituko. Hatuna hata media moja iliyokuwa serious na kureport mambo ya maana.

Wale waandishi kidogo wenye upeo, hawana uthubutu kiasi cha kufanya kila kitu kwa script inayopendeza utawala.

Tasnia ya habari ni mithili ya udaktari, ni tasnia ya wito. Ila kwa sasa Tz uandishi wa habari umekuwa kama jukwaa la watu kujionyesha ili wateuliwe. Hili limeleta athari ya waandishi kuacha kureport na kuishia kusifia.

Mwisho na muhimu zaidi ni viongozi wetu kuwa na power kubwa sana kiasi cha kujihisi ni miungu watu. Interview mithili ya Ruto leo kama ingekuwa kwetu Samia angechagua maswali ya kuulizwa na angeenda na majibu yake. Na ingekuwa marufuku kwenda nje ya script kwa waandishi.

Rejea interview ya Samia na Kikeke jinsi Samia alivyomkaripia Kikeke kama mtoto kisa kaulizwa swali asilokuwa na jibu nalo.

Tanzania tuna safari ndefu mno na Kenya daima watatuona vituko.
 
U
Una zungumzia watangazaji au waandishi wa habari?
 
Wewe mbona unalia kwenye uzi wangu?

Unataka mabadiliko ila hutaki kuwa chanzo cha hayo mabadiliko. Kama unaona watanzania hawachukui hatua anza wewe kuchukua hiyo hatua. Kulialia won't change anything and nobody is here to save you. Change starts with you. Au hamia Kenya wameshakufanyia mabadiliko wewe ni kufika tu na kudandia bandwagon.
 
Lakini mbona kama hawakuwa na usawa? Walikuwa very biased, hawampi Mh Rais nafasi nzuri ya kujieleza. Yani walikuwa na majibu yao tayari. Hayakuwa mahojiano fair.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…